Yakobo alimaanisha nini kusema ‘ndipo BWANA atakuwa Mungu wangu’ Mwanzo 28:21

Yakobo alimaanisha nini kusema ‘ndipo BWANA atakuwa Mungu wangu’ Mwanzo 28:21

Mwanzo 28:21

[21]nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo BWANA atakuwa Mungu wangu.


JIBU:

Sura hiyo inaeleza ugumu wa safari ya Yakobo alipokuwa anamkimbia ndugu Yake Esau kuelekea nchi ya ugenini ya baba zake. 

Hivyo akiwa huko jangwani peke yake, haoni mbele wala nyuma, haoni msaada kwa mtu wala kitu, ndipo akamwekea Mungu nadhiri, na kumwambia maneno hayo. 

‘nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo BWANA atakuwa Mungu wangu’. 

Lakini swali linakuja je hakumwamini Mungu, au kumfanya Mungu wake mpaka hapo ambapo angetimiziwa nadhiri zake? Kwamaana baada ya miaka 20, ndio tunaona yakitimia hayo yote? je hiyo miaka yote ya hapo katikati YEHOVA hakuwa Mungu wake, mpaka wakati ambapo angetimiziwa nadhiri yake?

Jibu: mstari huo haumaanishi kwamba Yakobo alikuwa anamweka kwanza Mungu kwenye majaribio halafu akishamfanikisha ndipo amfanye rasmi kuwa Mungu wake.

Hapana, ingekuwa hivyo tusingeona  katika kipindi hicho chote Yakobo akimtumainia Mungu wa baba zake, angeendelea tu na mambo yake mpaka huo wakati ufike.Lakini tunaona Yakobo hakucha kumwamini Mungu mahali popote.

Katika kauli hiyo hapo Yakobo alikuwa anaongezea tu, kujitoa kwakwe zaidi kwa Mungu, endapo  atarudishwa salama, na ndio maana maana ukiendelea vifungu vinavyofuata..

anasema atamtolea Mungu wake Fungu la kumi kwa kila atakachokipata..

jambo ambalo hapo mwanzo asingeweza kwasababu alikuwa hana chochote.

Mwanzo 28:21-22

[21]nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo BWANA atakuwa Mungu wangu.

[22]Na jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi. 

Kwa namna nyingine..anamwambia Mungu nitafanya vizuri zaidi kwako, endapo nitarudi salama, kutoka katika nchi ya ugenini.

Au ni sawa na leo mtu aseme Bwana nitakutumikia endapo utaniondolea huu ugonjwa wangu wa kupooza. 

Hiyo haimaanishi kuwa amemwekea Mungu masharti, kwamba sasahivi hataki mtumikia mpaka aponywe hapana, lakini anaeleza kikwazo chake. Na kwamba kikiondolewa ataweza timiza vizuri matakwa yake ya kiutumishi. Ndicho alichokimaanisha Yakobo.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

TABIA ZA NJIA YA MUNGU KWA MKRISTO

USIMPE NGUVU SHETANI.

Kutoka 21:10 ina maana gani?.

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments