Jibu: Tusome,
Isaya 66:3 “Yeye achinjaye ng’ombe ni kama yeye amwuaye mtu; na yeye atoaye dhabihu ya mwana-kondoo ni kama yeye avunjaye shingo ya mbwa; na yeye atoaye matoleo ni kama yeye atoaye damu ya nguruwe; na yeye afukizaye uvumba ni kama yeye abarikiye sanamu; naam, wamezichagua njia zao wenyewe, na nafsi zao zafurahia machukizo yao”.
Mstari huo tukiusoma kama ulivyo ni rahisi kutafsiri kuwa “Biblia imekataza kuchinja wanyama na kula nyama”…lakini kiuhalisia hiyo sio maana yake kabisa…kwasababu kama hiyo ingekuwa ndio maana yake basi pia hapo imekataza matoleo… na tunajua matoleo ni jambo linalokubalika mbele za Mungu (Warumi 25:26).
Sasa tukisoma kuanzia ule mstari wa kwanza utaona Mungu anawakemea au kuwaonya wale watu ambao wanakusanya vingi na vikubwa na kwenda kumtolea Mungu, wakidhani kuwa Mungu anapendezwa na sadaka zao hizo kubwa na nyingi na huku mioyoni wapo mbali na Mungu.
Na utaona Bwana anazidi kusema.. “Mbingu na dunia ni mali yake, hakuna chochote tutakachoweza kumpa yeye ambacho kitakuwa cha kipekee”…ikifunua kuwa Mungu hana haja na vitu bali mioyo yetu, kwasababu kila kitu ni chake.
Isaya 66:1 “BWANA asema hivi, Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu; mtanijengea nyumba ya namna gani? Na mahali pangu pa kupumzikia ni mahali gani?
2 Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema BWANA; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu”.
Umeona?..Mtu mnyonge ndiye atakayemwangalia Bwana, mtu mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno lake…Maana yake mtu wa namna hii atakapoleta sadaka yake ndio Mungu atakayoikubali, lakini mtu mwovu na mwenye kiburi Mungu haitaki sadaka yake.
Sasa endapo mtu mwovu anayemkataa Mungu analeta sadaka yake mbele za Mungu, sadaka yake hiyo inaonekana kama ni sadaka ya hatia.
Kama akileta Ng’ombe na kumpeleka kwa Kuhani kama sadaka ya kuteketezwa, Bwana ataiona sadaka hiyo kama ni kafara ya Mtu sio ya ng’ombe, hivyo atajitafutia laana badala ya baraka.
Utaona maandiko yanazidi kulisisitiza hilo katika Mithali 15:8
.Mithali 15:8 “Sadaka ya mtu mbaya ni chukizo kwa BWANA…”
Ndio maana katika Isaya 66, Bwana anasema..
Kwahiyo tunachoweza kujifunza ni kuwa, Bwana hapendezwi na matoleo mabaya, yeye alisema kulitii Neno lake ni bora kuliko dhabihu Soma (1Samweli 15:22).
Hivyo usipeleke madhabahuni fedha haramu, fedha iliyopatikana kwa rushwa, kwa wizi, kwa uuuzaji wa vitu haramu kama bangi, pombe, sigara au hata kwa uuzaji wa mwili.
Kumbukumbu 23:18 “Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya BWANA, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yo yote; kwani haya ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako, yote mawili”
Vile vile hatupaswi kumtolea Mungu dhabihu huku hatuna mapatano sisi kwa sisi..
Mathayo 5:23 “Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,24 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako”
Bwana Yesu atusaidie.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Nyama zilizosongolewa ni zipi?Je kunywa damu ni dhambi?
HAPAKUWA NA NAFASI YA KUPITA KWA YULE MNYAMA ALIYEKUWA CHINI YANGU.
Kwanini Bwana aliwalenga mbwa na nguruwe tu katika Mathayo 7:6?
UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?
MASWALI NA MAJIBU: YAHUSUYO NDOA- Sehemu ya 2.
Rudi nyumbani
Print this post
mara nyingi nimekuwa nikijiuliza jambo hili, wakati unapo zozana na ndugu yako na baada ya masaa ma chache kila mtu akayaachilia mambo hayo(kuyasamee, kuto kuyakumbuka tena na amuja ombana msamaa)je kuna umuhimu wa kuomba msamaha tena?