Kaniki ni nini katika biblia? (Yeremia 8:21).

Kaniki ni nini katika biblia? (Yeremia 8:21).

Jibu: Neno “kaniki” limeonekana mara mbili tu katika biblia..(Yeremia 8:21 na Yeremia 14:2).

Na sehemu zote mbili linamaanisha “vazi jeusi lililovaliwa na watu wanaoomboleza” aidha kutokana na janga fulani au msiba.

Tamaduni za kuvaa kaniki katika misiba, zipo mpaka leo katika baadhi ya jamii za watu, ndio maana katika baadhi ya misiba utaona watu wanavaa mavazi meusi.

Desturi hiyo ilikuwepo tangu enzi na enzi…

Na katika biblia tunaona Yeremia aluvaa vazi hili wakati anaomboleza kutokana na msiba mkubwa uliowapata watu wake  (yaani wana wa Israeli) baada ya kuuawa na Nebukadreza na baadhi yao kuchukuliwa mateka mpaka Babeli.

Yeremia  8:21 “Kwa sababu ya maumivu ya binti ya watu wangu nimeumia mimi; nimevaa kaniki; ushangao umenishika”.

Na wana wa Yuda wote waliomboleza kutokana na msiba huo.

Yeremia 14:2 “Yuda huomboleza, Na malango yake yamelegea Wameketi chini wamevaa kaniki; Na kilio cha Yerusalemu kimepaa juu”.

Je na sisi leo tunapoomboleza ni sharti kuvaa “Kaniki” (vazi jeusi)? Jibu ni La! Sio Sharti wala Amri..

Zaidi sana maombolezo ya misiba ya kidunia hayatufaidii chochote katika maisha yetu ya kiroho…lakini maombolezo ya dhambi zetu yanafaa sana..

Tunapoomboleza kwaajili ya dhambi zetu na za wengine, kwaajili ya makosa yetu na ya wengine, maaombolezo hayo yanafaa zaidi na yana matunda makubwa.

Yakobo 4:8 “Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.

9 HUZUNIKENI NA KUOMBOLEZA NA KULIA. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa KUOMBOLEZA, na furaha yenu kuwa hamu.

10 Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza”.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Kwanini Raheli aliiba miungu ya Baba yake, (Labani) Mwanzo 31:19.

Wana wa Manabii walikuwa ni watu gani?

Sikukuu ya kutabaruku ni ipi?

USIYADHARAU MARUDIA YA BWANA.

Nuru yetu inapaswa iangaze au isiangaze kulingana na Mathayo 5:16 na Mathayo 6:1?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Alpha Mgaya
Alpha Mgaya
1 year ago

Bwana Yesu apewe sifa? Kwa kweli nimebarikiwa sana na mafundisho yaliyomo katika kundi Hili husasan sikukuu za kiyahudi na fundisho tunalolipata, meza ya Bwana na kaniki ni Nini katika Biblia. Mungu awabariki sana

Jean marie bita
Jean marie bita
1 year ago

Je mtu asipobatizwa katika jina la yesu kristo ahiwezipokea roho mtakatifu?