Je! tunapaswa kukiamini Kitabu cha Henoko?

Je! tunapaswa kukiamini Kitabu cha Henoko?

SWALI: Kitabu cha Henoko ndio kitabu kipi hicho, Je! Sisi kama wakristo tunapaswa kukiamini?


JIBU: Kitabu cha Henoko ni moja ya vitabu vya Apokrifa ambavyo viliandika kati ya miaka 200 kabla ya Kristo(KK), na  miaka 400 baada ya Kristo(WK). Vitabu hivi  vinaaminiwa na baadhi ya wakristo kuwa  vilihifadhiwa kwa siri, kutokana na kuwa vilikuwa na siri za ndani sana kuhusu Mungu na historia ya ulimwengu kwa ujumla, kiasi kwamba havikuweza kujumuishwa moja kwa moja kwenye biblia yenye vitabu 66 ambayo tunayo hivi sasa.

Lakini si kweli, vitabu hivi havikujumuishwa katika biblia takatifu kwasababu vilikuwa na siri za Mungu hapana badala yake vilionekana kujaa habari nyingi za kutungwa, ambazo zinakinzana na misingi ya imani ya Kikristo.

Sasa tukirudi katika hichi kitabu cha Henoko, kiligunduliwa kwenye miaka ya 1700 huko Ethiopia, baadaye kikasafirishwa mpaka Uingereza kwa ajili ya kutafsiriwa katika lugha nyingine, Kitabu hichi kilijulikana kama Henoko wa  Kwanza (1Henoko), kwasababu kulikuja kuwa pia na matoleo mengine yaliyofuata baadaye.

Vipande vya nyaraka vya kitabu hichi pia viligunduliwa huko Israeli mnao mwaka 1947, kwenye mapango yalikuwa katika fukwe za bahari ya chumvi (dead sea), Na kwenye mapango hayo kulionekana pia machapishi ya vitabu vyote vya agano la kale isipokuwa tu kitabu cha Esta, inasadikika ni vitabu ambavyo vilikuwa vimehifadhiwa huko na watu wa kale ambao waliishi kabla hata ya Kristo kuja duniani.

Sasa kitabu hiki kinamueleza Henoko ambaye alikuwa ni mtu wa saba kutoka Adamu kama tunavyosoma katika biblia Mwanzo 5:18-24…Henoko hakuonja mauti kama ilivyokuwa kwa wanadamu wengine, bali alinyakuliwa kama Eliya. Hiyo imekuwa ikawafanya watu wengi waamini kuwa mtu huyu alipewa siri nyingi za rohoni na kuziandika kwa ajili ya watu wa baadaye.

Hivyo kitabu hichi kilipogunduliwa, kilidhaniwa  kuwa mwandishi wake  ni Henoko, japo hilo jambo halikuthibitika kuwa ni kweli. Kitabu hichi kimejaa historia zinaeleza visa vya dunia ya kwanza kugharikishwa na maji, kinasema baadhi malaika wa Mungu  ambao walikuwa ni waangalizi wa huku ulimwenguni, ambao idadi yao ilikuwa ni 200 waliwaona binti za wanadamu, kisha wakawatamani, , hivyo wakashauriana washuke duniani wajitwalie wake, waishi nao, na kweli wakafanya hivyo  wakashuka duniani wakawapa mimba wanawake, ndio wakazaa wale majitu ambayo tunayasoma katika Mwanzo 6

Zaidi ya yote, malaika hawa kwa kuwa walikuwa na ujuzi, wakawafundisha wanadamu, kubuni silaha za chuma, kufanya uharibifu, wengine wakawafundisha wanadamu kufanya uchawi, na wengine kusoma nyota za mbinguni. Pamoja na hayo watoto wao waliowazaa wakawa wakatili kupita kiasi, ndio wale wanefili, wakawa wanaharibu kila kitu ikiwemo mimea, wanyama, mpaka wanadamu. Urefu wa majitu hayo ulikuwa ni futi 4500, sawa na Jengo la ghorofa 415. Jambo ambalo ni ngumu kusadikika,  Hakuna kiumbe cha namna hiyo kinaweza kuzaliwa na mwanamke. Japo wanefili kweli walikuwa ni wakubwa lakini sio kwa kiwango hicho.

Baadaye baadhi ya malaika wa mbinguni wakampelekea Mungu habari zao,  lakini Mungu akakataa kuwasamehe, akawafunga katika vifungo vya giza, ndio hapo Mungu akamwambia Henoko kuwa atakwenda kuiangamiza dunia kwa gharika.  Hii ndio habari ambayo inafahamika sana

Zipo habari nyingine katika kitabu hicho ambazo kiuhalisia hazina uhalisia wowote  na maandiko.

Tunapaswa tujue vitabu hivi vimejaa hadithi nyingi za kutungwa, ambazo ni sumu kwa Mkristo, na ndio maana huwezi kuziona vikijumuishwa katika biblia yenye vitabu 66 vilivyovuviwa na Roho Mtakatifu, kwasababu vinakinzana na misingi ya kweli ya maandiko.

Bwana Yesu alisema..

Mathayo 22:29 “Yesu akajibu, akawaambia, Mwapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu.

30 Kwa maana katika kiyama hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika mbinguni”.

Unaona? Hakuna andiko lolote linaloonyesha kuwa malaika wanaoa, au wanazaliana, malaika hawakuumbiwa viungo vya uzazi kama tulivyonavyo sisi, hawahitaji kuzaliana, wao tayari walishaumbwa, ndivyo walivyo na idadi yao tayari ipo kamili, Lakini kusema walishuka duniani, ni fundisho la uongo ambalo wakristo wengi wanaliamini mpaka leo, na chanzo chake walikitoa katika hichi kitabu cha Henoko.

Waliowaona binti za wanadamu wakawatamani, walikuwa ni watakatifu wa Mungu, ambao hao hawakujichanganya na mambo ya ulimwengu tangu mwanzo, bali walitumia sehemu kubwa ya maisha yao, kuliita jina la Bwana na kumwabudu Mungu soma Mwanzo 4:26 utalithibitisha hilo ndio ule  uzao wote wa Sethi (Wakina Henoko, Methusela, Na Nuhu).. Lakini binti za wanadamu walikuwa ni watu wa kidunia tu, ambao walitokea katika ule uzao wa Kaini..hao ndio tangu mwanzo walikuwa na ujuzi mkubwa, na hodari na pia wakatili ukisoma pale Mwanzo 4:16-23 utaona ni jinsi gani, uzao wa Kaini ulivyokuwa hodari, wenye ujuzi mwingine, lakini pia mwovu kwa uuaji, kama Baba yao alivyokuwa.

Baadaye sasa walipojichanganya mbegu ndipo Mungu akakasirika, akaghahiri na kuuangamiza ulimwengu wote, ni sawa na leo hii, Mungu aone, watakatifu wake wote, wanaiga na kufanya mambo ya ulimwengu, wanawake wanavaa vimini, wanatembea nusu uchi barabarani, wanaume watakatifu wanakuwa mashoga n.k. kiasi kwamba huwezi kuona tofauti yoyote kati yao na ulimwenguni, hapo kinachofuata ni Mungu kuuteketeza ulimwengu, ndivyo ilivyokuwa kwa watu wa kipindi kile. Watakatifu walijitofautisha kabisa na wana wa ulimwengu..

Hivyo hakuna sababu ya mkristo kuamini, moja kwa moja vyanzo ambavyo havipo katika biblia, kwasababu vingi kati ya hivyo vinakasoro nyingi na vimejaa hadithi nyingi zilizotungwa na wanadamu lakini sio kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu.

Kwamfano kwasasa Kanisa Katoliki, limeamua kuchukua baadhi ya hivi vitabu vya Apokrifa na kuviongezea kwenye biblia takatifu yenye vitabu 66, kufikia 73. Vitabu vyenyewe ikiwemo Yudithi, Baruku, Yoshua bin Sira, Wamakabayo 1&2,  Hekima.

Vitabu hivi vinakinzana na misingi ya imani, kwamfano, vinafundisha kwenda toharani, yaani mtu mwenye dhambi anaweza kwenda mbinguni tena, lakini baada ya kupitishwa mahali panapoitwa toharani ili kutakaswa,.,Fundisho lingine ni kuwa Mungu, anasikia maombi ya wafu, mambo ambayo ni uongo, biblia inasema, mtu ameandikiwa kuishi mara moja na baada ya kifo ni hukumu (Waebrania 9:27).

Kwahiyo, vitabu vya Aprokifa, sio vya kuviamini, kama uaminivyo biblia, iwe ni kitabu cha Henoko, au kingine chochote kile nje ya vitabu 66 vya biblia sio vya kuiamini vinamakosa mengi na wakati mwingine vimejaa uongo mwingi, ambao unapotosha kabisa.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Kitabu cha YASHARI kinachozungumziwa katika 2Samweli 1:17-18, ni kitabu gani?

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1

Chuo cha vita vya Bwana ni kipi?(Hesabu 21:14)

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 7 (Yeremia na Maombolezo)

UNYAKUO.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

9 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Bernad Mpangala
Bernad Mpangala
1 year ago

Sasa mimi nina Hoja tata. Musa tumesoma vitabu vyake vitano vinavyomhusu ingawa inaonekana ALIKUFA ila kaburi lake hakuna anayejua ni Siri yao na Mungu……… Eliiya hakuna asiyefahamu habari zake ameandikwa sana kwenye wafalme…….lkn ajabu ni kwamba wajanja walizuia na kuondoa historia ya Henoko ambapo Kuna kitabu chake kinaitwa ufunuo wa henoko Mwanzo 5:21-24 “Henoko akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela. Henoko akaenda pamoja na Mungu, baada ya kumzaa Methusela miaka mia tatu, akazaa wana waume na wake. Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na mitano. Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu Alimtwaa” Halafu eti mtu aliyetembea na Mungu vizuri na akatwaliwa halafu asiwe na historia namna alivyokwenda na Mungu?

Ukisoma Waraka wa Yuda 1:14-16
Ndio utaona Kulikuwa na kitabu cha henoko na yuda anesoma Sana hiki kitabu anaposema
“Na Henoko mtu wa saba baada ya Adamu, aitoa maneno ya Unabii juu ya hao, akisema, angalia Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu, maelfu, ili afanye hukumu juu ya watu wote na kuwaadhibisha wote, wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote za upotevu walizozitenda, bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote, ambayo hao wenye dhambi, wasiomcha Mungu wameyanena juu yake. Watu hawa ni wenye kunung’unika wenye kulalamika, waendao kwa tamaa zao, na vinywa vyao vyanena maneno makuu mno ya kiburi, wakipendelea watu wenye cheo kwa ajili ya faida”.

Hii inaonyesha kabisa mtume yuda amenukuu maneno ya henoko toka kwenye ufunuo wa henoko lkn wajanja wakautoa..

Ayubu Michael Gabriel
Ayubu Michael Gabriel
1 month ago

Nahisii kuna vitu vingii sana vya siri vimo kwenye kitabu cha henoko ,,, lakn kwa ajiri ya kujifunza ni vyema tukisome tujifunze

Anonymous
Anonymous
2 years ago

Ila hata yeye mbona kama anekisoma kwanza..!

PETER SARAKIKYA
PETER SARAKIKYA
2 years ago

NATAMANI NIKIPATE KITABU CHA HENOKO NIKISOME

Anonymous
Anonymous
2 years ago

Lakini mwalimu hapo juu kasema hakifai

Olomy
Olomy
10 months ago
Reply to  Anonymous

Si ni lazima tukisome ili tufanye maamuzi wenyewe kama kina faa au hakifai

Cristin Mongi
Cristin Mongi
5 months ago

Nina hitaji kitabo cha henoko nikisom

Ayubu Michael Gabriel
Ayubu Michael Gabriel
1 month ago
Reply to  Cristin Mongi

Ikiwezekana ukikipata naomba msaada piaa nikisome