NI LAZIMA KUENDELEZA UTAKASO.

NI LAZIMA KUENDELEZA UTAKASO.

Utakaso wa ndani ni jambo endelevu.. hakuna hatua ambayo mtu amefika na kusema hapa sasa nimekamilika na sihitaji tena kujitakasa.. hakuna, lakini Biblia inatufundisha kuwa ni lazima tujitakase utu wetu wa ndani na kuwa wapya siku baada ya siku.

2Wakorintho 4:16 “Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, LAKINI UTU WETU WA NDANI UNAFANYWA UPYA SIKU KWA SIKU”.

Na tena katika Ufunuo, maandiko yanasema “Mtakatifu na azidi kutakaswa (Ufunuo 22:11)”

Sasa tunahoji kama Mtakatifu ameshakamilika kuna haja gani tena ya kuendelea kutakaswa?..Umeona?.. maana yake mtakatifu ni lazima aendelee na utakaso, ijapokuwa anaitwa “Mtakatifu” hakuna mahali atafika na kusema sasa nimekamilika..

Kila hatua ya usafi tunayoifikia inatufungua macho kuona uchafu mwingine uliopo ndani, na tunashughulika na huo, na mwingine na mwingine..mpaka siku ya ukombozi wa miili yetu (Waefeso 4:30).

Sasa twende mbele zaidi kuangalia vitu gani vinavyomtakasa mtu.

    1. ROHO MTAKATIFU.

Roho Mtakatifu ndio sabuni ya kwanza ya kuondoa uchafu ndani ya Mtu ndio maana kuna umuhimu sana wa Mtu kupokea ujazo wa Roho Mtakatifu baada ya kuamini.

1Petro 1:2 “kama vile Mungu Baba alivyotangulia kuwajua katika KUTAKASWA NA ROHO, hata mkapata kutii na kununyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani na ziongezwe kwenu”.

Soma pia 1Wakorintho 6:11 na Warumi 15:16.

Kanuni ya Ujazo wa Roho Mtakatifu ni ile tunayoisoma katika Matendo 2:37-38, yaani kutubu kwa kumaanisha kuacha dhambi na ubatizo wa maji mengi kwa jina la Bwana YESU.

    2. NENO LA MUNGU

Maneno ya MUNGU yaliyoandikwa ndani ya kitabu ya Biblia ndio sabuni ndio sabuni ya pili kumtakasa mtu maisha yake. Bwana YESU alisema, tunatakaswa na kweli ya Neno la MUNGU.

Yohana 17:17 “Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli”.

Soma pia Waefeso 5:26..

Mtu mwenye desturi ya kusoma Neno la Mungu ni lazima kila siku atakuwa anayaona makosa yake, lakini mtu asiyesoma Neno la Mungu kila siku atajiona yupo sawa na hahitaji kujitakasa wala kurekebishwa. Kwanini? Kwasababu Neno la Mungu ni kama kioo, mtu huwezi kujua uso wako upoje kama hujitazami kwenye kioo (Yakobo 1:22-23).

   3. MAOMBI.

Maombi yanatakasa utu wa ndani katika kiwango kikubwa sana.. na si tu utu wa ndani bali vitu vyote pia..

1Timotheo 4:5 “kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba”.

Kiwango cha mtu kukua kiroho pia kinapimwa na kiwango cha Maombi, mtu anayeongeza viwango vyake vya maombi kila siku ni mtu pia anayekua kiroho.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Print this post

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply