LAANA NI NINI KIBIBLIA?

LAANA NI NINI KIBIBLIA?

Kibiblia  Neno laana linatafsiri kwa namna mbili.

Namna ya kwanza, ni Kupoteza sifa ya kukubaliwa na Mungu kwa jambo lolote lile. Na hii chanzo chake ni lile anguko la mwanadamu tangu mwanzo.

Namna ya pili, ni apizo alitoalo mtu kwa mwenzake au alitoalo Mungu mwenyewe, kwa mwanadamu ili wafikiwe na ubaya fulani, au wakasifikiwe na Mema waliyokusudiwa.

 

LAANA YA KWANZA:

Sasa laana hii ya kwanza, inazalika kwasababu ya  asili yetu, ambayo ilionekana tangu Adamu, kuhasi maagizo ya Mungu, ambayo hata sisi sote tuliopo leo, asili hiyo ipo ndani yetu. Ni sawa na unavyomwona mdudu kama mende, ukimtazama tu tangu akiwa mtoto, utamchukia hata kabla hajaonyesha hali yake ya kupenda uchafu, kwasababu unajua asili hiyo ipo ndani yake. Atakuja kuwa mchafu tu.

 

Ndivyo ilivyo kwetu sisi, tayari Mungu alishaona tangu tunazaliwa tutamwasi tu yeye, mfano wa baba yetu Adamu.

Na ndio maana akaandaa mpango wa kuzaliwa upya mara ya pili, kupitia Yesu Kristo. Hivyo mtu yeyote anayezaliwa mara ya pili, anaondolewa katika laana hiyo ya kukataliwa na Mungu, na anakuwa mwana wa Baraka. Laana hii haiwezi kuondoka bila damu ya Yesu.

 

Hiyo ndio sababu kwanini maandiko yanasema Yesu alifanyika laana kwa ajili yetu. Maana yake, tunapokombolewa na yeye tunafanywa kuwa watu wengine kabisa wenye asili nyingine wasio na laana, wenye kukubaliwa na kupendwa na Mungu.

 

Wagalatia 3:13  Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;

14  ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani.

 

Hivyo wewe uliyeokoka, na kupokea Roho Mtakatifu unaitwa, mbarikiwa, unaitwa mungu duniani, mtoto wa Mungu kwelikweli.

LAANA YA PILI

Lakini laana ya pili, kama tulivyoona ipo katika maapizo ambayo huyatoa Mungu au mwanadamu mwenyewe.

a) Tukianzana na zile zinazonenwa na Mungu

Mungu anaweza kukutamkia laana, hata kama utakuwa umekombolewa na yeye. Unaweza kushiriki mabaya. Laana hizi zinaweza kukufanya usipoteze wokovu wako, lakini zikakukosesha mambo mengi sana duniani.

 

Mfano wa hizi ndio zile alizowaambia wana wa Israeli, kwamba watakapoacha sheria zake, basi watatawanywa katika mataifa yote, watakuwa mikia na sio vichwa, nchi itazuliwa Baraka zake, wataondokeshewa adui zao N.k. (Kumbukumbu 28)

 

Mfano pia wa hizi, ndio kama ile aliyoilaani nchi, na nyoka pale Edeni. Akasema itatoa miiba, na nyoka atakwenda kwa tumbo (Mwanzo 3:17). Vilevile ndio ile aliyomwambia Kaini kuwa atakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani (Mwanzo 4:12).

 

Hata sasa wapo wengi wanaokutana na maapizo hayo ya Mungu kwa kufanya dhambi au makosa ya makusudi. Namna ya kueupuka laana hizi ni kutii agizo la Mungu.

Kwasababu unapozizoelea zitakufanya uangukie kabisa kwenye kundi lile la kwanza la kukataliwa kabisa..la watu ambao hawajaokoka.

 

Waebrania 6:4  Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu,5  na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo,

6  wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.

7  Maana nchi inayoinywa mvua inayoinyeshea mara kwa mara, na kuzaa mboga zenye manufaa kwa hao ambao kwa ajili yao yalimwa, hushiriki baraka zitokazo kwa Mungu; 8  bali ikitoa miiba na magugu hukataliwa na kuwa karibu na laana; ambayo mwisho wake ni kuteketezwa.

 

Kinyume cha laana ni Baraka, unapotii amri za Mungu, umejiwekea mazingira mazuri ya kupokea Baraka.

 

b) Lakini pia zipo laana  zinazonenwa na  mwanadamu.

Hizi nazo zimegawanyika katika makundi mawili.

 

i) Kundi la kwanza ni la watu wa Mungu/wenye haki.

Kwamfano Utakumbuka Hamu alipoona uchi wa baba yake. Nuhu aliulaani uzao wake, Hivyo watu wa Mungu wamepewa mamlaka hiyo, hata sasa, ndio maana Bwana Yesu alisema mtakalolifunga duniani, limefungwa mbinguni, na akatusihi pia tuwe watu wa kubariki kuliko  kulaani. (1Petro 3:9)

Unapokosewa na mwenye dhambi epuka kutoa neno la madhara kwake, kwasababu hakika jambo hilo litampata na kumwangamiza kabisa. Ndicho alichokifanya Elisha kwa wale vijana arobaini na wawili waliomdhihaki.

 

ii) Kundi la pili ni laana zitokazo kwa watu waovu.

 

Husasani wachawi, nao pia huweza kusema jambo likatokea, Utakumbuka kisa cha Balaamu mchawi, alipoajiriwa na Balaki kwenda kuwalaani Israeli wa Mungu, lakini alishindwa akajikuta anawabariki badala ya kuwalaani.

Akasema hakuna uchawi (Hesabu 23:23).

Ikiwa wewe umeokoka, huna haja ya kuogopa laana za hawa, kwasababu haziwezi kukupata, kwasababu unalindwa na nguvu za Mungu, hizi huwa zinawapata watu ambao wapo nje ya Kristo YESU.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NUHU WA SASA.

MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI.

KUVUNJA MAAGANO YA UKOO.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments