tofauti iliyopo kati ya Imani na ujasiri, ni ipi?

tofauti iliyopo kati ya Imani na ujasiri, ni ipi?

SWALI: Bwana Yesu asifiwe, naomba kufahamu tofauti iliyopo kati ya Imani na ujasiri.


Ujasiri ni ile hali ya kuweza kukabiliana na tatizo au shida, au changamoto Fulani, (uwezo wa kuushinda woga).. Ujasiri unaweza kuonekana kwa kiumbe hai chochote cha Mungu, kwamfano unaweza kuonekana kwa mtu, vilevile unaweza kuonekana kwa Simba, au mbwa, au nyoka. Pia ni hali ambayo mtu/kiumbe kinaweza kuzaliwa nao, tofauti na imani,

Lakini Imani, inatokana na Neno ‘kuamini’.. Maana yake ni kwamba huzalika kwa kutegemea, kuamini kitu kingine (Haisimami yenyewe kama yenyewe)..Na kwa kupitia hicho ndio unapata  sasa wa kutenda Neno ambalo mtu ulikuwa huwezi kulifanya. Kwamfano kwanini leo hii ukipishana na kuku barabarani hushtuki, lakini ukipishana na nyoka unaruka na kukimbia, au unachukua hatua ya kupambana naye? Ni kwasababu umeyaamini macho yako yaliyokupa taarifa kule kile ni kiumbe salama na kile ni hatari, lakini kama usingekuwa na macho matendo hayo yasingezalika. Hivyo ujasiri ni zao la imani, lakini imani haiwezi kuwa zao la ujasiri.

Na ndivyo ilivyo kwetu sisi, ili tuweze kupata IMANI timilifu. Hatuna budi tuwe na kitu cha uhakika cha kutegemea. Na hicho si kingine zaidi ya NENO LA MUNGU.. Hapo ndio mwisho wa mambo yote. Hilo ndio jicho letu la ndani tunalopaswa tulifufue, kwasababu ndio litatupa ujasiri wa kufanya mambo yote, na kutenda mambo yote yasiyowezekana kwa namna ya kibinadamu.

Na imani hii, haiji kwa njia nyingine yoyote isipokuwa kwa kulisikia Neno la Mungu biblia inasema hivyo .

Warumi 10:17 “Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo”.

Unaposoma Neno la Mungu, na kuona ndani yake, matendo makuu aliyoyofanya, ndipo unapopata Imani  sasa na wewe ya kutenda au kusonga mbele, kwamfano, wewe ni tasa, unaposoma habari za Sara na Ibrahimu, na kuona katika uzee wa miaka 100 ndio wanapata watoto, hapo na wewe utapata nguvu ya kumwamini Mungu ukijua kuwa kama aliweza kufanya kwa Sara atafanya na kwako, kwasababu yeye ni Yule Yule jana na leo na hata milele. Lakini ikiwa huijui hii habari au huitafakari mara kwa mara, imani yako haiwezi kutokea, utabakia kusema mimi ndio basi, tena siwezi kuzaa.

Daudi alipokwenda kushindana na Goliati, alitafakari jinsi Mungu alivyomshindania, akiwa porini anachunga mbuzi na kondoo, jinsi alivyoweza kuua simba na dubu. Akamwesabia Mungu kuwa anaweza pia kumsaidia kwa Yule Goliati mtu wa miraba minne, na kweli ikawa hivyo.. Halikadhalika na wewe ili uweze kutenda mambo makubwa, kufungua mambo ambayo hayawezekani kwa akili za kibinadamu, unahitaji Imani, lakini si imani kwa wanadamu au kwa vitu au kwenye mali, bali imani kwa Mungu, ambalo ndio NENO LAKE.

Penda sana, kusoma Neno, kiwe ndio chakula chako asubuhi, mchana na jioni.

Biblia inasema..

Waebrania 11:24 “Kwa imani Musa alipokuwa mtu mzima, akakataa kuitwa mwana wa binti Farao;

25 akaona ni afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa kitambo;

26 akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo.

27 Kwa imani akatoka Misri, asiogope ghadhabu ya mfalme; maana alistahimili kama amwonaye yeye asiyeonekana.

28 Kwa imani akaifanya Pasaka, na kule kunyunyiza damu, ili yule mwenye kuwaangamiza wazaliwa wa kwanza asiwaguse wao.

29 Kwa imani wakapita kati ya Bahari ya Shamu, kama katika nchi kavu; Wamisri walipojaribu kufanya vivyo wakatoswa.

30 Kwa imani kuta za Yeriko zikaanguka, zilipokwisha kuzungukwa siku saba.11.31 Kwa imani Rahabu, yule kahaba, hakuangamia pamoja na hao walioasi; kwa kuwa aliwakaribisha wale wapelelezi kwa amani.

32 Nami niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gideoni na Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii;

33 ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba,

34 walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga. Walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni.

35 Wanawake walipokea wafu wao waliofufuliwa. Lakini wengine waliumizwa vibaya hata kuuawa, wasikubali ukombozi, ili wapate ufufuo ulio bora;

36 wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani;

37 walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno, walijaribiwa, waliuawa kwa upanga; walizunguka-zunguka wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; walikuwa wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya;

Hiyo ndio tofauti kati ya imani na ujasiri.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

KIWANGO CHA TATU CHA IMANI.

ENZI NA MAMLAKA AMEZIFANYA KUWA MKOGO

NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?

KWANINI TUNAPASWA KWENDA KUIHUBIRI INJILI KWA UJASIRI WOTE?

Je!Sisi kama wakristo Tunaruhusiwa kuchangia ujenzi wa Imani nyingine?

Agano ni nini? na kuna aina ngapi za maagano?

Atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani? Maana yake nini?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Frank Nambaya
Frank Nambaya
2 years ago

Ujumbe mzuri
Ahsante