Birika walilooga Makahaba lilikuwaje?

Birika walilooga Makahaba lilikuwaje?

Swali: Katika kifo cha Ahabu, biblia inasema alikufa na gari lake likaenda kuoshwa katika birika ambalo wanaoga Makahaba, (1Wafalme 22:38)..hili birika walilokuwa wanaoga makahaba lilikuwaje?

Jibu: Turejee.

1Wafalme 22:37 “Hivyo akafa mfalme, akachukuliwa Samaria, wakamzika mfalme huko Samaria. 

38 Wakaliosha gari penye birika la Samaria, na mbwa wakaramba damu yake; (basi ndipo walipooga makahaba); sawasawa na neno la Bwana alilolinena. 

39 Na mambo yote ya Ahabu yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, na nyumba ya pembe aliyoijenga, na miji yote aliyoijenga, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli?”

Ikumbukwe Ahabu alimwua Nabothi Myezreeli na kumdhulumu kiwanja chake, (1Wafalme 21:1-16), na baada ya kumwua ndipo unabii ukaja kupitia Eliya, kumwambia kuwa atakufa na damu yake italambwa na mbwa kama alivyomwua Nabothi (soma 1Wafalme 21:17-27).

Baada ya miaka mitatu, ndipo unabii huo unakuja kutimia, Mfalme Ahabu alikufa alipokuwa vitani na damu yake ikalambwa na mbwa mahali pale pale mbwa walipolamba damu ya Nabothi.

Lakini tunasoma tena jambo lingine lililoambatana na kifo cha Ahabu, kwamba mahali pale gari lake lilipooshwa ni mahali pia Makahaba wanapooga.

Sasa biblia haijaeleza kwa kina hili birika ambalo walikuwa wanaoga makahaba lilikuwaje. Lakini ni wazi kuwa hili halikuwa birika la kiyahudi, Kwani mabirika/ mabwawa ya kiyahudi yalikuwa yanatumika na makuhani na watu wa kawaida katika kuoga(kutawadhia) ili kujitoa unajisi.

Walawi 15: 16 “Na mtu ye yote akitokwa na shahawa yake, ndipo ataoga mwili wake wote majini, naye atakuwa najisi hata jioni”.

Soma pia Walawi 15:13, Kumbukumbu 23:10-11.

Lakini hili Birika/bwana hili ambalo makahaba walikuwa wanaoga, lilikuwa katika mji wa Samaria mtaa wa Yezreeli, ambao ndio ulikuwa kitovu cha ibada zote za mungu baali. Hivyo hili halikuwa bwawa la dini ya kiyahudi, bali lilikuwa ni bwawa la mungu baali. Huenda makahaba walikuwa wanaoga hapo kulingana na desturi zao za kibaali, kwani desturi nyingi za dini ya kibaali zilikuwa zinakaribia kufanana na za dini ya kiyahudi.. (mfano wa hizo utaona ni ile sadaka Ahabu aliyoitoa katika 1Wafalme 18:20-30).

Hivyo huenda nao pia walikuwa na desturi kama hiyo ya wayahudi ya kujiosha katika mabwawa/mabirikia.

Lakini lililo kubwa la kujifunza hapo ni kuwa Neno la Mungu kamwe halipiti.. Alisema Ahabu atakufa na damu yake italambwa na mbwa, na kweli alikufa sawasawa na neno hilo miaka mitatu baadaye, katika kifo cha aibu zaidi hata ya  kile alichomuua Nabothi.

Na vile vile alisema, kuwa atarudi tena pamoja na ujira wake kulimlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo, Neno hilo halitapita, ni lazima litimie na sasa tupo katika siku za kurudi kwake, muda wowote unyakuo unatokea!

Ufunuo 22:12  “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.

13  Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.

14  Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake”

Je umeokoka kikweli kweli au bado una uvuguvugu?…Ufunuo 3:16 “Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu”.

Mathayo 24:35 “Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe”.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo:

Je Mungu anaweza kumdanganya mtu?

BIRIKA LA SILOAMU.

USIMPE NGUVU SHETANI.

Baali alikuwa nani?

Birika ni nini?, na yale Matao matano katika birika la Bethzatha ni nini?.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

5 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Loanyuni Tarakwa
Loanyuni Tarakwa
1 year ago

Amen.

Kim
Kim
1 year ago

Mungu akubariki

Anonymous
Anonymous
1 year ago
Reply to  Kim

Amen atubariki sote..

Patrick
Patrick
1 year ago

Mungu awabariki,fikilia tena damu ya mfalme kulambwa na imbwa ni ayibu tena gari la mfalme kusukuliwa mahali kahaba wanaogea ni mchafu kama zaidi!

Loanyuni Tarakwa
Loanyuni Tarakwa
1 year ago
Reply to  Patrick

Ni aibu