Kitabu cha Wagalatia ni moja ya nyaraka ambazo mtume Paulo aliziandika kwa makanisa aliyoyapanda. Tunaona mwanzoni kabisa mwa waraka huu Paulo mwenyewe anajitambulisha akionyesha kuwa yeye ndiye mwandishi.
Waraka huu unamwonyesha Paulo akiwastaajabia watakatifu wa kanisa la Galatia kwa kuacha Imani ambayo aliwaachia hapo mwanzo, alipokuwa analisimamisha kanisa hilo, jambo ambalo lilimfanya mpaka imani yake impelekee kufikiri kuwa wamelogwa(Wagalatia 3:1), kwa jinsi tu walivyoiacha imani kwa haraka.
Kwa mujibu wa waraka huu, tunaona Paulo alilijenga kanisa hilo katika msingi wa imani katika neema ya Yesu Kristo.Na si katika msingi wa matendo ya sheria kama kigezo cha kukubaliwa na Mungu.
Kutokana na kuwa kanisa hili lilikuwa na mchanganyiko wa wayahudi pamoja na watu wa mataifa waliomwamini Kristo.Hapo ndipo tatizo lilipoanzia baada ya baadhi ya wakristo wa kiyahudi kuanza kuwashurutisha watu wa mataifa kwa kuwaambia kwamba hawawezi kuokolewa kama hawataishika torati ya Musa, kama hawatatimiza maagizo kama tohara, kushika siku, miezi, na miaka.(Wagalatia 4:8-10)
Hivyo hiyo ikawafanya watu kuacha kuishi tena kwa Imani iliyo katika neema ya Kristo Yesu, na kuangalia matendo ya sheria kama ndio kigezo cha kukubaliwa na Mungu?
Hivyo Paulo alipojua mageuzi hayo, ndio akawaandikia waraka huo kwa ukali, akiwaambia wokovu wetu huja kwa imani iliyo katika Yesu Kristo itendayo kazi katika upendo. Na si katika matendo ya sheria. Kwasababu kama ingekuwa hivyo Kristo alikufa bure. Torati ingeendelea tu kutawala.
Wagalatia 5:6
[6]Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.
Akasema torati, haikuwahi kumkamilisha mtu, na mtu anayeishi kwa hiyo ametengwa na Kristo, bado yupo chini ya laana.
kuishi kwa sheria ni kurudia mafundisho manyonge.
Lakini Swali ambalo alitarajia lingeulizwa na wagalatia, ni hili;
Je sasa hatuna haja ya kuyatazama matendo mema, tuishi tu, kama tunavyotaka kwasababu tunahesabiwa haki kwa neema ya Kristo tu?
Mbeleni kabisa katika sura ya tano, Mtume Paulo alitolea ufafanuzi, na kuwaambia tukishaokolewa, Maana yake ni kuwa tumeusulubisha mwili pamoja na tamaa zake mbaya..Hivyo hakuna nafasi ya dhambi kupata nguvu ndani yetu.
Wagalatia 5:24
[24]Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.
Je hilo inawezekanaje? kama hatuna sheria?
Linawezekana kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Ambaye tumepewa na Mungu.
Wagalatia 4:6
[6]Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba.
Hivyo Paulo anaendelea kueleza ni wajibu wa kila mwamini kutembea katika Roho. Ili awasaidie Roho kuzishinda tamaa zote za mwili, na mambo maovu.
Wagalatia 5:16-21
[16]Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.
[17]Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.
[18]Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.
[19]Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
[20]ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
,[21]husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
Je waraka huu ulilenga hasa nini?
Kwamba kwa nguvu zetu, au dini zetu au torati kamwe hatuwezi kumpendeza Mungu bali tuitegemee neema ya Kristo ambayo kwa hiyo tumepokea Roho awezaye kutufanya wakamilifu.
Hivyo ni wajibu wako kama mkristo. Kila wakati wote kujawa Roho (Waefeso 5:18). Ambayo hiyo huja kwa kuwa waombaji, wasomaji Neno, na kufanya ibada mioyoni mwetu wakati wote..
Tukiwa watu wa namna hiyo sheria wala dhambi inakuwa haina nguvu ndani yetu. Kwasababu tunakuwa chini ya neema ya Yesu Kristo.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Wapelelezi wa uhuru wa wakristo ni watu gani (Wagalatia 2:4)?
Rudi Nyumbani
About the author