Katika biblia (Agano la kale), kimiminika kilichokuwa kinatolewa sadaka ni “Divai” na si kitu kingine,
Walawi 23:13 “Na sadaka yake ya unga itakuwa sehemu za kumi mbili za efa za unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, ni kafara iliyosongezwa kwa Bwana kwa moto kuwa harufu ya kupendeza; na SADAKA YAKE YA KINYWAJI ITAKUWA NI DIVAI, robo ya hini”.
Unaweza kuona pia sadaka hii ya Kinywaji ikitajwa katika kitabu cha Kutoka 29:40, Kutoka 30:9, na Walawi 23:18, Hesabu 6:15, Hesabu 15:6 na Hesabu 28:17..
Sasa swali linakuja kwanini IWE DIVAI na si kitu kingine?
Sasa Sadaka ya kinywaji (Divai) iliyokuwa inapelekwa katika madhabahu haikuwa kwa kazi ya Ulevi, bali kwa matumizi ya Nishati.
Katika sheria za Musa, Bwana aliagiza pia wana wa Israeli watoe sadaka ya kinywaji, ambayo ilikuwa ni DIVAI. Na divai hiyo ilipelekwa kwa kuhani, na kuhani aliingia nayo ndani ya hema, na kuitwaa sehemu ndogo ya ile Divai, na kisha kuimimina juu ya madhahabu Pamoja na unga mwembamba, na kuwasha moto juu yake.
Asili ya sadaka hii ni wapi?
Matoleo ya sadaka ya kinywaji yalianzia kwa Yakobo kipindi alipotokewa na Mungu kule Betheli, kama vile sadaka ya Zaka ilivyoanzia kwa Ibrahimu kipindi anakutana na Melkizedeki na hatimaye ikaja kuwa sheria kwa Israeli yote. Vivyo hivyo na sadaka ya kinywaji.
Mwanzo 35:9 “MUNGU AKAMTOKEA YAKOBO TENA, aliporudi kutoka Padan-aramu akambariki.
10 Mungu akamwambia, Jina lako ni Yakobo; hutaitwa tena Yakobo, lakini Israeli litakuwa jina lako. Akamwita jina lake, Israeli.
11 Mungu akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uzidi ukaongezeke. Taifa na kundi la mataifa watatoka kwako, na wafalme watatoka viunoni mwako.
12 Na nchi hii niliyowapa Ibrahimu na Isaka nitakupa wewe, na uzao wako baada yako nitawapa nchi hiyo.
13 Mungu akakwea juu kutoka kwake mahali hapo aliposema naye.
14 Yakobo akasimamisha nguzo mahali aliposema naye, nguzo ya mawe, AKAMIMINA JUU YAKE SADAKA YA KINYWAJI, AKAMIMINA MAFUTA JUU YAKE.
15 Yakobo akapaita mahali pale, Mungu aliposema naye, Betheli.”
Sasa Sadaka ya Kinywaji inawakilisha nini katika Agano jipya?
Sadaka ya kinywaji katika Agano jipya inawakilisha damu ya YESU, ambayo ilimwagika/kumiminwa kwaajili yetu, mara moja tu! (kumbuka damu ya Yesu, inafananishwa na Divai), Bwana Yesu alilisema hilo wazi..
Luka 22:19 “Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, [Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.
20 Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, KIKOMBE HIKI NI AGANO JIPYA KATIKA DAMU YANGU, INAYOMWAGIKA KWA AJILI YENU”.
Umeona hapo! Kile kikombe (Divai) kilikuwa ni Damu ya Yesu iliyotiririka na iliyomwagika pale Kalvari, na ni ufunuo wa Ile sadaka ya kinywaji ambayo ilikuwa inamiminwa juu ya madhabahu. Na pia ni ufunuo wa meza ya Bwana.
Bwana Yesu akubariki
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Sadaka ya kutikiswa ilikuwaje?
Nini maana ya.. “Utoapo sadaka mkono wako wa kuume usijue ufanyalo mkono wako wa kushoto”
About the author