FUNDISHO LA BWANA JUU YA KUZALIWA MARA YA PILI.

FUNDISHO LA BWANA JUU YA KUZALIWA MARA YA PILI.

Jina la BWANA wetu YESU KRISTO libarikiwe, karibu tujifunze biblia neno la Mungu wetu ambalo ni Taa na Mwanga wa njia yetu (Zab.119:105).

Hebu tuangalie uzito wa kuzaliwa mara ya pili kupitia maneno ya BWANA WETU YESU KRISTO.

Yohana 3:1 “Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi.

2  Huyo alimjia usiku, akamwambia, RABI, TWAJUA YA KUWA U MWALIMU, UMETOKA KWA MUNGU; KWA MAANA HAKUNA MTU AWEZAYE KUZIFANYA ISHARA HIZI UZIFANYAZO WEWE, ISIPOKUWA MUNGU YU PAMOJA NAYE.

3  Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.

4  Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?

5  Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, MTU ASIPOZALIWA KWA MAJI NA KWA ROHO, HAWEZI KUUINGIA UFALME WA MUNGU”.

Hapa Nekodemo anataja vigezo vya Mtu kuwa na MUNGU kuwa ni “Ishara azifanyazo”…na anamthibitisha Bwana kwa ishara hizo, lakini Bwana anamrekebisha, kuwa “MTU asipozaliwa mara ya pili hawezi kuurithi ufalme wa Mungu (maana yake hawezi kuwa na MUNGU)”… Je! na sisi leo tunalijua hilo??????….Je unalijua hilo??? .

Nikodemo anaona ISHARA ni tiketi ya kuwa na MUNGU,… Bwana YESU anataja KUZALIWA MARA YA PILI ndio TIKETI.. Sasa tuchukue ya nani tuache ya nani?.. Bila Shaka maneno ya BWANA YESU ni hakika, na tena ndio uzima.

Ndugu haijalishi tutakuwa na uwezo wa kufanya miujiza mingi na mikubwa kiasi gani, kama HATUJAZALIWA MARA YA PILI (Maana yake kwa maji na kwa Roho) hatuwezi kuwa na Mungu, kutembea naye wala hatutamwona siku ile.

Mtu anapozaliwa mara ya pili anakuwa kiumbe kipya, maana yake yale maisha ya kwanza ya dhambi yanakuwa hayapo tena maishani mwake.

Kuzaliwa kwa maji ni Ubatizo wa Maji mengi na kwa jina la Bwana YESU na kuzaliwa kwa Roho ni ubatizo wa Roho Mtakatifu (Matendo 2:37-38), mambo haya ndiyo yanamkamilisha mtu baada ya kutubu.

Na anayetuzaa mara ya si mtu bali ni Mungu mwenyewe, na Mungu ni Roho (sawasawa na Yohana 4:24), na tunapozaliwa na Roho, basi tunakuwa watu wa rohoni.

Yohana 3:6 “Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho”

Na kuwa mtu wa rohoni, si kuona maono, au mapepo, bali ni kuzaliwa katika Roho, na Maji. Na sifa kuu ya mtu wa rohoni ni kuushinda ulimwengu (dhambi na mambo mengine ya kidunia).

1Yohana 5:4  “Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu”.

Soma pia 1Yohana 3:9 na 1Yohana 5:18.

Hivyo ukiona tamaa za kidunia bado zinakusumbua kuna uwezekano kuwa bado hujazaliwa mara ya pili, kwasababu wote waliozaliwa mara ya pili wanayo nguvu ndani yao ya kuushinda ulimwengu na ndio watu wa rohoni.

Je ishara ni uthibitisho wa mtu kuwa na Mungu??..jibu ni ndio!, lakini si uthibitisho wa kwanza… bali uthibithsho wa kwanza wa mtu kuwa na Mungu ni KUZALIWA MARA YA PILI. Kwasababu wapo watakaotenda miujiza na kufanya ishara nyingi lakini wasimwone Bwana siku ile sawasawa na Mathayo 7:22.

Kwahiyo kilicho cha msingi kuliko vyote ni “KUZALIWA MARA YA PILI (kuwa kiumbe kipya)”  na mengine ndio yafuate.

Wagalatia 6:15 “Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya“.

1Petro 1:23 “Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele”.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

FUNDISHO KUU LA NEEMA YA MUNGU KWETU.

JE! SISI KAMA WAKRISTO NI DHAMBI KUSHEHEREKEA KRISMASI?.

UMUHIMU WA KUZALIWA MARA YA PILI.

VITA VYA KIFIKRA BAADA YA KUZALIWA MARA YA PILI

KWANINI YESU NI ADAMU WA PILI?

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments