Silaha za Mkono wa kuume na za mkono wa kushoto ni zipi

Silaha za Mkono wa kuume na za mkono wa kushoto ni zipi

SWALI: Katika 2Wakorintho 6:7, Hizo Silaha za Mkono wa kuume  na za mkono wa kushoto ni zipi?


JIBU: Tusome,

2Wakorintho 6:7 “katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za haki za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto”

Mkono wa kuume ni mkono wa kulia, Hivyo kulingana na hilo andiko zipo silaha za mkono wa kulia na za mkono wa  kushoto. Lakini kiuhalisia zipo silaha za miguuni pia, na za kifuani na za kichwani..Lakini hapa tutakwenda kuzizungumzia hizi za mikononi tu, maana ndizo zilizotajwa hapa.

Sasa swali hizo silaha ni zipi?

Jibu tunalipata katika kitabu cha Waefeso.

Waefeso 6:13 “Kwa sababu hiyo twaeni SİLAHA zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.

14  Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,

15  na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani;

16  zaidi ya yote MKİİTWAA NGAO YA İMANİ, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.

17  Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na UPANGA WA ROHO ambao ni neno la Mungu”

Ukimsoma vizuri huyu Askari utaona Kashika UPANGA mkono mmoja na Mkono wa pili kashikilia NGAO. Sasa hizo mbili “Ngao pamoja na Upanga” ndio silaha za mkono wa kuume na kushoto.

Biblia imeelezea hapo Ngano ni nini? Kwamba ni Imani,..Maana yake ni kwamba Imani ni silaha, na inafungiwa mkononi, maana yake haipaswi kuangushwa hata kidogo, tukiwa nayo hiyo, tuna uwezo wa kuizima mishale yote ya adui shetani, Vile vile kwa Imani tunaweza kufanya mambo yasiyowezekana Kulingana na Waebrania 11.

Na pia biblia imeelezea Upanga ni nini? Kwamba ni Neno la Mungu..Tukiwa na Neno la Mungu la kutosha ndani yetu, shetani na majeshi yake hawatatuweza kamwe. Tutamkata na majeshi yake vipande vipande, kwasababu tunalijua Neno.

Waebrania 4:12 “Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.

13  Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu”

Hivyo IMANI na NENO LA MUNGU, ni pacha, wanakwenda pamoja…na vyote vinashikiliwa mkononi na si miguuni, na vinategemeana…kama biblia inavyosema katika Warumi…

Warumi 10:17 “Basi İMANİ, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa NENO LA KRİSTO”.

Umeona hapo? Hizo ndio silaha mbili za Mkono wa kuume na kushoto.

Je! Na wewe unazo?..Kumbuka hizo huwezi kusema unazo kama hujawa askari, na lazima kuwe na vita mbele yako?. Kama hakuna vita vyovyote vya kiimani unavyopambana basi wewe bado sio askari, hauhitaji ngao wala upanga mikononi mwako. Kama unakwenda disko, au bar au kujiuza…Ngao ya nini hapo? Unakinga nini kutoka kwa yule adui? Katika roho mikono yako inaonekana imebeba matatizo tu.

Lakini unapokuwa mkristo kweli kweli na kuacha mambo yote ya dunia, hapo wewe ni askari tena unayeogopeka katika ulimwengu wa adui shetani, Na pia ndio unayewindwa zaidi, hivyo inakugharimu kukisha kila wakati ili usipatikane na madhara.

Bwana atujalie tuwe maaskari wa bora wa Kristo, huku tumevaa silaha zote za haki.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

MASOMO MBALIMBALI YA NENO LA MUNGU.

Je! Kusoma biblia kwenye simu ukiwa kanisani ni dhambi?

Je! habari ya Yusufu, inabeba ujumbe gani kwa agano jipya?

KUOTA UMECHOMWA KISU/KUOTA UMEPIGWA RISASI.

NENO LA MUNGU NI NINI?.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Letcia Alphonce
Letcia Alphonce
2 years ago

Asante sana