Ni mji gani mtakatifu shetani aliomchukua Bwana YESU? (Mathayo 4:5)

Ni mji gani mtakatifu shetani aliomchukua Bwana YESU? (Mathayo 4:5)

Je huu mji mtakatifu shetani aliomchukua Bwana katika Mathayo 4:5 ni mji gani?.. maana tunajua shetani hawezi kumiliki vitu vitakatifu?


Jibu: Turejee..

Mathayo 4:5 “Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu.
6 akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.

7 Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako”.

Mji Mtakatifu unaozungumziwa hapo ambao shetani alimpeleka Bwana YESU ni YERUSALEMU (Ya duniani) iliyopo pale Israeli..

Kumbuka ipo YERUSALEMU YA MBINGUNI, ambayo itakuja kushuka baada ya hukumu ya mwisho, na Yerusalemu hiyo Mpya shetani hawezi kufika wala watu ambao hawajamwamini Bwana hawataingia (kulingana na maandiko).

Ufunuo 21:1 “Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.

2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.

3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao”.

Ruka mpaka mstari wa 23-27..

“23 Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-Kondoo.

24 Na mataifa watatembea katika nuru yake. Na wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani yake.

25 Na milango yake haitafungwa kamwe mchana; kwa maana humo hamna usiku.

26 Nao wataleta utukufu na heshima ya mataifa ndani yake.

27 Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo”.

Lakini Mji shetani aliompeleka Bwana ulikuwa ni Yerusalemu ya duniani, (ule mji ule wa Daudi), mahali pale ambapo Hekalu la Sulemani lilijengwa..Yerusalemu hii ya duniani shetani anaweza kufika wakati wowote na mtu mwingine yoyote anaweza kufika, (awe mtakatifu au asiwe mtakatifu), anaweza kufika, na hata leo watu wanafika pale..

Na shetani alimpomfikisha Bwana YESU katika Hekalu, alimpandisha mpaka kwenye kinara chake, na kumwambia ajirushe chini, kwa maana imeandikwa atawaagiza malaika nao watamwokoa na ajali ile (sawasawa na Zaburi 91:11-12).

Lakini Kwakuwa Bwana YESU alikuwa amejaa Roho Mtakatifu, alizijuza hila na mbinu zote za ibilisi, na aliweza kumjibu kwa Neno, kuwa imeandikwa tusimjaribu Bwana MUNGU wetu.

Ni jambo gani tunaweza kujifunza hapo?

shetani anapotaka kumjaribu mtu anayemcha MUNGU hampeleki kwa waganga wa kienyeji, wala hampeleki kwenye mazingira ya dhambi ili atende dhambi, bali anampeleka sehemu takatifu, kama kanisani, au katikati ya watu wanaomtafuta MUNGU,
Ndio maana utaona leo mtu amesimama lakini anaanguka/anaangushwa katika dhambi na mtu/watu wa kanisani.

Utaona Askofu, au mchungaji, au mwinjilisti, au Nabii, au Mtume au mwimbaji wa kwaya anaanguka katika uzinzi na watu wa kanisani, ni mara chache sana na watu wa nje, kwanini?.
Kwasababu shetani anajua sehemu pekee ya kumjaribu mtu aliyeokoka na kusimama ni kanisani, akimletea wanaojiuza huko barabarani ni ngumu kuanguka..

Ndicho alichotaka kujaribu kufanya kwa Bwana YESU kumpeleka Hekaluni, kwanini asingempekeka kwenye vinara vingine vya mahali pengine, badala yake akachagua Hekalu?.. ni kwasababu alijua hapo ni rahisi kumwangusha Bwana.

Hivyo na sisi tuliookoka ni muhimu kuwa makini katika nyumba ya MUNGU kwani huko huko shetani anaweza kupata nafasi.

Bwana atusaidie.
Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 2)

MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 3)

MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 1)

Je! Yesu aliwezaje kuchukuliwa na shetani juu ya kinara cha hekalu kujaribiwa?

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments