Swali: Je wakristo tunaruhusiwa kukopa benki au kutoka kwa watu?..kama ni ndio, kwanini maandiko yaseme mtakopesha wala hamtakopa? (Kumbukumbu 15:6).
Jibu: Turejee..
Kumbukumbu 15:6 “Kwani Bwana, Mungu wako, atakubarikia, kama alivyokuahidi; nawe utakopesha mataifa mengi, lakini hutakopa; tena utayatawala mataifa mengi, usitawaliwe na wao”
Kuna kukupa kwa aina mbili; 1) KWA AJILI YA KUTATUA TATIZO/JANGA…. 2) KWAAJILI YA KUJITANUA.
1. KUKOPA KWAJILI YA KUTATUA MATATIZO.
Kukopa kwa namna hii ni ile hali ambayo, mtu anapatwa na baa Fulani au janga, hivyo ili kujikimu au kujikidhi anakwenda kutafuta msaada kwa njia ya kukopa!.. Sasa kukopa kwa namna hii ndiko kunakozungumziwa hapo katika Kumbukumbu 15:6 (kwamba tutakopesha wala hatutakopa).
Na kwanini tutakuwa watu wa namna hiyo (ya kutokukopa)?.. ni kwasababu Mungu ni msaada wetu ambaye hataruhusu tupate matatizo hayo pasipo kuwa na sababu yoyote. Hivyo tutabaki katika usalama wake ambao utatuhifadhi dhidi ya madhara yote ya yule adui.
Hivyo kama mkristo ukiona unapitia vipindi vya mfululizo vya kukopa ili kukidhi mahitaji yako ikiwemo chakula, basi jaribu kulitazama jambo hilo kiroho Zaidi, na Bwana atakusaidia kukutoa hapo!.
2. KUKOPA KWAAJILI YA KUJITANUA.
Hii ni aina ya pili ya UKOPAJI, ambayo biblia haijaikataza!.. Inapotokea huna janga lolote, huna baa lolote, na unaishi vizuri kwa katika neema ya Mungu, kiasi kwamba ukipatacho kinakidhi hali ya kutokuwa na haja ya kukopa!.. Lakini ukapenda kujitanua Zaidi ya hapo kifedha au kibiashara au kimiradi kama mtu wa Mungu, na ukaamua kwenda kukopa ili kuongeza labda ule mtaji ulio nao ili kutanua kazi au biashara..
Kukopa kwa namna hii “hakujakatazwa kwa mkristo” na wala hakumaanishi kuwa wewe ni maskini, kwasababu hata watu wengi walio matajiri sana pia wanakopa!!.. lengo lao la kukopa si kukidhi mahitaji (kwamba wana janga fulani au baa fulani, hivyo wasipopata huo mkopo wanaweza kudhurika) bali mara nyingi ni kwa lengo la kutanua biashara zao wazifanyazo au miradi yao.
Na Mkristo anapofikia mahali anahitaji kutanuka Zaidi anaweza kuchukua mkopo, na isiwe na tafsiri yoyote kwamba ni maskini au muhitaji, na kwamba pasipo huo hawezi kuishi.
Kanuni ya KUKOPA ni sawa na ile ya KUUZA tu!… Mtu anayeuza shamba kwaajili ya matatizo, ni tofauti na yule anayeuza shamba kama biashara!..kadhalika mtu anayekopa kwaajili ya kutatua matatizo/au janga Fulani ni tofauti na yule anayekopa kwaajili ya kujitanua.
Bwana atusaidie katika yote.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
WENGINE WANAKESHA KWAAJILI YAKO.
SABATO ILIFANYIKA KWAAJILI YA MWANADAMU NA SI MWANADAMU KWAAJILI YA SABATO!
Kaniki ni nini katika biblia? (Yeremia 8:21).
About the author