Uchungu wa mauti ni nini, kibiblia?
Matendo 2:23 “mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu zamani, ninyi mkamsulibisha kwa mikono ya watu wabaya, mkamwua; 24 ambaye Mungu alimfufua, akiufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao.
Matendo 2:23 “mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu zamani, ninyi mkamsulibisha kwa mikono ya watu wabaya, mkamwua;
24 ambaye Mungu alimfufua, akiufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao.
JIBU: Uchungu wa mauti, ni kufa bila kuwa na matumaini ya kufufuka, yaani kuoza na kupotea kabisa, ndicho kilichowakuta wanadamu wote, waliokufa, kabla ya Kristo walioza wakapotea kabisa, roho zao zikawa zipo ardhini tu, (makao ya wafu), Lakini Bwana wetu Yesu Kristo, yeye alipokufa, hakupotelea mavumbini, wala hakuoza, bali alifufuka siku ya tatu. Akawa mtu wa kwanza, aliyekufa akafufuka, kisha akapaa mbinguni, akiishi milele.
Na ndio maana hapo biblia inasema..
“ambaye Mungu alimfufua, akiufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao”.
Walipodhani, Kristo hawezi kufufuka, mpaka wakamwekea na muhuri na walinzi kwenye kaburi lake, hilo bado halikuwezekana, alifufuka tu. Kwasababu haiwezekani, uchungu wa mauti umshike Bwana.
Hata sasa sisi, sote, tuliomwamini, tunapokufa, uchungu wa mauti hautukamati, na ndio maana siku ile Bwana alipofufuka alifufuka na watakatifu wake akawapeleka peponi, (Mathayo 27:51-53), sisi kama watakatifu tunapokufa hatulali makaburini tena, wala hatuendi jehanamu, bali tunahamishwa na kupelekwa peponi,(sehemu nzuri sana ya raha) tukingojea siku ile kuu ya ukombozi wa miili yetu, ndipo tutakapoichukua miili yetu ardhini, na moja kwa moja tutakwenda mbinguni, Bwana wetu Yesu Kristo alipo.
Lakini kama bado upo nje ya Kristo, uchungu wa mauti, ni lazima ukupate tu, kwasababu ukifa utakwenda jehanamu huko chini, kuteswa, huku ukisubiria siku ile ya ufufuo uhukumiwe, kisha utupwe katika lile ziwa la moto. Ndugu Usichukulie rahisi rahisi kifo kama wewe ni mwenye dhambi, uchungu wa mauti hauelezeki, soma ile Habari ya Tajiri na Lazaro,(Luka 16:19-31) ndipo utapata picha halisi ni nini kinawakuta watu wote, wanaokufa sasa nje ya Kristo.
Je bado unaishi katika dhambi? Bado unaishi Maisha ya uvuguvugu, kumbuka, hakuna anayejua siku yake ya kuondoka hapa duniani, Ikiwa leo ndio siku yako, Jiulize Huko utakapokwenda utakuwa mgeni wa nani?
Majibu tunayo sote mioyoni mwetu.
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Nini maana ya “Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati”
DHAMBI YA MAUTI
Wote wanaokumbwa na mauti sasa ni kutokana na dhambi zao?
KU WAPI, EWE MAUTI, KUSHINDA KWAKO?
Nini maana ya “Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea;?
Rudi nyumbani
Print this post