Swali: Je mkristo anaruhusiwa kuchangia damu kwa mgonjwa aliye katika uhitaji huo, kwaajili ya kuokoa maisha yake?
Jibu: Biblia inasema maneno yafuatayo…
1Yohana 3:16 “Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; IMETUPASA NA SISI KUUTOA UHAI WETU KWA AJILI YA HAO NDUGU. 17 Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo”
1Yohana 3:16 “Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; IMETUPASA NA SISI KUUTOA UHAI WETU KWA AJILI YA HAO NDUGU.
17 Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo”
Maadamu mtu akiondolewa damu kiasi kidogo mwilini mwake, Hafi!!.. na vile vile mtu anayepokea damu mwilini mwake pia Hafi!, kinyume chake ndio anapata UZIMA! (wa mwilini).. basi ni wazi kuwa si dhambi kuchangia damu kwa mtu mwingine…..Zaidi sana ni jambo la upendo, ikiwa hakuna njia nyingine ya kumsaidia mhitaji huyo zaidi ya hiyo ya kumchangia damu.
Kwanini si dhambi!.. ni kwasababu hata sehemu ya damu tulizonazo tumepokea kutoka kwa wazazi wetu!…HAKUNA MTU ANAYEZALIWA DUNIANI NA DAMU YAKE MAALUM (Special), wote tunazipokea kutoka kwa wazazi wetu ndio maana zinamfanano na hao!, na zinamfanano na ndugu zetu tuliozaliwa nao familia moja.
Kwahiyo kumchangia damu mgonjwa si dhambi!… Maana utamchangia atapona!, na kwa njia hiyo yaweza kuwa sababu ya kumvuta kwa KRISTO, (akiona upendo wako namna hiyo).. lakini kama ukimnyima na akifa katika hali yake ya kutokuamini hakuna faida yoyote wewe unayoipata…
Kwahiyo ni afadhali utafute namna ya kuokoa roho kwa njia hiyo, kwasababu hakuna hasara yoyote unayopata katika mwili wako utoapo kiasi kidogo hiko cha damu na kumpatia mwingine!.. ni lita ngapi za damu umepoteza wakati wa mzunguko wako (wewe mwanamke) na bado unaendelea kuishi.
Ni lita ngapi za damu umepoteza wewe mwanaume ulipopata majeraha au ulipofyozwa na hao mbu kutandani mwako siku zote za maisha yako?.. Kwa kutafakari hayo yote hakuna sababu ya kumnyima damu ndugu yako, ikiwa kuna ulazima huo, na wala hakuna sehemu yoyote kwenye biblia iliyokataza kuchangia damu.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Je!Sisi kama wakristo Tunaruhusiwa kuchangia ujenzi wa Imani nyingine?
Je mama mjamzito anaruhusiwa kufunga?
Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?
Nini maana ya Mithali 27:21 inaposema “mtu hujaribiwa kwa sifa zake?”
JE UMEUFIKIA ULE UTUKUFU HALISI WA MANA?
Rudi Nyumbani
Print this post