UFUATILIAJI NI SEHEMU YA HUDUMA MUHIMU KWENYE UINJILISTI

UFUATILIAJI NI SEHEMU YA HUDUMA MUHIMU KWENYE UINJILISTI

Matendo  11:25

Kisha akatoka akaenda Tarso kumtafuta Sauli;

Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo, napenda leo tujifunza jambo moja ambalo huwenda linasahaulika miongoni mwetu kama watendakazi shambani mwa Bwana.

Hatuna budi kufahamu ,ufuatiliaji huenda sambamba na uinjilisti. Twaweza hubiria watu wakaokoka, wakamjua Kristo, wakati mwingine wakaweza hata kujisimamia wenyewe, lakini tusipojijengea tabia ya kuwafuatilia na kukaa nao, kuwaimarisha, basi kazi yetu yaweza kuwa bure, au isiwe na matunda mazuri kama ipasavyo.

tunajifunza kwa mtu mmoja aliyeitwa Barnaba, aliyejulikana pia kama mwana wa faraja. Huyu aliithamini huduma hii. Baada ya kusikia kuwa Paulo, amegeuka na kuwa mkristo, lakini akaenda mahali panaitwa Tarso, mbali kidogo na kanisa, Barnaba aliona si vema amwache huko. Ikabidi afunge safari yeye mwenyewe kutoka Antiokia aende kumtafuta.

Hatujui safari yake ilichukua siku ngapi, wiki ngapi, miezi mingapi. Lakini hatimaye akampata ..Alipomwona huwenda hakuridhishwa na mazingira ya kihuduma aliyokuwa nayo, hakuridhishwa na hali ya kiroho aliyokuwa nayo. Kwasababu hata mtume Paulo kuondoka Yerusalemu ilikuwa si kupenda kwake ni kutokana pia na kukataliwa na kanisa, na hatari ya kuuliwa na wayahudi.

Lakini Barnaba alipomuona. Akamchukua amlete mahali bora zaidi, ambapo kanisa lipo hai. Akafika akaendelea na huduma, akaanza kuwa moto tena na kutokea hapo ndipo Mungu alipomfanya mhubiri wa kimataifa.

Leo hii tunasoma ushujaa wa Paulo, lakini kusimama kwake kulichangiwa na nguvu ya kufuatiliwa kwa waliomtangulia kiroho.

Je na sisi tumejiwekea desturi hii? kuwafuatilia mara kwa mara tunaowashuhudia injili?

Kamwe usimdharau mwongofu mpya, hata kama atakuwa anasua-sua, au mdhaifu sasa. Fahamu kuwa huyo ndio Paulo wa baadaye. Usihubiri tu ukaacha, ukadhani atajikuza mwenyewe.  Shughulika naye, omba naye, mfuate alipo, mfundishe, ikiwezekana mwamishe eneo alilopo ikiwa linamfanya asisimame kiroho. Na kazi yako itazaa matunda, usichoke.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

FAHAMU MAISHA YA YESU KABLA YA HUDUMA.

MAUMIVU  NYUMA-YA-HUDUMA.

MAMBO NANE (8), AMBAYO WEWE KAMA KIONGOZI UTAIGWA.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest


0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments