Washami ni watu gani katika biblia?

Washami ni watu gani katika biblia?

Jibu: Washami wametajwa mara nyingi katika biblia, baadhi ya mistari iliyowataja na kama ifuatayo.. 2Samweli 8:6, 1Wafalme 20:21, 2Wafalme 5:2, Yeremia 35:11, Amosi 9:7 na sehemu nyingine nyingi utaona jamii hii ya watu ikitajwa.

Tukio mojawapo maarufu lililozungumziwa katika biblia liwahusulo Washami, ni lile la Nabii Elisha kulipiga upofu Jeshi lao na kuliongoza mpaka katikati ya Samaria. (soma 2Wafalme 6:10-20).

Sasa swali hawa Washami walikuwa ni watu gani?

Washami walikuwa ni watu walioishi katika Nchi ijulikanayo kama Siria/Syria kwasasa,

Kiswahili cha Siria ni  “Shamu” hivyo wenyeji wa nchi ya Shamu ndio walioitwa Washami.

Jamii ya watu hawa Washami, kwasasa haipo!, wala haijulikani, kutokana na Falme nyingi kupita zilizotawala dunia na hivyo kuchanganya jamii za watu katika maeneo husika, hivyo hakuna jamii ya washami ijulikanayo leo duniani, lakini nchi hiyo bado ipo, na sasa wanaishi waarabu (Uzao wa Ishmaeli), ndio inayoitwa Siria, na makao makuu yake ni Dameski. (Kumbuka hawa waarabu sio washami  waliozungumziwa katika biblia, bali wapo tu kama wahamiaji waliohamia katika hiyo nchi)

Kiroho Washami wanawakilisha jeshi la Adui, kwani ukisoma katika biblia  utaona ni karibia mara zote jeshi hili lilikinzana na Israeli. Na utaona wakati ule Elisha alipokuwa na mtumish wake, walipoona jeshi la Washami limewazunguka, Elisha alimwambia mtumishi wake asiogope kwani walio upande wao ni wengi kuliko jeshi wanaloliona mbele yao.

2Wafalme 6:15 “Hata asubuhi na mapema mtumishi wake yule mtu wa Mungu alipoondoka, na kwenda nje, kumbe! Pana jeshi la watu, na farasi na magari, wameuzingira mji ule. Mtumishi wake akamwambia, Ole wetu! Bwana wangu, tufanyeje?

16 Akamjibu, USIOGOPE; MAANA WALIO PAMOJA NASI NI WENGI KULIKO WALE WALIO PAMOJA NAO.

17 Elisha akaomba, akasema, Ee Bwana, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona. Bwana akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote.”

Hali kadhalika na sisi ni lazima siku zote tuone, na kufahamu kuwa jeshi la Mungu linalotuzunguka ni kubwa kuliko lile la Adui, ikiwa tupo ndani ya Neema ya damu yake!, lakini kama tupo nje ya Neema ya damu yake (yaani wokovu), basi tufahamu kuwa adui atakuwa na nguvu juu yetu, na wala hakuna tutakachoweza kumfanya, Nguvu yetu na ujasiri wetu upo katika Yesu tu?

Je umeokoka? Kama bado ni afadhali ukaokoka leo, maana hujui kesho itakuwaje, na kama unahitaji msaada huo basi wasiliana nasi kwa namba zetu tajwa hapa chini.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mada Nyinginezo:

Wasamaria walikuwa ni watu gani?

Kisiwa cha Patmo kipo nchi gani?.

KAMA MTUMISHI WA MUNGU, TAFUTA MAARIFA KWA BIDII.

BWANA AWEZA KUKUPA ZAIDI SANA KULIKO HIZO.

Je Yuda alienda wapi, ni mbinguni au jehanamu?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments