Katika agano la lake, iliruhusiwa Kufanya hivyo, ikiwa mtu amefiwa na ndugu yake na hana mtoto, aliruhusiwa kwenda kumwoa mke wa ndugu yake ili amwinulie uzao, lakini halikuwa kwa lengo la kimahisiano ya kindoa kana kwamba ni wapenzi. Bali kwa kusudi tu la kumwinulia uzao.
Kumbukumbu la Torati 25:5-10
[5]Watakapoketi pamoja mtu na nduguye, mmojawapo akafa, wala hana mwana wa kiume, mke wa yule aliyekufa asiolewe nje na mgeni; nduguye yule mumewe amwingilie amweke kwake awe mkewe, kumfanyia yampasayo nduguye mumewe.Â
[6]Na iwe, yule mzaliwa wa kwanza atakayemzaa, amfuate nduguye aliyekufa kwa jina lake, lisije likafutwa jina lake katika Israeli.Â
[7]Na yule mtu kwamba hapendi kumtwaa mke wa nduguye, aende huyo mke wa nduguye langoni kwa wazee, akawaambie, Nduguye mume wangu yuakataa kumsimamishia nduguye jina katika Israeli, hataki kunitimizia yampasayo nduguye mume wangu.Â
[8]Ndipo wamwite wazee wa mji wake waseme naye; naye akisimama na kusema, Sitaki mimi kumtwaa mwanamke huyu,Â
[9]ndipo mke wa nduguye amkaribie mbele ya hao wazee, amvue kiatu chake mguuni mwake, na kumtemea mate ya uso; kisha atajibu yule mwanamke, aseme, Mume akataaye kumjengea nduguye nyumba yake na afanywe hivi.Â
[10]Na jina lake katika Israeli liitwe, Nyumba ya mvuliwa kiatu.Â
Halikadhalika tunapokuja kwenye agano jipya hatuoni pia agizo lolote la moja kwa moja linalokatazama ndugu kuoa mke wa ndugu yake aliyekufa…
Zaidi inasema mwanamke Yeyote anapokuwa mjane yupo huru kuolewa na ‘Yeyote’ amtakaye katika Bwana..Â
1 Wakorintho 7:39
[39]Mwanamke hufungwa maadamu mumewe yu hai, lakini ikiwa mumewe amefariki, yu huru kuolewa na mtu ye yote amtakaye; katika Bwana tu.Â
Warumi 7:3
[3]Basi wakati awapo hai mumewe, kama akiwa na mume mwingine huitwa mzinzi. Ila mumewe akifa, amekuwa huru, hafungwi na sheria hiyo, hata yeye si mzinzi, ajapoolewa na mume mwingine.Â
Hiyo ikimaanisha kuwa anaweza akawa huru kuolewa hata na ndugu wa kaka yake (aliyefariki)…
Lakini lazima tufahamu kuwa si kila jambo linalohalalishwa kibiblia linaweza likafaa katika mazingira yote au majira yote, yapo mambo mengine ya kuzingatia, mfano utamaduni wa mahali fulani..
Kwasababu Biblia bado inatuambia…
1 Wakorintho 10:23
[23]Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vifaavyo. Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vijengavyo.Â
Kwa mfano kwa wayahudi ilikuwa ni tamaduni Watu kusalimiana kwa ‘busu’ la upendo. Lakini katika mazingira ya jamii zetu jambo kama hilo huleta ukakasi, au kutoa tafsiri nyingine hata kama nia sio mbaya..ndio maana tunaishia kipeana mikono, na ikizidi sana kukumbatiana kwa jinsia tu zinazofanana.
Â
Vivyo hivyo katika jambo hili, kuoa mke wa ndugu yako aliyefariki, kijamii halina munyu ndani yake.
Â
Hivyo twaweza sema kijamii halikubaliki, lakini kibiblia halijakatazwa..ukiniomba mimi ushauri nitakuambia usifanye hivyo..kaoe pengine..lakini ukimwoa mke wa ndugu yako aliyekufa pia hujafanya dhambi ikiwa tu, pana makubaliano kamili katika pande zote mbili, lakini pia wewe mwenye uwe haupo katika ndoa.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>Â
https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE.
Pale mwanandoa mmoja anaposhindwa kutimiza wajibu wake ufanyaje?
https://wingulamashahidi.org/2019/08/31/bwana-yesu-alikuwa-anamaanisha-nini-kusema-marko-219%e2%80%b3walioalikwa-harusini-wawezaje-kufunga-maada
About the author