Anaposema mwanamume mmoja katika elfu nimemwona anamaana gani?

Anaposema mwanamume mmoja katika elfu nimemwona anamaana gani?

SWALI: Mhubiri anaposema mwanamume mmoja katika elfu nimemwona bali mwanamke mmoja miongoni mwa wote mimi sikumwona, anamaana gani,?


JIBU: Tusome,

Mhubiri 7:27 Tazama, asema Mhubiri, mimi nimeyaona hayo kwa kulinganisha hili na hili, ili kuitafuta jumla;  28 ambayo bado nafsi yangu nikali nikiitafuta, nisiione; mwanamume mmoja katika elfu nimemwona; bali mwanamke mmoja miongoni mwa wote mimi sikumwona.

Ukichunguza hapo utaona Sulemani hajaenda moja kwa moja kutaja mtu aliyemwona Kwamba ni mtu ‘mkalimifu’ au ‘ mtu anayeelekea ukamilifu’.

Katika maisha yake ya kuchunguza na kulinganisha mambo kwa hekima ya ki-Mungu, aliona kuna vitu Fulani vipo katika jinsia fulani na kuna vitu Fulani havipo katika jinsia husika,. Kumbuka Sulemani alikuwa na uzoefu wa kuishi na wanawake wengi, alikuwa na wake mia saba na masuria mia tatu, bado na wakwe zake kama angependa kuwahesabu, jumla yao ingekuwa ni kubwa sana. Hivyo alipokuwa anayasema maneno hayo, hakuwa anabahatisha mawazo yake, au anaonyesha udhaifu kwa wanawake hapana..

Sulemani aliona katika jambo la juhudi ya kuulekea ukamilifu wote aliouhitaji Mungu, halikuwa kwa jinsia zote, bali kwa jinsia ya kiume tu, na tena kati ya hao ni wachache sana aliowaona, yaani mmoja kati ya elfu, lakini kwa wanawake hakuwahi kuona hata kwa mmoja,. Lakini hakumaanisha kwamba mtu huyo aliyemwona tayari alikuwa ni “Mkamilifu”..Kwasababu kipindi chote kile alichokuwepo, hakukuwahi kutokea mwanamume aliyempendeza Mungu kwa utimilifu wake wote, isipokuwa wapo waliojitahidi kusogelea hatua hizo lakini hawakufikia,  mfano wa hao ni kama Ayubu, na Henoko. N.k. Lakini hao wote bado hawakuwa wakamilifu kwa viwango Mungu alivyovitaka, japo kulikuwa na vimelea hivyo, tofauti na katika ile jinsia nyingine.

Lakini maono yake yalikuja kutimia kwa mwokozi wetu YESU KRISTO, yeye ndiye aliyeishi asilimia mia maisha ya ukamilifu ya kumpendeza Mungu bila kutenda dhambi yoyote,ambaye alijaribiwa kama sisi tulivyojaribiwa bila kumkosea Mungu. Na ndio maana kwanini Masihi hakuja katika jinsia ya kike, kuukomboa ulimwengu bali jinsia ya kiume.

Hivyo huyo mwanaume pekee aliyefikia ukamilifu ni Yesu tu, Sisi wengine wote tumepungukiwa na utukufu wa Mungu, iwe ni wa jinsia ya kike au ya kiume. Na wote tunaokolewa kwa neema yake tu pindi tunapomwamini yeye. Hiyo ikiwa wewe bado hujaupokea wokovu, na unatamani kufanya hivyo sasa, basi bofya hapa ili uweze kupata mwongozo huo wa kumruhusu Kristo aingie maishani mwako akuokoe.>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA

Biblia ilimaanisha nini iliposema “Mwanamke atamlinda mwanamume” Yeremia 31:22?

MWANAMKE ABIGAILI ANAFUNZO GANI KWA WANAWAKE?

KIKOMBE CHA GHADHABU YA MUNGU KINAJAA.

Je, kama hauna ubatizo sahihi hauwezi kuwa na Roho Mtakatifu?

Biblia inasemaje kuhusu Nywele?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments