Wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli.

Wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli.

SWALI: 2Timotheo 3:7, ina maana gani inaposema;

wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli.


JIBU: Katika kitabu cha 2Timotheo sura ya tatu(3), kuanzia mstari 1-9. Kinaeleza sifa za watu watakaozuka katika siku za mwisho.  Tabia ambazo hapo mwanzo hazikuwepo. Sasa ukisoma pale utaona zimeorodheshwa baadhi ikiwemo kutokea watu wenye kupenda fedha, watu wakali, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu,..na nyinginezo

Lakini ipo sifa nyingine inatajwa pale, kuwa litazuka kundi la watu wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake..ndio hao ambao anaeleza sasa mbeleni, wanajifunza sikuzote ila wasiweze kuufikia ujuzi wa kweli.

Tusome;

2 Timotheo 3:5-9

[5]wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.

[6]Kwa maana katika hao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi;

[7]wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli.

[8]Na kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Musa, vivyo hivyo na hawa wanapingana na ile kweli; ni watu walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani.

[9]Lakini hawataendelea sana; maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama vile na upumbavu wa hao ulivyokuwa dhahiri.

Maana ya ujuzi;

Ujuzi maana yake ni ufanisi au kukifanya kitu kwa utashi wote. Mtu anaweza akafanya jambo lakini akiwa hana ujuzi nalo litakuwa ni kituko kama sio hasara kabisa. Kwamfano mtu atasema, mimi naweza kujenga (na hajasomea ujenzi). Hivyo akaenda kununua tofali na kuanza kupandisha, unajua ni nini kitamkuta? kwasababu hajui kanuni za ujenzi anaenda  kufanana na yule mtu aliyejenga nyumba yake juu ya machanga.

Ndivyo ilivyokuwa kwa hawa watu, hawakuufikia huo ujuzi wa kweli, kwasababu walikuwa na nia zao wenyewe za tofauti na sio ya Kristo, walilenga kuwakusanya wanawake waliokuwa na mizigo ya dhambi, kama daraja lao, na hifadhi yao ya kihuduma, ili watumize malengo yao. Sasa Kwa urefu wa tabia za wanawake hao bofya link hii  uwasome >>> Wanaowachukua wanawake wajinga mateka ni akina nani?

Lakini huo ujuzi wa kweli ni upi?

ujuzi wa kweli ni UTAUWA/ UTAKATIFU. Mtu anayefikia kilele cha kuifahamu kweli ya Kristo huishia katika utakatifu wa kweli. Tunalisoma hilo katika;

Tito 1:1

[1]Paulo, mtumwa wa Mungu, na mtume wa Yesu Kristo; kwa ajili ya imani ya wateule wa Mungu, na ‘ujuzi wa kweli’ ile iletayo utauwa;

Umeona ujuzi wa kweli, lazima ulete utauwa.

Lakini watu hawa walikuwa na mfano wa utauwa lakini walizikana nguvu zake kimatendo, ndio maana hawakufikia..waliitwa wakristo lakini wakristo jina, waliitwa mitume, wainjilisti, manabii, waalimu, watakatifu, lakini nia zao zipo penginepo. Walikuwa na elimu za vyuoni, wanajua kuyachambua maandiko, na vifungu vyote, lakini maisha ya utakatifu yapo mbali na wao.

Ndilo linalotendeka leo hii, maarifa tuliyonayo kuhusu Mungu ni mengi, zaidi hata watu wa kale, tuna wingi wa vyuo vya theolojia, na makanisa, na mafudisho mengi. Lakini maisha ya wengi hayamwakisi Kristo katika utakatifu wa kweli.

ndio hili neno linatimia,

wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli

Ni swali la kujiuliza na sisi, je! wokovu wetu umefikia ujuzi wa kweli? Kumbuka hizi ni siku za mwisho, mafundisho uliyonayo yanakusukuma kwenye nini? FUATA UTAKATIFU.

Bwana akubariki

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Nini maana ya mhubiri 9:11? si wenye mbio washindao katika michezo?

MWE NA HASIRA, ILA MSITENDE DHAMBI.

NJIA KUU YA KUINGIA KATIKA ULE MJI.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments