JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 3)

JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 3)

Shalom, huu ni mfululizo, wa Makala ambazo zinaeleza vigezo ambavyo Mungu, atavitumia kuwapa watu wake thawabu mbalimbali, au atakavyovitumia kuwakaribisha katika ufalme wake, hii ni sehemu ya tatu, ikiwa hukupitia sehemu zilizotangulia utatumia ujumbe inbox tukutumie chambuzi zake.

3) Biblia inatuonyesha kuna watu watu wataingizwa katika ufalme wa Mungu, bila kutambua sababu.

Inashangaza lipo kundi la watu ambalo litapewa neema ya kuungia ufalme wa Bwana wetu Yesu Kristo, bila lenyewe kutambua sababu mpaka litakapofunuliwa na Kristo mwenyewe siku ile.

Tunalisoma kundi hilo katika vifungu hivi.

Mathayo 25:31 “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;

32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi;

33 atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto.

34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;

35 kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha;

36 nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia.

37 Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha?

38 Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika?

39 Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia?

40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.

41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;

42 kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe;

43 nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama.

44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie?

45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.

46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele”.

Kundi hili, ni lile, lilowahifadhi, watumishi wa Kristo, wakiwa hapa duniani, wasijue kuwa walikuwa wanamtendea Kristo mwenyewe, hapa hazungumzii maskini, na omba omba, au  mayatima hapana, wanaowahudumia hao wanayothawabu yao, ambayo tutaiona katika Makala inayofuata, bali wanaozungumziwa hapa ni watakatifu wa Bwana, ambao kutokana na maisha yao ya  utumishi, walipitia kupungukiwa, kuumwa, kukosa chakula, nguo, makazi n.k. Sasa wapo ambao waliwaona na kuwahifadhi, wasijue kuwa wanamtendea Kristo mwenyewe.

Sasa siku ile itakapofika, hawa watumishi wa Bwana watasimama na kuwataja mbele ya Kristo, na kwasababu hiyo Kristo atawapa neema ya kuuingia ufalme wake. Sawasawa na ule mfano wakili dhalimu tunaousoma katika Luka 16:1-12.

Mtume Paulo aliwaombea rehema ndugu wa mtu mmoja aliyeitwa Onesiforo, kwa jinsi walivyomtunza na kumuhudumia kwa mahitaji mbalimbali alipokuwa anahubiri.

2Timotheo 1:16 “Bwana awape rehema wale walio wa mlango wake Onesiforo; maana mara nyingi aliniburudisha, wala hakuuonea haya mnyororo wangu;

17 bali, alipokuwapo hapa Rumi, alinitafuta kwa bidii akanipata.

18 Bwana na ampe kuona rehema machoni pa Bwana siku ile. Na jinsi alivyonihudumia kwa mengi huko Efeso, wewe unajua sana”.

Vivyo hivyo, na wale ambao, wanawaona watu wanaomtafuta Mungu, ni kama mizigo kwao, wanawadhihaki, wanawatukana, wanawafukuza, hata wakiomba maji wanawaona ni wavivu. Watu ambao wanaposikia watumishi wa kweli wa Mungu ni kama kero kwa kwao, Watu kama hawa upo wakati Kristo naye atawakana.

Inatufundisha nini?, tukisema tunampenda Kristo, tunamaanisha kuwa tunawapenda na wale wampendao, kama unawachukia watakatifu, utampendaje Kristo?. Hivyo, wapo watu ambao Kristo atawakaribisha kwa namna hii,. Vilevile wapo watu ambao Kristo atawafukuza kwa namna hii. Kwasababu hawakumkaribisha Kristo kwao.

Shalom.

Usikose mwendelezo..

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 1)

JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 2)

JINSI YA KUSOMA BIBLIA.

HUTATAMBUA LOLOTE, SIKU YA UNYAKUO IKIFIKA.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments