Swali: Haya malimbuko ya Akaya tunayoyasoma katika 1Wakorintho 16:15 yalikuwaje?
Jibu: Turejee..
1Wakorintho 16:15 “Tena ndugu, nawasihi; (mnawajua watu wa nyumbani mwa STEFANA kwamba ni MALIMBUKO YA AKAYA, nao wamejitia katika kazi ya kuwahudumu watakatifu)”.
“Akaya” inayotajwa hapo si mtu, bali ni eneo/mji uliopo maeneno ya Ugiriki kwa sasa. Mji huu umetajwa pia katika Matendo 18:12, Matendo 19:21, 2Wakorintho 1:1, 1Wathesalonike 1:7-8 na Yuda 1:6.
Mji huu wa Akaya, ulikuwa ni moja ya miji ambayo Mtume Paulo alipita kuhubiri injili ya BWANA YESU. Na mmoja wa watu wa kwanza kabisa kumpokea Bwana YESU na kuokoka katika Mji huo ni huyu mtu aliyeitwa STEFANA pamoja na nyumba yake yote.
Hawa ndio walikuwa watu wa kwanza kabisa kuipokea injili katika mji huo, na baadaye wakaongezeka wengine wengi. Hiyo ndio maana ya Malimbuko iliyotajwa hapo… Sio malimbuko ya mazao ile inayotajwa katika Kutoka 22:29, bali inayomaanisha “wa kwanza kupokea injili”.. kwamaana maana tu ya malimbuko ni “kuzaliwa kwa kwanza”, hivyo hawa watu walikuwa ni wa kwanza kuzaliwa katika injili katika mji huo wa Akaya.
Lakini sifa nyingine ya kipekee aliyokuwa nayo huyu Stefana pamoja na nyumba yake yote ni roho ya UKARIMU, ambayo waliionyesha sana kwa Paulo na watumishi wengine waliokwenda kuhubiri injili katika miji hiyo, walikuwa tayari kutoa vya kwao ili kuwatunza watumishi wa Mungu.
Na kwa tabia hiyo, ndiyo Mtume Paulo kwa kuongozwa na roho anawaagiza watu wa Korintho pamoja na sisi kwa ujumla tuige tabia kama hiyo na pia tuwatii sana watu wanaojitoa kwaajili ya kuishika mkono kazi ya Mungu, na pia tuwe tayari kushirikiana nao..
1Wakorintho 16:14 “Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo.
15 Tena ndugu, nawasihi; (mnawajua watu wa nyumbani mwa Stefana kwamba ni MALIMBUKO YA AKAYA, nao wamejitia katika kazi ya kuwahudumu watakatifu);
16 WATIINI WATU KAMA HAWA, NA KILA MTU AFANYAYE KAZI PAMOJA NAO, NA KUJITAABISHA.
17 Nami nafurahi kwa sababu ya kuja kwao Stefana na Fortunato na Akaiko; maana hawa wamenikirimia kwa wingi yale niliyopungukiwa kwenu”
Bwana atubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
INJILI YA MILELE NI IPI KATIKA BIBLIA?
About the author