Huwezi kufanya kazi zote peke yako..
Aliyeunda injini ya gari, alihitaji mwingine mwenye ubobezi katika utengenezaji wa matairi, lakini pia alimhitaji mbobezi wa umeme wa magari, hivyo ili gari lisimame na kuanza kutembea limegharimu mikono na ujuzi wa wataalamu wengi.
Vile vile, mtumishi wa Mungu mmoja hawezi kufanya mambo yote peke yake, kuna wakati wengine watahusika tu.
Katika biblia kuna mahali Filipo alihubiri na kubatiza, lakini lakini Petro na Yohana waliwaombea hao waliobatizwa ili wajazwe Roho Mtakatifu.
Matendo 8:12 ”Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake.
13 Na yeye Simoni mwenyewe aliamini akabatizwa, akashikamana na Filipo; akashangaa alipoziona ishara na miujiza mikubwa inayotendeka.
14 Na mitume waliokuwako Yerusalemu, waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu, wakawapelekea Petro na Yohana;
15 ambao waliposhuka, wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu;
16 kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu.
17 Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu”
Umeona? mmoja Anabatiza wengine wanaombea ujazo wa Roho Mtakatifu..
Mambo yote yanakamilika namna hiyo katika ushirikiano na umoja wa Roho, na ndivyo kanisa la kwanza lilivyoenenda, hakukuwa na mashindano wala wivu katikati yao, tofauti na leo ambapo kila mtu anajiona bora kuliko mwingine.
Maandiko yanazidi kutuonyesha kuwa hata Paulo, hakupanda na kuwagia yeye, bali matunda yake yalipaliliwa na wengine.
1 Wakorintho 3:6-7 “Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu.
7 Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye”.
Kama mtumishi wa Mungu, Je unaweza kuruhusu watumishi wengine wawajenge wale uliowatafuta wewe?…
Kumbuka si kila mtumishi ni wa kweli!…wengi ni wa uongo, lakini je inapotokea umehakiki kuwa kweli yule ni mtumishi wa Mungu, je waweza kuruhusu yule uliyemvua wewe ajengwe na mtumishi mwingine kama wewe?.
Kama hilo jambo gumu basi msaada wa haraka kutoka kwa Bwana unahitajika kwasababu ndivyo Mitume walivyofanya na sisi tunapaswa tufuate hivyo vielelezo.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
NITAUVUTAJE UWEPO WA ROHO MTAKATIFU KARIBU NAMI?
KAMA MTUMISHI WA MUNGU, TAFUTA MAARIFA KWA BIDII.
JE! MTUMISHI KUTOKUWA NA FEDHA NI ISHARA KUWA KUNA TATIZO KATIKA IMANI YAKE?
About the author