CHA KUTUMAINI SINA, Swahili Lyrics. (My hope is built on nothing less)
Tenzi hii iliandikwa na mchungaji wa kanisa la kipatisti, aliyeitwa Edward Mote, raia wa nchi ya uingereza, mnamo mwaka 1834, Edward Mote alifanikiwa pia kuandika tenzi nyingine nyingi Zaidi ya 100, lakini iliyopata umaarufu mkubwa ni hii ijulikanayo kama “Cha Kutumaini sina”.
Tenzi hii aliibuni akirejea ule mfano alioutoa Bwana Yesu wa mjenzi mwenye akili aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba imara, Na yule mpumbavu ambaye aliijenga nyumba yake juu ya mchanga (Mathayo 7:24-27), Na kuonyesha ni jinsi gani mtu anapaswa aishi kwa kwa kumtegemea Kristo aliye mwamba salama, na ulio imara.
1Wakorintho 10:4 “wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo”
Na ndio hapo akaundika wimbo huu;
Cha kutumaini sina
Ila damu yake Bwana,
Sina wema wa kutosha
Dhambi zangu kuziosha;
Kwake Yesu nasimama,
Ndiye mwamba; ni salama
Ndiye mwamba ni salama
Njia yangu iwe ndefu
Yeye hunipa wokovu;
Mawimbi yakinipiga
Nguvu zake ndiyo nanga.
Kwake Yesu nasimama,
Ndiye mwamba; ni salama
Ndiye mwamba ni salama
Damu yake na sadaka
Nategemea daima,
Yote chini yakiisha,
Mwokozi atanitosha.
Kwake Yesu nasimama,
Ndiye mwamba; ni salama
Ndiye mwamba ni salama
Nikiitwa hukumuni,
Rohoni nina amani;
Nikivikwa haki yake
Sina hofu mbele zake.
Kwake Yesu nasimama,
Ndiye mwamba; ni salama
Ndiye mwamba ni salama
*****
Amen hata mimi na wewe, tukiwa ndani ya Kristo, tupo salama wakati wote, lakini tukimkosa yeye ndani yetu, basi hata kuimba kwetu ni bure, tutakuwa tu sawa na yule mpumbavu aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga..
Hivyo ukiwa unahitaji kuokoka ili Yesu leo awe kweli Mwamba ulio salama, basi fungua hapa kwa sala ya toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo ya biblia kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
MWAMBA WENYE IMARA
MWAMBA WETU.
TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.
KIFO CHA MTAKATIFU PERPETUA NA FELISTA.
WINGU KUBWA LA MASHAHIDI.
TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI.
https://wingulamashahidi.org/2018/06/27/2-swali-kwanini-mtu-atoe-pepo-aombee-wagonjwa-wapone-asikie-sauti-ya-mungu-ikimwambia-hiki-na-kile-kuhusu-watu-na-yeye-mwenyewe-kufunua-siri-za-mioyo-yao-aone-maono-na-kutembea-na-malaika-katika/
About the author