Rushwa inapofushaje macho?

Rushwa inapofushaje macho?

Biblia inasema rushwa inawapofusha macho hao waonao? (Kutoka 23:8) Ni kwa namna gani rushwa inaweza kumpofusha mtu macho?

Jibu: Tusome,

Kutoka 23:8 “Nawe usipokee rushwa; kwani hiyo rushwa huwapofusha macho hao waonao, na kuyapotoa maneno ya wenye haki”.

Ili tuelewe vizuri, hebu tutafakari mfano ufuatao..

Hakimu mahakamani anaona kabisa mhalifu fulani amefanya kosa linalostahili kifungo (yaani macho yake yanaona kabisa lile ni kosa alilolifanya, na anapaswa ahukumiwe kulingana na sheria)..Lakini anapopewa rushwa, palepale anajiziba macho, na kumwachia yule mhalifu, na kulifunika kosa lake.. (Sasa kitendo hicho cha hakimu kujiziba macho na kulifunika kosa, ndicho kinachoitwa kupofuka macho).. na hiyo yote ni kwasababu ya rushwa!..Laiti asingepokea rushwa angelitazama kosa na kulihukumu jinsi inavyostahili..

Ndio maana biblia inasema…“Rushwa huwapofusha macho hao waonao”..Wanaona na kujua kabisa jambo Fulani sio sawa, lakini rushwa inawafanya wasilione kama ni kosa tena..(macho yao yamepofuka!).

Na sio tu!, kuwapofusha macho hao wanaoipokea, bali pia “inayapotoa maneno ya wenye haki”.. maana yake.. wale watu wastahilio kupata haki, hawapati hiyo haki, wanaonena maneno ya haki, maneno yao yanapotoshwa kwasababu ya rushwa iliyotolewa na mwingine.

Ni mara ngapi, watu wasio na hatia wanafungwa, kwasababu tu upande mmoja umetoa rushwa?..

Biblia utaona inazidi kuliweka hilo wazi katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati..

Kumbukumbu 16:19 “Usipotoe maamuzi; wala usipendelee uso wa mtu; WALA USITWAE RUSHWA; KWA KUWA RUSHWA HUPOFUSHA MACHO YA WENYE AKILI, NA KUGEUZA DAAWA YA WENYE HAKI”.

Na sisi kama wakristo hatupaswi kupokea wala kutoa rushwa!..kwasababu rushwa ina laana nyuma yake.

Mithali 17:23 “ASIYE HAKI HUTOA RUSHWA KIFUANI, Ili kuzipotosha njia za hukumu”.

Katika biblia utaona mojawapo ya sababu iliyomfanya Nabii Samweli akubalike mbele za Mungu na watu, na kuzidi kupata kibali cha kuiamua Israeli mpaka uzee wake, ni mwenendo wake wa kutokubali Rushwa..

1Samweli 12:1 “Kisha Samweli akawaambia Israeli wote, Angalieni, nimeisikiliza sauti yenu katika hayo yote mliyoniambia, nami nimemtawaza mfalme juu yenu.

2 Basi sasa, angalieni, mfalme anakwenda mbele yenu; na mimi ni mzee, mwenye mvi; tena, tazameni, wana wangu wapo pamoja nanyi; nami nimekwenda mbele yenu toka ujana wangu hata leo.

3 NAMI NIPO HAPA; BASI, MNISHUHUDIE MBELE ZA BWANA, NA MBELE YA MASIHI WAKE,NALITWAA NG`OMBE WA NANI? AU NALITWAA PUNDA WA NANI? AU NI NANI NILIYE MDHULUMU? NI NANI NILIYEMWONEA? AU KWA MKONO WA NANI NIMEPOKEA RUSHWA INIPOFUSHE MACHO? NAMI NITAWARUDISHIA NINYI.

4 NAO WAKASEMA, HUKUTUDHULUMU, WALA HUKUTUONEA, WALA HUKUPOKEA KITU KWA MKONO WA MTU AWAYE YOTE.

5 Akawaambia, Bwana ni shahidi juu yenu, na masihi”

Umeona?..Samweli hakuwahi kupokea rushwa Maisha yake yote, na ndio ikawa sababu ya yeye kudumu katika Uamuzi wa Israeli, Lakini sasa kinyume chake, wanawe wawili aliowazaa hawakuwa kama yeye, wao walikuwa wanapokea rushwa..

Jambo ambalo liliwafanya wana hao wa Samweli kutolewa katika kiti cha Uamuzi wa Israeli, na hiyo ni kwasababu tu ya RUSHWA walizokuwa wanazipokea kutoka kwa watu..na matokeo yake ikasababisha Israeli nzima kuingia katika dhambi ya kutaka mfalme, kutokana na kwamba waliona Watoto hao wa Samweli hawafai..

1Samweli 8:1 “Hata Samweli alipokuwa mzee, aliwafanya wanawe wawe waamuzi juu ya Israeli.

2 Na jina la mwanawe mzaliwa wa kwanza aliitwa Yoeli; na jina la wa pili Abiya; walikuwa waamuzi katika Beer-sheba.

3 ILA WANAWE HAWAKUENDA KATIKA NJIA ZAKE, BALI WALIZIACHA, ILI WAPATE FAIDA; WAKAPOKEA RUSHWA, NA KUPOTOSHA HUKUMU.

4 Ndipo wazee wote wa Israeli wakakutana pamoja, wakamwendea Samweli huko Rama”

5 wakamwambia, Angalia, wewe umekuwa mzee, na wanao hawaendi katika njia zako; basi, tufanyie mfalme atuamue, mfano wa mataifa yote.

Hiyo ikitufundisha kuwa Rushwa, siku zote inatokosesha kibali mbele za Bwana na mbele za watu!…

Ukitaka udumu katika Nafasi yoyote uliyopo, ambayo ni Mungu kakuweka, basi kaa mbali na rushwa!.. ukitaka udumu katika utumishi (wa Mungu) kaa mbali na rushwa, ukitaka udumu katika kazi ya mikono unayoifanya basi kaa mbali na rushwa.. Wanadamu wengi wanaweza wasikuone unayoyafanya kwa siri, lakini Mungu anakuona, na yeye ndiye atakayekuvua hiyo nafasi..na Zaidi ya yote utakapokufa bila kuacha rushwa, basi utahukumiwa.

Ayubu 15:34 “Kwa kuwa jamii ya hao wasiomcha Mungu watakuwa tasa, NA MOTO UTATEKETEZA MAHEMA YENYE RUSHWA”.

Bwana atusaidie..

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

JE! JICHO LAKO LINAONA NINI KATIKATI YA MAJARIBU?

IELEWE SAUTI YA MUNGU.

Bwana aliposema “sikuja kutangua torati bali kuitimiliza” alikuwa anamaanisha nini?

NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?

Ni kwanini Yesu alisema Na wakisikia wasikie, wasielewe Wasije wakaongoka?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

7 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Joseph
Joseph
2 years ago

Ubarikiwe sana Kwa ujumbe mzuri

Anonymous
Anonymous
2 years ago

amen kubwa

lucas mhula
lucas mhula
2 years ago

Amen

malega
malega
2 years ago
Reply to  lucas mhula

ubarikiwe