Je biblia inajichanganya kwa habari za Yohana kuwa Eliya?

Je biblia inajichanganya kwa habari za Yohana kuwa Eliya?

Swali: Tunaona sehemu moja Bwana YESU akimshuhudia Yohana Mbatizaji kuwa yeye ndiye Eliya ajaye (Mathayo 11:14), lakini sehemu nyingine Yohana Mbatizaji anakataa jambo hilo kuwa yeye si Eliya, (Yohana 1:19-21) je ni yupi yupo sahihi, Bwana Yesu au Yohana Mbatizaji?.. au je biblia inajichanganya?

Jibu: Turejee mistari hiyo..

Mathayo 11:13 “Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana.

14  Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya atakayekuja”.

Ni kweli hapa Bwana YESU anasema “Yohana Mbatizaji ndiye Eliya ajaye”. Lakini kumbuka kuwa Bwana YESU hakumlenga Eliya kama Eliya, kwamba atarudi tena na kutokea duniani kuhubiri!.. La! Bali alimaanisha “roho ya Eliya/ huduma ya Eliya” ipo ndani ya Yohana Mbatizaji.

Ni sawa na kwenye ule mfano wa Lazaro na Tajiri Bwana YESU aliowaambia watu, pale Ibrahimu aliposema “Wanaye Musa na Manabii (Luka 16:29)” hakumaanisha Musa yupo sasahivi, bali alimaanisha kuwa watumishi wa Mungu wanaohubiri leo ndio akina Musa..

Hivyo Bwana YESU aliposema Yohana Mbatizaji ndiye Eliya alimaanisha ile roho iliyokuwa inatenda kazi ndani ya Eliya sasa ipo juu ya Yohana Mbatizaji. Sawasawa na ujumbe wa Malaika, aliompa Zakaria baba yake Yohana, kuwa mtoto atakayezaliwa atatangulia mbele za Bwana katika roho ya Eliya, lakini hatakuwa Eliya.

Luka 1:13 “Lakini yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana.

14  Nawe utakuwa na furaha na shangwe, na watu wengi watakufurahia kuzaliwa kwake.

15  Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; hatakunywa divai wala kileo; naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye.

16  Na wengi katika Waisraeli atawarejeza kwa Bwana Mungu wao.

17  NAYE ATATANGULIA MBELE ZAKE KATIKA ROHO YA ELIYA, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, na kuwatilia waasi akili za wenye haki, na kumwekea Bwana tayari watu waliotengenezwa.”

Hapo mstari wa 17 unasema, “Atatangulia katika roho ya Eliya”…na si kwamba atakuwa Eliya mwenyewe yule aliyepaa.. (Yule alishaondoka na hawezi kurudi tena).. Hivyo Yohana Mbatizaji, alijijua kuwa roho ya Eliya inatenda kazi ndani yake, lakini yeye si Eliya, na ndio maana walipomwuliza kama yeye ni Eliya akajibu siye.

Kwanini alijibu vile?..kwasababu ni kweli hakuwa Eliya, isipokuwa Huduma ya Eliya/roho iliyokuwa juu ya Eliya inatenda kazi ndani yake.

Yohana 1:19 “Na huu ndio ushuhuda wake Yohana, Wayahudi walipotuma kwake makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu ili wamwulize, Wewe u nani?

20  Naye alikiri, wala hakukana; alikiri kwamba, Mimi siye Kristo.

21  Wakamwuliza, Ni nini basi? U Eliya wewe? Akasema, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La”.

Kwahiyo kwa hitimisho ni kuwa Yohana Mbatizaji hakuwa Eliya aliyerudi… bali ni mtu ambaye roho ya Eliya ilikuwa inatenda kazi ndani yake. Hivyo biblia haijichanganyi mahali popote.

Je umeokoka?.. Kama bado basi fahamu kuwa unyakuo wa kanisa upo karibu sana, na Kristo amekaribia kulichukua kanisa lake. Hivyo fanya uamuzi sahihi leo wa kumkabidhi Bwana YESU maisha yako kabla ya ule mwisho.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

YEYE AJAYE ATAKUJA WALA HATAKAWIA.

Je Eliya aliandika waraka baada ya kupaa mbinguni?

Je! ile habari ya Herode kutaka kumwua Yohana mbatizaji inajichanganya?(Mathayo 14:5 na Marko 6:20).

ROHO YA ELIYA KATIKA AGANO JIPYA INATENDAJE KAZI?.

YOHANA MBATIZAJI

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest


2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Loyce Mkare
Loyce Mkare
8 months ago

Mine is not a comment but a question,l will ask it in kiswahili and it says ni nani anayeletea mokovu majaribu?

David Ntrmo
David Ntrmo
8 months ago
Reply to  Loyce Mkare

Your question is not understood at ll, correct spelling error