Je mtu anaweza kubatizwa mara mbili?

Je mtu anaweza kubatizwa mara mbili?

Jibu:  Kulingana na biblia UBATIZO unapaswa ufanyike mara moja tu katika kipindi chote cha maisha ya mtu, ikiwa mtu huyo atakuwa ametimiza vigezo hivi viwili.

  1. KABLA YA KUBATIZWA AWE AMEELEWA MAANA YA UBATIZO NA KUTUBU:

Maana ya Ubatizo ni kuzika utu wa kale na kufufuka katika utu upya, hivyo ikiwa mtu ameelewa kuwa lengo la ubatizo ni kuacha maisha ya kale na kuanza maisha mapya katika KRISTO, basi hiko ni kigezo cha kwanza cha Uthabiti wa Ubatizo wake,

Warumi 6:3 “Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu TULIBATIZWA KATIKA MAUTI YAKE?

4 Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.

5 Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake;

6 MKIJUA NENO HILI, YA KUWA UTU WETU WA KALE ULISULIBISHWA PAMOJA NAYE, ILI MWILI WA DHAMBI UBATILIKE, TUSITUMIKIE DHAMBI TENA”.

Na kwa kigezo hiki, watoto hawabatizwi kwani wanakuwa bado hawajatambua maana ya maisha mapya katika KRISTO ni nini?, watoto wanawekewa mikono tu na sio kubatizwa….Kwahiyo kama mtu alibatizwa utotoni hana budi kubatizwa tena upya.

  2. NI AINA GANI YA UBATIZO ALIOBATIZWA.

Hiki ni kigezo cha Pili, kama mtu alibatizwa sawasawa na maandiko kwa maji mengi na kwa jina la Mwokozi YESU sawasawa na Mathayo 28:19 na Matendo 2:38 na si kwa maji machache na kwa majina ya watu wengine, basi huyo mtu hahitaji kubatizwa tena.

Lakini kama alibatizwa kwa ubatizo wa maji machache hata kama alishatubu dhambi zake, ni lazima abatizwe upya mara nyingine, kwasababu katika biblia hakuna mahali popote panaonyesha mtu yeyote amebatizwa kwa kunyunyiziwa, kwasababu maana tu yenyewe ya ubatizo ni kuzamisha/kuzika

Vile vile kama mtu alibatizwa kwa ubatizo wa Yohana, au wa mtu Fulani tofauti na  YESU hana budi kubatizwa upya.. Biblia inatuonyesha watu waliobatizwa kwa ubatizo wa Yohana kurudia ubatizo wao baada ya kukutana na injili ya ubatizo wa jina la YESU.

Matendo 19:3 “Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana.

4 Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu  

5 WALIPOSIKIA HAYA WAKABATIZWA KWA JINA LA BWANA YESU.

6 Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri.

7 Na jumla yao walipata wanaume kumi na wawili.”

Hapa tunaona hawa watu walibatizwa upya baada ya kusikia kuwa ubatizo sahihi ni wa Bwana YESU sio tena wa Yohana..

Kwahiyo na sisi hatuna budi kujihakika kama kweli tumebatizwa ubatizo sahihi, kama tumebatizwa ubatizo sahihi kulingana na vigezo hivyo hapo juu basi hatuna haja ya kubatizwa upya, Huo ubatizo unatosha, kinachobakia ni kuendelea kuishindania Imani kwa kujinga na ulimwengu na kutimiza wito ulioitiwa..

Lakini kama ubatizo wetu haujakamilishwa na Neno la MUNGU, hatuna budi kurudia ubatizo kwani si dhambi.

Na kumbuka matokeo ya ubatizo sahihi ni kumfanya mtu asimame imara katika IMANI, wengi waliobatizwa ubatizo sahihi baada ya toba kamili na uelewa kamili juu ya ubatizo ni ngumu kuishi tena maisha ya dhambi baada ya hapo, bali wanakuwa wanasimama maisha yao yote, kwani ubatizo unawaongezea Neema ya ziada ya kuweza kuishi bila kurudi rudi nyuma.

Mtu aliyebatizwa kwa maji mengi na kwa jina la Bwana YESU, halafu akarudi tena kwenye maisha ya dhambi kama mwanzo, basi kuna shida katika KUAMINI KWAKE tangu mwanzo, huenda hakuelewa maana ya ubatizo kabla ya kubatizwa, na hivyo hakutubu kisawasawa, lakini kama angetubu kisawasawa na akabatizwa asingeweza kurudi tena alikotoka, hiyo ndio nguvu ya ubatizo.

Ikiwa bado hujabatizwa na unahitaji kubatizwa basi wasiliana nasi kwa namba hizi, 0789001312, tutakupa mwongozo sahihi wa kujua maana ya ubatizo na hatimaye kukubatiza ikiwa utakuwa maeneo karibu na tulipo, na ubatizo ni bure.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?

AGIZO LA TOBA LINAENDANA NA UBATIZO!.

Ni sahihi kusema sikuitiwa kuhubiri ubatizo kama Paulo alivyosema (1Wakorintho 1:17)?.

Ubatizo wa moto ni upi?

Je ni lazima kupitia mafundisho ya muda mrefu kabla ya kubatizwa?

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments