Kufufuka kwa Bwana kulitabiriwa wapi katika agano la kale?

Kufufuka kwa Bwana kulitabiriwa wapi katika agano la kale?

Swali: Bwana Yesu alitabiriwa wapi katika agano la kale kwamba atafufuka?


Jibu: Kabla ya kuona ni wapi alitabiriwa kufufuka, tutazame kwanza ni wapi alipotabiriwa kuteswa, na kuzikwa, na kukaa kaburini siku tatu.

  1.KUTESWA

Unabii wa mateso ya Bwana Yesu kwaajili ya dhambi zetu upo wazi katika unabii wa Isaya.

Isaya 53:4 “Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.

5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.

   2. KUZIWA NA KUKAA KABURINI SIKU TATU (3)

Unabii wa Bwana Yesu kukaa kaburini siku tatu, umejificha nyuma ya maisha ya nabii YONA,..Bwana YESU mwenyewe alisema kama vile Yona alivyokaa tumboni mwa samaki siku tatu mchana na usiku ndivyo na yeye atakavyokaa katika moyo wa nchi siku tatu.

Mathayo 12:39 “Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona.

40  Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi”.

Kwahiyo maisha ya Yona yalibeba unabii wa Bwana YESU wa kukaa kaburini siku tatu. Na ndiyo ishara pekee iliyofanikiwa kuwafanya watu wa Ninawi waokoke na adhabu kutoka kwa Mungu. Vivyo hivyo kwa kuamini ishara ya Bwana Yesu ya kufa na kufufuka tunapata kuokoka na ziwa la moto, aliloandaliwa shetani na malaika zake.

     3. KUFUFUKA

Unabii wa kufufuka kwa Bwana Yesu kwa sehemu tunaupata katika habari hiyo hiyo ya Yona, kwani Yona baada ya kukaa katika tumbo la samaki mwishowe alitapikwa na yule samaki, vile vile kwa KRISTO, baada ya siku tatu alifufuka kutoka kaburini.

Lakini Zaidi sana pia Daudi, kwa kuwa ni nabii aliona ufufuo wa YESU (Masihi)..na kutabiri kuwa “hataona uharibifu wala roho yake haitasalia kuzimu” (Soma Zaburi 16:10). Lakini Mtume Petro anakuja kuuweka vizuri unabii huo wa Daudi katika kitabu cha Matendo ya Mitume mlango wa pili.

Matendo 2:29 “Waume, ndugu zangu, mniwie radhi, niseme kwa ujasiri mbele yenu habari za baba yetu mkuu, Daudi, ya kuwa alifariki akazikwa, na kaburi lake liko kwetu hata leo.

30  BASI KWA KUWA NI NABII, akijua ya kuwa Mungu amemwapia kwa kiapo, ya kwamba katika uzao wa viuno vyake atamketisha mmoja katika kiti chake cha enzi;

31  yeye mwenyewe akitangulia kuyaona haya, ALITAJA HABARI ZA KUFUFUKA KWAKE KRISTO, YA KWAMBA ROHO YAKE HAIKUACHWA KUZIMU, WALA MWILI WAKE HAUKUONA UHARIBIFU.

32  Yesu huyo Mungu alimfufua, na sisi sote tu mashahidi wake”.

Na ndivyo ilivyotokea kama Daudi alivyotabiri “mwili wa Bwana haukuona uharibifu (yaani haukuoza)” na vile vile “roho yake haikubaki kuzimu” ndio maana alifufuka baada ya siku tatu.

Kwahiyo biblia ilishatabiri yote kuhusiana na maisha ya Bwana Yesu kuanzia kuzaliwa kwake mpaka kufa kwake na mpaka kupaa na kurudi kwake mara ya pili, na utawala wake wa miaka elfu hapa duniani, na nafasi yake katika umilele ujao.

Unabii wa Bwana Yesu kuzaliwa Bethlehemu kasome Mika 5:2, unabii wa Bwana Yesu kuingia Yerusalemu kwa shangwe akiwa juu ya mwana-punda huku akiimbiwa Hosana Hosana kasome Zekaria 9:9, unabii wa Bwana Yesu kusalitiwa na Yuda kasome Zaburi 41:9, unabii wa mavazi ya Bwana Yesu kugawanywa kwa kura kasome Zaburi 22:18.

Unabii wa Bwana Yesu kupewa kuzungumza maneno yale “Mungu wangu mbona umeniacha” kasome Zaburi 22:1,  Unabii wa Bwana Yesu kupewa Siki badala ya maji kasome Zaburi 69:21, unabii wa Bwana Yesu kusulibiwa pamoja na wahalifu upo katika Isaya 53:12 n.k N.K

Je umempokea huyu YESU?..kama bado basi fahamu kuwa nafasi yako ni leo na si kesho. Kwasababu upo unabii wa kurudi kwake ambao tupo mbioni kuushuhudia, saa yoyote KRISTO anatokea mawinguni na kuwanyakua walio wake, je wewe ambaye hujaokoka utakuwa wapi?

Mpokee Bwana Yesu leo na kubatizwa na kujazwa Roho Mtakatifu.

Ikiwa utahitaji msaada leo katika kuokoka basi wasaliana nasi kwa namba zetu zilizoanishwa mwisho wa somo hili au fungua hapa >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

TUNAMHITAJI SANA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUYAELEWA MAANDIKO.

MADHARA YA KUTAFUTA ISHARA.

Katika (Mathayo 25:8 na Marko 16:8) Wale wanawake walitangaza kufufuka kwa Bwana au walikaa kimya?

YONA: Mlango 1

YONA: Mlango wa 2

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments