Zaburi 78:18-19
[18]Wakamjaribu Mungu mioyoni mwao Kwa kutaka chakula kwa tamaa zao. [19]Naam, walimwamba Mungu, wakasema, Je! Mungu aweza kuandika meza jangwani?
Kumwamba kama ilivyotumika hapo ni “kuzungumza kinyume”
Hivyo hapo anaposema
“Naam, walimwamba Mungu, wakasema, Je! Mungu aweza kuandika meza jangwani?”
Ni sawa na kusema..
Naam, walizungumza kinyume na Mungu, wakisema Je! Mungu aweza kuandika meza jangwani?
Wana wa Israeli kule jangwani, vinywa vyao havikuwa vya shukrani au vya kuomba, bali vivywa vya kumjaribu Mungu na manung’uniko, ijapokuwa walijua uweza wake wote, lakini walijifanya kama Mungu wao hawezi kuwaokoa, wakawa wanauliza maswali yaliyoonekana magumu, kumbe nafsini mwao wanajua yote yanawezekana, wanafanya tu makusudi ili waone Yehova atafanya nini. Na ndio sababu iliyomfanya Mungu asipendezwe nao.
Na sisi pia tusiwe watu wa kumwamba Mungu, kwa kusema maneno ya kutoamini.
Shalom
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Kama Musa aliandika vitabu vya torati, Je! kifo chake alikiandikaje mule?
Rudi Nyumbani
About the author