Kamsa ni nini kwenye biblia? (Sefania 1:16, Wimbo 3:8)

Kamsa ni nini kwenye biblia? (Sefania 1:16, Wimbo 3:8)

Kamsa ni nini?


Kamsa ni Ukelele wa habari ya moto au vita (kwa lugha ya kiingereza-Battle cries)

Vifungu hivyo vinaeleza Neno hilo;

Wimbo 3:8 “Wote wameshika upanga, Wamehitimu kupigana; Kila mtu anao upanga wake pajani Kwa hofu ya KAMSA ZA USIKU”.

 

Sefania 1:15 “Siku ile ni siku ya ghadhabu, Siku ya fadhaa na dhiki, Siku ya uharibifu na ukiwa, Siku ya giza na utusitusi, Siku ya mawingu na giza kuu,

16 Siku ya tarumbeta NA YA KAMSA, Juu ya miji yenye maboma, Juu ya buruji zilizo ndefu sana.

17 Nami nitawaletea wanadamu dhiki, hata watakwenda kama vipofu, kwa sababu wamemtenda Bwana dhambi; na damu yao itamwagwa kama mavumbi, na nyama yao kama mavi.

18 Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya Bwana; bali nchi yote pia itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, ukomo wa kutisha”.

Unaona? Ile siku kuu ya Bwana imefananishwa na ya kama kelele za vita..ambazo huwa zinatokea ghafla..Mfano tu wa Wana wa Israeli walivyozizunguka zile kuta za Yeriko kwa muda wa siku 7 na siku hiyo hiyo ya saba, wakapiga kelele kubwa sana (Kamsa) kuashiria kuwa vita vimeanza..

Na baada ya kilele kutoka, zile kuta za Yeriko zilizama chini saa ile ile, na biblia inatuambia mioyo ya watu wa Yeriko ikayeyuka (Yoshua 5:1) wakaishiwa nguvu kabisa.

Yoshua 6:20 “Basi watu wakapiga kelele, na makuhani wakazipiga tarumbeta; hata ikawa, hapo watu waliposikia sauti ya tarumbeta hao watu wakapiga kelele kwa sauti kuu sana, na ule ukuta wa mji ukaanguka nchi kabisa, hata watu wakapanda juu, wakaingia katika mji, kila mtu akiendelea kukabili mbele; wakautwaa huo mji.

21 Basi wakaangamiza kabisa vitu vyote vilivyokuwa ndani ya mji, wanaume na wanawake, watoto na wazee, na ng’ombe, na kondoo, na punda, kwa makali ya upanga”.


Ndivyo itakavyokuwa katika siku ule ya Mwisho Kristo atakapotokea mawinguni na malaika zake watakatifu.. Tarumbeta na Kamsa italia kutoka mbinguni, kuashiria kuwa mwisho wa kila mwenyewe dhambi umefika..

Siku hiyo kila jicho litamwona, na mataifa yote wataomboleza kwa kilio kisichoweza kuelezeka, lakini hiyo  haitasaidia, waovu wote watakuwa kama mizoga juu ya dunia nzima. Ndugu tusitamani tuwepo katika hicho kipindi kibaya sana.

Soma Ufunuo sura ya 19 na 20 yote uone jinsi waovu watakavyoangamizwa na Bwana mwenyewe siku hiyo ikifika.

Swali ni Je! Na wewe unataka uwepo huo wakati? Mimi sitaki, Kumbuka mpaka hayo yote yatokee unyakuo utakuwa umeshapita. Watakaoshuhudia hayo ni wale wote ambao hawakwenda katika unyakuo, watakaopokea chapa ya mnyama.

Ili kufahamu kwa marefu juu ya kalenda  ya matukio yote ya siku za mwisho, angalia vichwa vya masomo mengine chini.

Hivyo tubu dhambi zako kama bado wewe ni mwenye dhambi, hizi ni siku za mwisho kweli kweli , siku za Kamsa za Mungu  mwenyezi.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

SIKU YA HASIRA YA BWANA.

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!

CHUKIZO LA UHARIBIFU

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments