KAMA MKRISTO EPUKE KUENDEKEZA BAADHI YA DHAMBI

KAMA MKRISTO EPUKE KUENDEKEZA BAADHI YA DHAMBI

Wewe umemwaga damu nyingi,

Kuna wakati Daudi aliingiwa na wazo la kumjengea Mungu nyumba, hivyo wazo hilo likawa jema sana machoni pa Mungu, likamfurahisha sana Bwana mpaka akamwahidia Baraka tele katika ufalme wake..Lakini tunasoma Mungu alimzuia Daudi asiijenge hiyo nyumba, bali mwana wake Sulemani ndiye aje kuijenga, sio kwamba Mungu alikuwa hatamani Daudi aijenge, hapana Mungu alimpenda sana, na alikuwa kipenzi chake, lakini kulikuwa na kikwazo kilichomkwamisha..

Embu tusome…

1 Nyakati 22:7-8

[7]Daudi akamwambia Sulemani mwanawe, Kwangu mimi nia yangu ilikuwa kujenga nyumba kwa ajili ya jina la BWANA, Mungu wangu. 

[8]Lakini neno la BWANA likanijia, kusema, Wewe umemwaga damu nyingi, na vita vikubwa umevifanya; wewe hutajenga nyumba kwa ajili ya jina langu, kwa sababu umemwaga damu nyingi juu ya nchi machoni pangu; 

Sababu yenyewe Mungu ameitoa hapo kwamba Daudi “amemwaga Damu za watu wengi”..Daudi hakujua kuuwa kwakwe watu sio jambo ambalo lilikuwa linavutia machoni pa Bwana,japokuwa Mungu alikuwa pamoja naye wakati wote, hakujua kuwa kuua kule kulikuwa kunapeleka harufu mbaya mbele za Mungu aliye mtakatifu na msafi.

Hivyo wakati anapeleka ombi lake la kumjengea hekalu, Mungu akamkataza kwasababu alimuona ananuka damu za watu wengi, Na sikuzote Mungu hawezi kuruhusu mikono yenye damu, kushiriki katika kujenga vitu vitakatifu.

Ni nini  Bwana anataka tujifunze.

Sisi kama wakristo, zipo dhambi au makosa ambayo tunayazoelea kuyafanya mara kwa mara, lakini hatujui kuwa tunamkosea Mungu, wakati mwingine tunapumbazika, kuona rehema na fadhili zake zinatufuata kila mahali, lakini ndani ya mioyo yetu tunamwaga damu kila kukicha kama Daudi.

Kwamfano, katika agano jipya, hatuui kwa Upanga au kwa mkuki, maandiko yanasema..

1Yohana 3:15  “Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake.

Kitendo tu cha kuwa na chuki, na jirani yako, au ndugu yako, kumbe rohoni unatafsirika kama mwuaji, hivyo chuki hizo zinavyoendelea na kuzidi wakati baada ya wakati, zinavyozidishwa kwa watu wengine kadha wa kadha, ndivyo mtu huyo anavyoonekana anamwaga damu nyingi.

Na madhara yake utakuja kuyaona mbeleni, wakati ambapo unamwomba Mungu kibali cha kutenda jambo Fulani jema kwa ajili yake, anakuzuia, unataka Mungu atembee na wewe katika viwango Fulani vya juu, anakuzuia, kwasababu umeendekeza makosa au dhambi hizo kwa muda mrefu.

Hivyo, tunapaswa, kila inapoitwa leo, tuangalie ni wapi tumezoelea kupafanya ambapo hapampendezi Mungu, kisha tuache mara moja, ili isije kutuletea madhara mbeleni, Kama ni katika usengenyaji, tuache mara moja, kama ni katika uongo, rushwa, udhuru,wivu, manung’uniko tuache mara moja.

Bwana atusaidie

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo:

KWANINI DAUDI ALIKUWA NI MTU ALIYEUPENDEZA MOYO WA MUNGU?

EPUKA KUCHELEWA IBADA.

NAAM, HATA WABAYA KWA SIKU YA UBAYA. 

Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?

KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?

KIFAHAMU KIGEZO  CHA KUSAMEHEWA NA MUNGU.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Vinah
Vinah
1 year ago

Amen, naomba kuuliza vita vya harmagedoni vitatokea baada ya utawala wa miaka elfu moja wa Yesu Kristo duniani au kabla ya utawala huo?

Vinah
Vinah
1 year ago

Amen. Vita vya harmagedoni vitatokea baada ya utawala wa miaka elfu moja wa Yesu Kristo duniani au kabla?

Anonymous
Anonymous
1 year ago

amen, lakini kunajambo nimekuwa nikilifanya kwamuda mrefu nimekuwa niki bet lakini kuna watu kadhaa wamekua wakisema kubet ni dhambi, hivi inawezekana je ikawa dhambi? mbona kuna watu wanafanya biashara inakuwa sio dhambi wengine wanatumia pesa kwa aina nyingi inakuwa sio dhambi, kadhalika mimi ku bet tu kwenye simu ya itel (sio hata android) inaweza je kuwa dhambi, tena ninapo bet nikwenye kandanda na nipesa ndogo kama vile 500 yakikongomani au 1000 yakikongomani?