Kabari ni nini kwenye biblia?(Yoshua 7:21,24)

Kabari ni nini kwenye biblia?(Yoshua 7:21,24)

Kabari ni nini?


Kabari ni ni kipande kikubwa cha kitu Fulani aidha mbao, chuma,  dhahabu, shaba n.k.. (donge)

Katika biblia tunaona wana wa Israeli walipoingia nchi ya ahadi na kuwepo maagizo kuwa vitu vyote vya thamani watakavyovikuta kule vitatolewa wakfu kwa Bwana(Yoshua 6:19), lakini tunaona walipofika kulikuwa na mtu mmoja aliyeitwa Akani, mwana wa Karmi, huyu alipofika tu aliyeingiwa na tamaa, pale alipoona vitu vya thamani, ikiwemo hizi kabari (vipande) vya dhahabu, hakuvithaminisha kwa Bwana, bali alikwenda kuvificha(Yoshua 7:11).

Akasababisha mpaka taifa zima la Israeli kupigwa na kufadhaishwa mbele ya maadui zao. Hiyo ikawafanya wapepeleze tatizo ni nini, ndipo walipogundua kuwa ni huyu Akani ameficha baadhi ya vitu vya thamani walivyovikuta kule, hivyo wakamkamata na kumuua.

Yoshua 7:21 “Nilipoona katika nyara joho nzuri ya Babeli, na shekeli mia mbili za fedha, na kabari YA DHAHABU, uzani wake shekeli hamsini, basi nalivitamani nikavitwaa; tazama, vimefichwa mchangani katikati ya hema yangu, na ile fedha chini yake…..

24 Kisha Yoshua, na Israeli wote pamoja naye, wakamtwaa Akani, mwana wa Zera, na ile fedha, na Lile joho, na ile KABARI YA DHAHABU, na wanawe, na binti zake, na ng’ombe zake, na punda zake, na kondoo zake, na hema yake, na vitu vyote alivyokuwa navyo, wakavileta juu hata bonde la Akori”.

Hiyo inatufundisha nini? Inatufundisha kuwa tusiwe na tamaa ya mali ikiwa sisi ni watoto wa Mungu, kwani haitatugharimu maisha yetu tu, bali itagharimu kama sio kuathiri na maisha ya wengine pia. Na ndio maana biblia inasema,

1Timotheo 6:10 “Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi”.

Bwana atusaidie, tupende kujikusanyia  zaidi kabari za ufalme wa mbinguni kuliko hizi za hapa duniani..Kwani za hapa duniani ni za kitambo tu, lakini zile zinadumu milele.

Shalom.

Tazama tafsiri ya maneno mengine chini.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Mkatale ni nini katika biblia? (Matendo 16:24)

Daawa ni nini kama tunavyosoma katika biblia?

Kwanini Yesu Kristo ni mwana wa Adamu?

FANYIKA SIPORA WA KRISTO, UNYAKUO UPO KARIBU.

JIEPUSHE NA UNAJISI.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments