Je ni Wokovu gani Simeoni aliouona? (Luka 2:30)

Je ni Wokovu gani Simeoni aliouona? (Luka 2:30)

Swali: Tunasoma Simeoni alipomwona mtoto YESU, Alikiri kuuona Wokovu wa MUNGU, sasa swali ni Wokovu gani huo alioupata?


Jibu: Tuanzie ule mstari wa 25 ili tuweze kuelewa vyema…

Luka 2:25 “Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, naye ni mtu mwenye haki, mcha Mungu, akiitarajia faraja ya Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.

26  Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana.

27  Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria,

28  yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake, akamshukuru Mungu, akisema,

29  Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema;

30  KWA KUWA MACHO YANGU YAMEUONA WOKOVU WAKO,

31  Uliouweka tayari machoni pa watu wote;

32  Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli”

Sasa hapo hajasema AMEUPATA WOKOVU..La! bali anasema “MACHO YANGU YAMEUONA WOKOVU”.. kuuona wokovu na kuupata wokovu ni vitu viwili tofauti…

Wokovu wa Mungu unapatikana kupitia mmoja tu, naye ni YESU KRISTO (Matendo 4:12),..Baada ya YESU kusulibiwa ndipo watu wakaanza kuupata wokovu, lakini kabla ya hapo waliusikia na kuuona tu,…waliousikia ni manabii wa kale na watu wote wa agano la kale, na waliouona ni watu waliokuwepo kipindi BWANA YESU anazaliwa, na walioupata ni wote waliomwamini baada ya kufufuka kwake.

Sasa utauliza vipi waliokufa katika haki wakati wa agano la kale, je hawakupata wokovu kabisa katika kipindi chao?… Jibu ni kwamba baada ya kufa kwao wokovu wao ulikuwa haujakamilika, lakini KRISTO aliposhuka kuzimu na kuchukua mamlaka yote ya walio hai na waliokufa, ndipo wokovu wao ukakamilika (maana yake wakaupata wokovu).

1Petro 1:10 “Katika habari ya wokovu huo manabii walitafuta-tafuta na kuchunguza-chunguza, ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi.

11 Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo.

12 Wakafunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu walihudumu katika mambo hayo, ambayo sasa yamehubiriwa kwenu na wale waliowahubiri ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Mambo hayo malaika wanatamani kuyachungulia”.

Kwahiyo Simoni aliuona Wokovu, kwakuwa anayebeba wokovu (YESU KRISTO) yupo pale.

Na wote tunaomwamini sasa, tunapokea wokovu wa roho zetu.

Je umempokea YESU?… Je umeoshwa dhambi zako kwa damu yake?

Matendo 4:12 “Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo”

Maran atha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

FAHAMU KANUNI ZA KUZISUBIRIA AHADI ZA MUNGU?

Nini tofauti ya haya maneno. 1) KUOKOKA, 2) WOKOVU, 3) KUONGOKA.?

Kama tunaokolewa kwa neema kwanini wokovu tuupate kwa nguvu?

UKIAMINI NA UKIMKIRI YESU KWA KINYWA CHAKO, UTAOKOKA.

Je mtu anaweza kupoteza wokovu?

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments