Juya ni nini kwenye biblia? (Mathayo 13:47)

Juya ni nini kwenye biblia? (Mathayo 13:47)

Juya maana yake ni jarife, au wavu wa kuvulia samaki.

Habari hiyo inapatikana kwenye vifungu hivi vya maandiko;

Habakuki 1:13 “Wewe uliye na macho safi hata usiweze kuangalia uovu, wewe usiyeweza kutazama ukaidi, mbona unawaangalia watendao kwa hila; na kunyamaza kimya, hapo mtu mwovu ammezapo mtu aliye mwenye haki kuliko yeye;

14 na kufanya wanadamu kuwa kama samaki wa baharini, kama vitu vitambaavyo, ambavyo havina mtawala?

15 Yeye huwatoa wote kwa ndoana yake, huwakamata katika wavu wake, na kuwakusanya katika JUYA lake; ndiyo sababu afurahi na kupendezwa.

16 Kwa sababu hiyo huutolea wavu wake sadaka, na kulifukizia uvumba JUYA lake; kwa sababu kwa vitu vile fungu lake limenona, na chakula chake kimekuwa tele.

17 Je! Atawatoa walio katika wavu wake, asiache kuwaua watu wa mataifa daima”?

Na katika agano jipya Bwana Yesu aliutumia pia mfano wa Juya la mvuvi kufananisha na jinsi mwisho wa dunia utakavyokuwa.

Mathayo 13:47 “Tena ufalme wa mbinguni umefanana na juya, lililotupwa baharini, likakusanya samaki wa kila namna;

48 hata lilipojaa, walilivuta pwani; wakaketi, wakakusanya walio wema vyomboni, bali walio wabaya wakawatupa.

49 Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki,

50 na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno”.

Lakini ni ujumbe gani mkubwa tunaupata kwenye mfano wa  Juya?

Hapo katika mfano wa Yesu tunaona walivuliwa samaki wa aina zote na kupelekwa nje kabisa ya pwani, ikiashiria kuwa wanadamu wote watavunwa ile siku ya mwisho, wawe ni watakatifu wawe ni waovu wote watavunwa, maana yake ni kuwa kila mmoja wetu atahusika, tutatolewa kwenye huu ulimwengu wa sasa, na hapo ndipo walio wema wataenda mbinguni kwa Mungu na wale walio waovu watatupwa katika ziwa la moto.

Na kibaya zaidi siku zenyewe ndio hizi tuishizo. Wakati wowote paraparanda italia, na mwisho utafika, Je bado upo vuguvugu, bado unautumaini ulimwenguni usiodumu milele?.

Kama wewe ni mwenyewe dhambi na unataka leo Yesu ayaokoe maisha yako. Ili ikitokea hata mwisho umefika leo, uwekwe kapuni mwa Bwana, basi uamuzi huo ni mzuri sana. Kumbuka biblia inasema saa ya wokovu ni sasa, Na wakati uliokubalika ni huu.

Kama ni hivyo fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba na Mungu akubariki  >>>> SALA YA TOBA

Tazama pia maneno mengine ya biblia chini.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

LAKINI USIKU WA MANANE, PAKAWA NA KELELE.

UMEFUMBULIWA MACHO YAKO YA KIROHO?

UNYAKUO.

https://wingulamashahidi.org/ikabodi-maana-yake-ni-nini/

Biblia inamaanisha nini inaposema “Tusitweze unabii”?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
5 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Daudi Sagara
Daudi Sagara
2 years ago

Mbarikiwe sana

Anonymous
Anonymous
2 years ago

Amina umejibu swar langu kabra sijakuuliza ubalikiwe