Swali: Patasi ni nini kama tunavyosoma katika kitabu cha Kutoka 32:4?
Jibu: Turejee..
Kutoka 32:4 “Akaipokea mikononi mwao akaitengeneza kwa PATASI, akaifanya iwe sanamu ya ndama kwa kuiyeyusha; nao wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri.”
“Patasi” ni zana inayotumika kuchonga vitu vya jamii ya mbao au chuma. Kifaa hiki mara nyingi kinatumiwa na mafundi seremala, katika kuchonga mbao, na kuzitia urembo mbalimbali, au maandishi (Tazama picha chini).
Katika biblia neno hili limeonekana mara moja tu, pale ambapo wana wa Israeli walipojitengenezea sanamu ya ndama ili iwarudishe Misri walikotoka. Na waliifanya kwa kuyeyusha dhahabu zao na kisha kuzichonga kwa mfano wa ndama kupitia patasi.
Kutoka 32:1 “Hata watu walipoona ya kuwa Musa amekawia kushuka katika mlima, wakakusanyana wakamwendea Haruni, wakamwambia, Haya! Katufanyizie miungu itakayokwenda mbele yetu, kwa maana Musa huyo aliyetutoa katika nchi ya Misri hatujui yaliyompata. 2 Haruni akawaambia, Zivunjeni pete za dhahabu zilizo katika masikio ya wake zenu, na wana wenu, na binti zenu, mkaniletee. 3 Watu wote wakazivunja pete za dhahabu zilizo katika masikio yao, wakamletea Haruni. 4 Akaipokea mikononi mwao akaitengeneza kwa patasi, akaifanya iwe sanamu ya ndama kwa kuiyeyusha; nao wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri. 5 Naye Haruni alipoona jambo hili, akajenga madhabahu mbele yake; Haruni akatangaza akasema, Kesho itakuwa sikukuu kwa Bwana. 6 Wakaondoka asubuhi na mapema, wakatoa dhabihu, wakaleta sadaka za amani, watu wakaketi kula na kunywa, wakaondoka wacheze. 7 Bwana akamwambia Musa, Haya! Shuka; kwa maana watu wako uliowatoa katika nchi ya Misri wamejiharibu nafsi zao”.
Kutoka 32:1 “Hata watu walipoona ya kuwa Musa amekawia kushuka katika mlima, wakakusanyana wakamwendea Haruni, wakamwambia, Haya! Katufanyizie miungu itakayokwenda mbele yetu, kwa maana Musa huyo aliyetutoa katika nchi ya Misri hatujui yaliyompata.
2 Haruni akawaambia, Zivunjeni pete za dhahabu zilizo katika masikio ya wake zenu, na wana wenu, na binti zenu, mkaniletee.
3 Watu wote wakazivunja pete za dhahabu zilizo katika masikio yao, wakamletea Haruni.
4 Akaipokea mikononi mwao akaitengeneza kwa patasi, akaifanya iwe sanamu ya ndama kwa kuiyeyusha; nao wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri.
5 Naye Haruni alipoona jambo hili, akajenga madhabahu mbele yake; Haruni akatangaza akasema, Kesho itakuwa sikukuu kwa Bwana.
6 Wakaondoka asubuhi na mapema, wakatoa dhabihu, wakaleta sadaka za amani, watu wakaketi kula na kunywa, wakaondoka wacheze.
7 Bwana akamwambia Musa, Haya! Shuka; kwa maana watu wako uliowatoa katika nchi ya Misri wamejiharibu nafsi zao”.
Kiroho jambo hili linaendelea hata sasa, sanamu zinaendelea kuchongwa hata sasa,..matendo yasiyofaa tuyafanyayo ndio ibada ya sanamu (soma Wakolosai 3:5) na tamaa zetu ndio “Patasi”.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
JINSI WATU WANAVYOIUNDA SANAMU YA NDAMA MIOYONI MWAO.
HARUNI
FIMBO YA HARUNI!
USIABUDU SANAMU.
Kwanini ndugu wanaokaa pamoja wawe kama mafuta ya Haruni?
Rudi Nyumbani
Print this post