Swali: Je ni vema sisi tuliookoka kushika matawi siku ya jumapili na kuingia nayo kanisani au kutembea nayo?
Jibu: Jumapili ya mitende ni jumapili moja kabla ya jumapili ya pasaka, ambapo katika historia ni siku ambayo KRISTO aliingia YERUSALEMU, na watu wakakata matawi ya mitende na kuyatandaza njiani ili Bwana YESU apite. (kumbuka, mtende ni mti unaozaa matunda ya tende).
Mathayo 21:1 “Hata walipokaribia Yerusalemu, na kufika Bethfage, katika mlima wa Mizeituni, ndipo Yesu alipotuma wanafunzi wawili akiwaambia,
2 Enendeni mpaka kijiji kile kinachowakabili, na mara mtaona punda amefungwa, na mwana punda pamoja naye; wafungueni mniletee.
3 Na kama mtu akiwaambia neno, semeni, Bwana anawahitaji; na mara huyo atawapeleka.
4 Haya yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na nabii, akisema,
5 Mwambieni binti Sayuni Tazama, mfalme wako anakuja kwako, Mpole, naye amepanda punda, Na mwana-punda, mtoto wa punda.
6 Wale wanafunzi wakaenda zao, wakafanya kama Yesu alivyowaamuru,
7 wakamleta yule punda na mwana-punda, wakaweka nguo zao juu yao, naye akaketi juu yake.
8 Watu wengi katika ule mkutano wakatandaza nguo zao njiani; NA WENGINE WAKAKATA MATAWI YA MITI, WAKAYATANDAZA NJIANI.
9 Na makutano waliotangulia, na wale waliofuata, wakapaza sauti, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la Bwana; Hosana juu mbinguni.
10 Hata alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakisema, Ni nani huyu?
11 Makutano wakasema, Huyu ni yule nabii, Yesu, wa Nazareti ya Galilaya”.
Sasa swali ni je! Na sisi ni sahihi/ruksa kuisheherekea/kuiadhimisha hii siku?
Jibu: Hatujapewa agizo lolote kwenye Biblia la kuiadhimisha jumapili ya mitende, wala jumapili ya pasaka. Isipokuwa kutokana na umuhimu wa hizo siku katika historia ya Ukristo, si vibaya kuzifanya hizo siku/tarehe kuwa za ibada ya kutafakari mambo yaliyotokea wakati huo.
Kwamfano katika jumapili ya mitende, ni wakati ambao watu walimsifu YESU kwa kumwimbia Hosana Hosana (yaani Okoa). Nasi kwa kutafakari jambo hilo twaweza kutengeneza kama igizo la wakati huo, na kumwimbia Bwana kwa furaha tukisema Hosana amebarikiwa yeye ajaye kwa jina la BWANA, kwa kufanya hivyo huku tumeshika matawi ya mitende sio kosa wala dhambi kwani ni sehemu ya sifa tu kama sifa nyingine zinazohusisha shangwe za kurusha rusha leso juu au matawi ya miti.
Lakini matawi yale yakifanyika kama ni vitu vitakatifu, (kwamba vimebeba nguvu Fulani ya kiungu, kama vile sanamu zinazowekwa kwenye baadhi ya makanisa) hilo ni kosa, kwani tayari hizo ni ibada za sanamu, na si tena kwa lengo la sifa za kumtukuza MUNGU.
Utakuta mtu anatembea na tawi lile si kwa lengo la sifa, wala tafakari ya mambo yaliyotokea miaka elfu mbili iliyopita, bali kama kisaidizi cha kuondoa mikosi, au matatizo, au cha kufukuzia wachawi n.k Huyu mtu anakuwa anafanya ibada za sanamu, na inaweza isiwe ni kosa lake bali la waliomfundisha.
Kwahiyo jumapili ya mitende si vibaya kuadhimishwa ikiwa itafanyika kwa ufunuo na maarifa namna hiyo, lakini kama itafanyika kidini na kidesturi, inageuka kuwa ibada ya sanamu, jambo ambalo ni machukizo kwa BWANA.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
AKAUKAZA USO WAKE KWENDA YERUSALEMU.
MUNGU AKETIYE MAHALI PA JUU PALIPOINUKA.
Ni mji gani mtakatifu shetani aliomchukua Bwana YESU? (Mathayo 4:5)
About the author