Je mtu anaweza kupoteza wokovu?

Je mtu anaweza kupoteza wokovu?

Jibu: Ipo elimu isemayo  kuwa “Mtu akiokolewa, ameokolewa na hivyo hawezi kupoteza wokovu”.. (Once saved, always saved).

Ni kweli msemo huo ni kama unataka kuleta maana kwamba mtu akiupokea wokovu hawezi tena kuupoteza…

Lakini maandiko yapo wazi yanayoonyesha kuwa mtu anaweza kuupoteza Wokovu.

Ufunuo 3:11 “Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, ASIJE MTU AKAITWAA TAJI YAKO

Sasa jiulize, kama mtu hawezi kupoteza wokovu alionao, kwanini Bwana YESU asisite kushika kile tulicho nacho.

Lakini pia, bado maandiko yanazidi kutufundisha kupitia safari ya wana wa Israeli, kwamba kweli walipata WOKOVU kutoka katika utumwa wa FARAO, lakini walipokuwa katika safari yao ya kuelekea KANAANI njiani waliupoteza ule wokovu, na Mtume Paulo kwa ufunuo wa Roho aliliona hilo pia na kulisema huku akulifananisha na Wokovu tuupatao, kwa njia ya kumwamini Bwana YESU na kuokoka kwamba tusipouthamini basi hatutapona kama wana wa Israeli walivyopotea.

Waebrania 2:1  “Kwa hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo yaliyosikiwa tusije tukayakosa.

2  Kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na kila kosa na uasi ulipata ujira wa haki,

SISI JE! TUTAPATAJE KUPONA, TUSIPOJALI WOKOVU MKUU NAMNA HII? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia”

Sasa kiswahili chepesi cha maandiko hayo ni hiki… “SISI JE TUTASALIMIKAJE TUSIPOUJALI NA KUUSHIKILIA ULE WOKOVU TULIOUPOKEA???” Na kumbuka hapo Mtume Paulo alikuwa haongei na watu ambao hawajaokoka, LA! Bali alikuwa anaongea na watu ambao tayari wanao wokovu, lakini huenda wanasuasua, hivyo anatoa hiyo tahadhari.

Wengi tusomapo mstari huo, tunawalenga wale wanaosikia injili lakini wanaifanya mioyo yao kuwa migumu kutii, lakini andiko hilo, halikuwa kwaajili ya watu walio nje ya Imani, bali kwa watu ambao tayari wanao WOKOVU.

Maana yake ni kwamba wokovu mtu anaweza kuupoteza kabisa kama hatakuwa makini, kama atakuwa sio mtu wa kujali.

Wanaoshikilia kuwa “Mtu akiokolewa ameokolewa hawezi kupoteza tena wokovu” wanasimamia mfano ule wa Baba na mtoto, kwamba mtoto akishazaliwa katika familia, hakuna kitakachoweza kumfanya asiwe mtoto wa baba yake.

Ni kweli kibinadamu hilo haliwezekani, aliyezaliwa katika familia ni lazima damu yake itabaki kuwa ya Baba yake hawezi kamwe kuupoteza ule wana (hiyo ni kweli kabisa)… Lakini kimaandiko sisi hatupokei uwezo wa kuwa wana kibinadamu, bali ni katika roho.. na kama uwezo huo unafanyika katika roho, basi pia katika roho unaweza kutanguka.

Ndicho kilichomtokea Esau, ni kweli alikuwa mwana wa kwanza wa Isaka, lakini alipoidharau nafasi yake ile ya uzaliwa wa kwanza ilihamia kwa ndugu yake Yakobo, yeye Esau aliendelea kuwa mzaliwa wa kwanza kwa tarehe za damu na nyama, lakini katika roho tayari ni mzaliwa wa pili, sasa kama mambo hayo yanaweza kubadilika hivyo, kwanini mtu asipoteze UWANA pale ambapo anaupuuzia wokovu wake? (Waebrani 12:16-17).

Ni wazi kuwa atapoteza ile hali ya kuwa Mwana wa Mungu, na atakuwa mwana wa Ibilisi katika roho, endapo asipouthamini wokovu wake.

2Petro 2:20  “Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza.

21  Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa.

22  Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni”

Hivyo kwa hitimisho ni kwamba Mtu anaweza kupoteza Wokovu endapo hataushikilia ipasavyo na hataujali, na kumbuka siku hizi za mwisho mafundisho haya yanamea kwa kasi sana, ambayo yanawafundisha watu kuwa ukishamwamini BWANA YESU inatosha, ishi uishivyo, fanya ufanyalo, wewe mbinguni utaenda.

Ndugu usidanganyike, maandiko yameweka wazi kabisa kuwa pasipo Utakatifu! Hakuna mtu atakayemwona MUNGU, iwe Mchungaji, iwe nabii, iwe Raisi wa nchi, iwe Mtume, iwe Papa, iwe mwanaume iwe mwanamke, iwe mtu yoyote ule. PASIPO UTAKATIFU, HAKUNA MBINGU!!!

Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, NA HUO UTAKATIFU, AMBAO HAPANA MTU ATAKAYEMWONA BWANA ASIPOKUWA NAO”

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

JE! SISI KAMA WAKRISTO NI DHAMBI KUSHEHEREKEA KRISMASI?.

Nini tofauti ya haya maneno. 1) KUOKOKA, 2) WOKOVU, 3) KUONGOKA.?

Kama tunaokolewa kwa neema kwanini wokovu tuupate kwa nguvu?

DHAMBI YA ULIMWENGU.

ESTA: Mlango wa 4

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments