Vyusa ni nini? (Ayubu 41:7)

Vyusa ni nini? (Ayubu 41:7)

Ayubu 41:7 Je! Waweza kuijaza ngozi yake na vyuma vyenye ncha, Au kichwa chake kwa vyusa?

Vyusa ni mikuki maalumu iliyoundwa kwa ajili ya kunasia samaki, ambayo wavuvi hutembea nayo, kuvizia samaki, hususani wale waliokaribia na kilele, kisha huwachoma kwa nguvu, na kuwavuta nje ya maji, na kwasababu ya ukali na mvuvi, na wepesi wa ngozi zao, mara nyingi mkuki ule hauwezi kunasuka mwilini mwao.

Sasa katika habari hiyo, ukianzia mistari ya juu hata katika sura nzima na zile zilizotangulia, ni Ni mahojiano kati ya Ayubu na Mungu, ambapo Mungu anamuuliza maswali Ayubu ayajibu, ni maswali ambayo mpaka sasa hayana majibu, mambo makuu ya Mungu na uweza wake usiofafanulika kwa ufahamu wa kibinadamu. Sasa moja ya mambo aliyokuwa anamuuliza Ayubu ni kuhusu, mnyama “Mamba”, kwa jinsi alivyomuumba kwa namna ya kipekee, tofauti na samaki wengine, Anamweleza  jinsi alivyo jasiri, asiye na woga, anamuuliza Ayubu je unaweza kutupa ndoano yako ukamvua kama vile ufanyavyo kwa samaki wengine?(Ay 41:1).

Kwa jinsi magamba yake yalivyo magumu, anasema hata upanga ukipita juu yake haumwingii..

41:26 Mtu akimpiga kwa upanga, haumwingii; Wala fumo, wala mshale, wala mkuki wenye ncha.

Ndio hapo sasa mbeleni anasema tena, je! Je unaweza kukitoba kichwa chake kwa vyusa, kama vile ufanyavyo kwa sangara, na perege? Si itakuwa sawa na unautoboa ukuta na chelewa.

Mungu kwa urefu ameeleza sifa zake mnyama huyu katika sura yote ya 41 (japo kimsingi alikuwa anamwelezea Kristo Yesu, kwa mfano wa wanyama), akimfananisha na mnyama huyu jinsi alivyokuwa thabiti kiasi kwamba hakukuwa silaha yoyote ya adui iliyompata, na jinsi alivyotisha na kuwa na nguvu za kushinda hata mauti..

Kwa uerfu wa habari hiyo fungua hapa usome>>>> SIFA ZA MAMBA YULE MKUBWA WA AYUBU.

Je! Umempokea mfalme huyu moyoni, mwenye nguvu za kutisha, asiyetikiswa na kitu chochote?. Kumbuka wokovu ni kwa faida yako mwenyewe, hakuna njia unaweza ukamshinda adui, kama Kristo hajakuficha ndani yake. Utavuliwa tu na adui kama samaki dhaifu, lakini uwapo ndani ya Kristo hakuna awezaye kukuvua. Ikiwa upo tayari kuyasalimisha maisha yako kwa Bwana Yesu..wasiliana na sisi kwa namba uzionazo mwisho wa makala hii.

Pia kwa maana za maneno mengine ya kwenye biblia fungua hapa >>>> Maana ya Maneno Kwenye Biblia

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Madongoa ni nini? (Ayubu 7:5)

Nini maana ya Selahamalekothi?

Ayubu alimaanisha nini kusema ‘nami nitarudi tena huko uchi vilevile;?

Print this post

About the author

Devis administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments