Swali: Madongoa kama inavyosomeka katika Ayubu 7:5, ni kitu gani, na ina ujumbe gani kiroho?.
Jibu: Turejee..
Ayubu 7:5 “Mwili wangu unavikwa mabuu na MADONGOA YA UDONGO; Ngozi yangu hufumba, kisha ikatumbuka tena”.
Madongoa ni udongo ulioshikamana pamoja, sawasawa na Ayubu 38:38..
Ayubu 38:38 “Wakati mavumbi yagandamanapo, Na madongoa kushikamana pamoja?”
Kikawaida ardhi yenye Madongoa haifai kwa kilimo, bali mpaka madongoa hayo yatakapovunjwa na kulainishwa, ndipo mbegu ziweze kupandwa…
Isaya 29:23 “Tegeni masikio, sikieni sauti yangu, sikilizeni mkasikie neno langu.
24 Je! Mwenye kulima alima daima, ili apande? Afunua daima MADONGOA YA NCHI YAKE, na kuyavunja?
25 Akiisha kuulainisha uso wa nchi yake, je! Hamwagi huko na huko kunde, na kutupa-tupa jira, na kuitia ngano safu safu, na shayiri mahali pake palipochaguliwa, na kusemethi karibu na mipaka yake?
26 Kwa maana Mungu wake anamwagiza vizuri na kumfundisha”.
Neno hili pia tunaweza kulisoma katika kile kitabu cha Hosea 10:11..
Ni ni nini tunachoweza kujifunza??
Kama vile ardhi yenye madongo ilivyokuwa ngumu kwa kilimo, hali kadhalika mioyo yetu inafananishwa na shamba sawasawa na ule mfano wa Mpanzi (Mathayo 13:18-23), na kama mioyo yetu ni migumu kwa namna hiyo basi ni ngumu pia kumzalia MUNGU matunda.
Mfano wa moyo wenye madongoa ni ule ulio mgumu kusikia Neno, mtu mwenye moyo wa kupuuzia, na kutokujali pale asikiapo Neno la MUNGU, mtu wa namna hii anahitaji sana kusaidiwa.
Je ni wewe mtu huyo?. Kama ndio basi mkimbilie YESU leo kwa kumaanisha kabisa naye ataufanya maoyo wako kuwa mlaini, na utayaona matunda ya BWANA.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Tufanyaje ili tuonekane tunampenda Mungu?
KWANINI NI NUHU, AYUBU NA DANIELI?
About the author