Mistari ya kujihamasisha kuzidi kuomba na kumsihi Bwana!
Zaburi 88:1 “Ee Bwana, Mungu wa wokovu wangu Mchana na usiku nimelia mbele zako.
2 MAOMBI YANGU YAFIKE MBELE ZAKO, Uutegee ukelele wangu sikio lako.
Zaburi 39:12 “Ee Bwana, usikie maombi yangu, Utege sikio lako niliapo, Usiyanyamalie machozi yangu. Kwa maana mimi ni mgeni wako, Msafiri kama baba zangu wote”.
Zaburi 54:2 “Ee Mungu, uyasikie maombi yangu, Uyasikilize maneno ya kinywa changu.
Zaburi 61:1 “Ee Mungu, ukisikie kilio changu, Uyasikilize maombi yangu”.
Zaburi 66:19 “Hakika Mungu amesikia; Ameisikiliza sauti ya maombi yangu
20 Na ahimidiwe Mungu asiyeyakataa maombi yangu, Wala kuniondolea fadhili zake.”
Zaburi 84: 8 “Bwana, Mungu wa majeshi, uyasikie maombi yangu, Ee Mungu wa Yakobo, usikilize”
Zaburi 86:6 “Ee Bwana, uyasikie maombi yangu; Uisikilize sauti ya dua zangu”.
Zaburi 88:13 “Lakini mimi nimekulilia Wewe, Bwana, Na asubuhi maombi yangu yatakuwasilia”.
Yona 2:7 “Roho yangu ilipozimia ndani yangu, Nalimkumbuka Bwana; Maombi yangu yakakuwasilia, Katika hekalu lako takatifu”.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618.
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
UNAMCHUKULIA YESU KWAKO KAMA NANI?
Amka, Ee upanga, juu ya mchungaji wangu (Zekaria 13:7-9)
Je! Israeli wote wataokolewa siku ya mwisho kulingana na Warumi 11:26?
About the author