MAOMBI YA KUOMBEA WATOTO.

MAOMBI YA KUOMBEA WATOTO.

(Masomo maalumu kwa wazazi na walezi)

Marko 9:21 “Akamwuliza babaye, Amepatwa na haya tangu lini? Akasema, TANGU UTOTO

Na mara nyingi amemtupa katika moto, na katika maji, amwangamize; lakini ukiweza neno lo lote, utuhurumie, na kutusaidia

23  Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye”.

Kuna umuhimu Mkubwa sana wa kuwaombea watoto, KILA SIKU (ZINGATIA HILI: KILA SIKU!!!!). Kwanini kila siku?..kwasababu adui naye anawatafuta kila siku, kwamaana anajua imeandikwa (Uzao wako utamponda kichwa (Mwanzo 3:15))

Vifuatavyo ni vipengele vya Maombi kwaajili ya mtoto/watoto.

        1.WOKOVU/NEEMA.

Mwombee mtoto wako Neema ya kumjua Mungu, na kuzungumza naye tangu akiwa tumboni, na ikiwa ulichelewa kuanza kufanya hivyo, basi bado unayo nafasi ya kumwombea hata sasa.

Andiko la kusimamia: 1 Timotheo 3:15  “na ya kuwa TANGU UTOTO umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu”

     2. UTII NA HESHIMA

Mwombee mtoto wako/watoto wako roho ya Utii..Ili wapate miaka mingi ya kuishi na ya kheri.

Andiko la kusimamia: Waefeso 6:1 “Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki.

2  Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, 6.3  Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia”.

       3. ULINZI

Waombee watoto wako ulinzi wa kiroho na kimwili,  Wakiroho- wasivamiwe wala kutumiwa na nguvu za giza angali wakiwa wadogo na hivyo kuaathirika tabia zao, vile vile wasiharibiwe na dunia wala wasijengeke katika misingi isiyofaa.

Andiko la kusimamia: 1Yohana 5:21  “Watoto wadogo, jilindeni nafsi zenu na sanamu”

      4. UKUAJI (KIROHO NA KIMWILI)

Waombee watoto wako wakue katika kumjua Mungu, vile vile wasipate shida yoyote ya kiafya itakayowaletea ulemavu au udumavu. Akili zao zikue vizuri na wawe na afya bora, vile vile magonjwa yasiwapate iwe ya kuambukiza au kurithi.

Andiko la kusimamia: Luka 2:39 “Basi, walipokwisha kuyatimiza yote kama yalivyoagizwa katika sheria ya Bwana, walirejea Galilaya mpaka mjini kwao, Nazareti.

40  Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake”.

       5. ELIMU

Waombee watoto wako wawe watu wa kupenda kusoma, na pia kufanya vizuri katika Elimu ya dunia.

Andiko la kusimamia: Mithali  4:13 “Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako”

      6. ROHO MTAKATIFU.

Waombee watoto wako wajazwe na Nguvu za Roho Mtakatifu katika nyakati zote, wakiwa tumboni kama Yohana Mbatizaji (Luka 1:15) na hata baada ya kuzaliwa na katika vipindi vyote vya ukuaji wao.

Andiko la kusimamia: Matendo 2:38 “ Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

39  Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie”.

Kama ukiweza kutumia muda wa kutosha kumwombea Mtoto wako/watoto wako katika vipengele hivyo (KILA SIKU, Asubuhi na jioni)  basi utamweka utawaweka katika nafasi nzuri sana kiroho na mafanikio katika wakati ujao.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

NINI MAANA YA SISI KUWA WATOTO WA MUNGU?

FAIDA ZA MAOMBI YA USIKU

Nini maana ya “Andiko huua, bali Roho huhuisha (2Wakorintho 3:6)

MWONGOZO WA MAOMBI YA WAHUDUMU/ WASIMAMAO MADHABAHUNI.

NI YESU YUPI UNATEMBEA NAYE?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments