JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 2)

JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 2)

Tumetazama, wapo watu ambapo siku ile ya hukumu, watalipwa thawabu sawa na wale ambao wameteseke Maisha yao yote katika kumtumikia Mungu. Na kigezo chenyewe kwanini Mungu afanye hivyo, tumeshakiona katika maandiko, ikiwa hujapata uchambuzi wake, tutumie ujumbe, inbox tukutumie..

Tutaendelea, na vigezo cha pili cha thawabu, za Mungu. Hichi tunakisoma katika Mathayo 24:44-51

2) Kwamba wapo watu watawekwa juu ya kazi yote ya Mungu, mbinguni.

Unaweza kujiuliza, Je! Inamaana kuna watu ambao hawatawekwa, juu ya kazi za Mungu siku ile? Jibu ni ndio, twende moja kwa moja katika Habari hii, tuone ni kigezo gani, Kristo anakitumia, katika kutoa thawabu kama hiyo.

Mathayo 24:44 “Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja.

45 Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake?

46 Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo.

47 Amin, nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote.

48 Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia;

49 akaanza kuwapiga wajoli wake, na kula na kunywa pamoja na walevi;

50 bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua,

51 atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno”.

Katika Habari hiyo, tunaona, mtu mmoja Tajiri aliondoka bila kutoa taarifa ya lini atarudi, lakini akamwacha mtumwa wake mmoja awe mwangalizi wa watu wake, ahakikishe anawahudumia, pasipo kusimamiwa. Lakini anasema kama mtumwa huyo atadhani kuwa Bwana wake atachelewa. akaanza kuwa mzembe, mara hawapi watu chakula, mara anawapiga, mara anaamrisha vibaya. Siku asiyodhani atakuja, na kumkata vipande vipande.

Lakini akimkuta yupo katika majukumu yake, basi ameahidi, kuwa atamweka juu vitu vyake vyote.

Leo hii kama wewe ni mtumishi wa Mungu, aidha mchungaji, nabii, mwalimu, mtume, mwimbaji, au unafanya kazi yoyote ile ya kuujenga ufalme wa Mungu..Fahamu kuwa Bwana anataka kukuona, wakati wote, muda wote, ukitumika kwa uaminifu katika hiyo kazi, ili siku atakapokujia ghafla (aidha kwa kifo au unyakuo ) akukute katika utumishi wako.

Lakini ukianza kuidharau kazi ya Mungu na kuigeuza kama vile biashara, hutaki kutumika mpaka ulipwe, hutaki kusimamia kundi lako kama mchungaji, unazini na washirika,  hutaki kuwafundisha watu kama mwalimu, unaona uvivu wa kuwahubiria wengine Habari njema, kama mwinjilisti, unamgeuza Mungu kama mtu baki, unamtumikia tu pale unapojisikia, ukiwa huna mudi, unaendelea na mambo yako.

Ndugu, thawabu kama hii itakupita, Kazi ya Mungu inapasa iwe ni sehemu ya Maisha yako, ikiwa umeitwa kweli na Bwana, usiruhusu mapengo pengo yasiyokuwa na lazima yakusonge, mpaka kusudi lote liyeyuke ndani yako.

Lakini ukisimama katika nafasi yako, kama vile, huyu ambaye Bwana Yesu alimzungumzia hapo kwamba alimkuta anawapa watu wake chakula kwa wakati, aliahidi kumweka juu ya kazi yake yote.

Katika huo ufalme wa milele unaokuja huko, zitakuwepo kazi na majukumu, na hivyo, tangu sasa Bwana anatafuta watakaozisimamia kama viongozi kazi hizo za kimbinguni tukufu sana. Na watakaopewa nafasi hizo za kipekee ni wewe na mimi endapo tutakuwa tunagawa posho la Bwana kwa wakati.

Hivyo tuamke, kama tulikuwa tunalegea mahali, tuanze kuitenda kazi ya Bwana kwa bidii mpya.

Bwana akubariki.

Usikose mwendelezo..

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 1)

JINSI YA KUSOMA BIBLIA.

JINSI YA KUEPUKA KUUMIZWA MOYO KUSIKOKUWA NA SABABU.

MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA FILEMONI.

REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
2 years ago

AMEN, UBARIKIWE SANA MTUMISHI WA MUNGU KWA MAFUNDISHO MAZURI YA MUNGU