USIKWEPE USHIRIKA NA MADHABAHU YA KRISTO.

USIKWEPE USHIRIKA NA MADHABAHU YA KRISTO.

Upo umuhimu wa kufanya ushirika.

Ushirika unatokana na neno kushiriki.  Na matokeo ya kushiriki ni kuambukizwa sifa au tabia ya kile kitu unachoshirikiana nacho.

Watu wengi hatujui hata Neno USHIRIKINA limetokana na neno kushiriki. Washirikina wanashiriki mambo ya kipepo, ili wapate sifa za kipepo, au waambukizwe tabia zao ndani yao na ndio maana wanaitwa washirikina. Ndio hapo utaona mtu anakwenda kwa mganga, kisha anapewa dawa Fulani anaambiwa anywe au aweke chini ya biashara yake, halafu itamfanya wateja wavutiwe na biashara yake. Mtu huyo analivuta pepo la mauti ndani yake, kwa ushirika anaoufanya kisa lile pepo linasimama pale na kushawishi watu waovu , kisha Yule mtu anapata anachokitafuta kwa muda, halafu mwisho wa siku pepo lile linageuka na kumuua,.kwasababu hatma ya shetani sikuzote ni kuchinja na kuiba. Lakini ikiwa mtu huyo hatofanya ushirikina wowote, hawezi kuwa na uwezo huo wa kipepo.

Sasa na katika Mungu ni vivyo hivyo. Unapokuwa nyumbani mwa Mungu Usiwe ni mtu wa kwenda na kutoka tu, kama mtembeleaji. Huna ushirika wowote na watakatifu wengine, huna ushirika wowote na Mungu,. Ukifanya hivyo hutakuwa na nguvu zozote au sifa au tabia zozote za ki-Mungu ndani yako.

Ushirika wa Kikristo Ni upi?

  1. Kuhudumu
  2. Meza ya Bwana
  3. Kutawadhana miguu

Kwamfano Unapohudumu, yaani unapojishughulisha na jambo Fulani ndani ya Kanisa labda kufundisha, kujitoa kwa ajili ya maendeleo ya kanisa kama kuchangia, kufagia, kujenga, kupiga deki, na vyovyote vile. Hapo ni sawa unafanya ushirika na watakatifu wengine katika kuujenga mwili wa Kristo. Na hivyo rohoni, unapokea uwezo au sifa nyingine ya ziada ambayo hapo kwanza ulikuwa huna. Na moja ya uwezo huo ni nguvu ya kuendelea mbele katika imani.

Na pia Meza ya Bwana. Huna budi kushiriki. Kwasababu hiyo inakuunganisha na Mungu moja kwa moja. Embu soma maandiko haya upate kuelewa vema;.

1Wakorintho 10:14  “Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu. 15  Nasema kama na watu wenye akili; lifikirini ninyi ninenalo.

16  Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, JE! SI USHIRIKA wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, SI USHIRIKA wa mwili wa Kristo? 17  Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja.

18  Waangalieni hao Waisraeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, je! Hawana shirika na madhabahu? 19  Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu?

20  Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani”.

Umeona? Kumbe kikombe na mkate ule ni USHIRIKA.. ambao sisi tunafanya na Mungu. Na hivyo una matokeo yake makubwa rohoni. Yesu alisema mtu asipoula mwili wangu, na kuinywa damu yangu hana uzima ndani yake. (Yohana 6:53)

Vivyo hivyo na kutawadhana miguu watakatifu. Unapomwosha mwenzako miguu, maana yake ni kuwa unajishusha na kujinyenyekeza kwake, hivyo unapokea neema ya Upendano wa ndugu ndani yako.

Hivyo kwa ufupi ili utake kupokea tabia zote za Ki-Mungu ndani yako,  kama Upendo, utu wema, furaha, amani, Uvumilivu, huna budi kuwa katika ushirika wake. Nje ya hapo, huwezi.

Matendo 2:41  “Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu. 42  Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali”

Usiukwepe ushirika wa Bwana.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo:

HUNA SHIRIKA NAMI.

MEZA YA BWANA, NA KUTAWADHANA MIGUU.

KANUNI RAHISI YA KUPOKEA BARAKA MARA DUFU.

HISTORIA YA BIBLIA YA KING JAMES, INA FUNZO GANI KWETU?

WANNE WALIO WAONGO.

Ni lini na wapi Ibrahimu aliioona siku ya Bwana akashangilia?

Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima; (Mithali 11:16)

ZIFAHAMU KAZI TATU ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA ULIMWENGU.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments