Je! Shetani anao uwezo wa kuumba, kama Mungu?

Je! Shetani anao uwezo wa kuumba, kama Mungu?

SWALI 1: Je! Shetani anaweza kuumba, kama Mungu? Kama sio Mbona kipindi cha Farao, tunaona wale waganga waliweza kuleta vyura na nyoka, kama alivyofanya Musa. Je wale vyura aliwaumbaje, uhai alitolea wapi kama sio Mungu?


JIBU:  Bwana Yesu anasema; Shetani ni mwongo, na sio tu mwongo, bali ni Baba wa huo;

Yohana 8:44 “..wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo”.

Maana yake ni kwamba ufalme wake ameujenga juu ya misingi ya uongo. Alitumia uongo kumnyang’anya Adamu nafasi yake ya umiliki. Vivyo hivyo hadi sasa anatumia uongo kuwadanganya watu wasiutambue ukweli  wote kuhusu yeye.

Anataka kuwadanganya watu, wadhani kuwa yeye ana nguvu za kuweza kukaribiana hata na Mungu au anao uwezo wa kuumba kama Mungu. Lakini ukweli ni kwamba, shetani au kiumbe chochote kile hakiwezi kuumba hata sisimizi. Uwezo huo anao Mungu tu, peke yake.

Kama ni hivyo, ni nini alikifanya kipindi cha Farao?

Alichokifanya kipindi cha Farao, si kingine zaidi ya uongo. Kutokana na maarifa aliyokuwa nayo kipindi kile ambayo anayo hadi sasa, shetani anaweza kubaliki kitu fulani kionekane ni kitu kingine mbele tu ya macho ya watu, au hata kujibadilisha yeye, aonekane ni malaika wa kweli, kumbe ndani ni yeye Yule yule shetani..Biblia inatuambia uwezo huo anao..

2Wakorintho 11:14 “Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru”.

Hivyo tabia hiyo anayo.. kipindi kile hakuumba nyoka wenye pumzi ya uhai, kama nyoka wengine, au vyura wapya..bali alifanya kazi yake hiyo ya kubadilisha maumbile ya vitu mbele ya macho ya watu.. Kwa lugha ya sasa wanaita “kiini-macho” au “mazingaumbwe”, na ndio maana nyoka wa Musa, hakuwaona wale kama ni nyoka wenzake, wanaohitaji mapambano, bali aliona kama ni chakula tu, akala.

Ni sawa na mwanadamu ambaye amefikia maarifa ya kutoa ‘photocopy’ kitu orijino, Shetani naye hapo amepafikia.Lakini hana uwezo wa kutengeneza orijino.

Kama shetani angekuwa na uwezo wa kuumba chura, hata mbwa angeweza, hata ng’ombe pia angeweza, na  sokwe nao. Na matokeo yake dunia, ingejawa na vitu vilivyoumbwa na Mungu, na vilivyoumbwa na shetani, leo hii tungesikia wale nguruwe si wa Mungu bali ni wa shetani, usiwaguse. Lakini hadi sasa hakuna rekodi ya kitu chochote kilichoumbwa na shetani, zaidi sana rekodi aliyonayo ni kuumba uovu na uasi duniani.

Pia tazama..

1 Jehanamu ni wapi?
2 Nini kinatokea baada ya kifo?
3 Freemason ni nini?
4 Siku ya unyakuo itakuwaje?
5 Upendo ni nini, je kuna aina ngapi za upendo?
6 Je! umepokea Kweli Roho Mtakatifu?
7 Mauti ya pili ni nini?
8 Faida za maombi
9 Jinsi ya kusoma biblia.
10 Je! kuna aina ngapi za malaika?

SWALI 2 : Je! Jini au pepo ni roho tu au pia wana miili inayoonekana, kiasi kwamba tunaweza kuwashika? Kama ndivyo Mbona Bwana Yesu alisema.

Luka 24:39 “Nishikenishikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo”.

JIBU: Ni kweli sawasawa na maneno ya Bwana Yesu, hakuna jini au pepo, au kiumbe chochote cha rohoni, chenye mwili, na kikaweza kuishi hapa duniani kama sisi.. Hakuna.

Kumbuka, Bwana Yesu alisema..

Mathayo 12:43 “Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate.

44 Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa.

45 Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya”.

SWALI 2 : Je! Jini au pepo ni roho tu au pia wana miili inayoonekana, kiasi kwamba tunaweza kuwashika? Kama ndivyo Mbona Bwana Yesu alisema.

Maandiko hayo ni kutuonyesha kuwa, mapepo, hayana miili yao wenyewe ya kuishia hapa duniani, yanategemea watu,au wanyama,ili kutembea duniani, kama wakati ule yalivyomwomba Bwana yawaingie wale nguruwe. Lakini yenyewe kama yenyewe, hayawezi kusimama na kuwa kama wanadamu kutembea duniani.

Lakini Je! Wale wanaoshuhudia kwamba mapepo yanawatokewa, na pengine kuzuni nao, ni nini vile?

Mapepo yanaouwezo wa kujidhihirisha mbele ya mtu kwa taswira ya kitu fulani, aidha ya mtu, au kitu, kukutisha au kukufanya uogope,  (Mathayo 14:26), au kukutokea katika ndoto,au maono.. lakini zaidi ya hapo yasiweza,  kuendelea na kuchukua maumbile na kuwa kama mwanadamu mwingine na kuishi hapa duniani, kama vile kula, kunywa, kufanyabiashara, kuoa, au kuolewa n.k. huo uwezo hawana kwasababu hawana miili. Pepo haliwezi kuzaa na wewe.

Vinginevyo, shetani angeshajidhihirisha siku nyingi na kuwa mfalme wa dunia. Lakini mpaka sasa ni roho tu, na atabakia kuwa roho, mpaka atakapotupwa kwenye ziwa la moto na mapepo yake.

Lakini kumbuka ukiwa ni mtu wa kujishughulisha na mambo ya ushirikina, aidha wewe ni mganga, au mchawi, au ulishawahi kwenda huko, ukafanyiwa matambiko, au kufanyiwa mazindiko ya kipepo, au ukala vitu vyao, Huo nao ni mlango unaoongeza wigo mkubwa sana, wa shetani au mapepo yake, kujidhihirisha kwako, kwasababu umeingizwa katika mtandao wao wa kiroho, hivyo inakuwa rahisi sana kwao kujidhihirisha kwako, na pengine kuchukua umbile ya kitu chochote kukuletea madhara mwilini. Tofauti na mtu ambaye  yupo mbali na mambo hayo.

Hivyo dawa pekee, ya kumfukuza shetani na majini yake, yasikutokee tokee au yasikufuate fuate ni kumkabidhi Yesu maisha yako. Kwa kumaanisha kabisa kuacha maisha ya dhambi, na baada ya hapo, ukazingatia kusoma NENO..

Kwasababu kuokoka ni sehemu ya kwanza, ya kuwekwa huru.. Ili kuukamilisha uhuru wako ni lazima Neno la Mungu likae ndani yako kwa wingi ili uweze kumshinda kabisa kabisa shetani.

 Biblia inasema.

Yohana 8:32 “tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru”.

Bwana Yesu, alikuwa ni mtakatifu wa Mungu, ambaye hakutenda dhambi, lakini hilo halikumzuia shetani asimjie, na kuzungumza naye. Lakini utaona alimshinda kwa Neno la Mungu lililokuwa ndani yake, na si kitu kingine.

Vivyo hivyo na wewe, ikiwa tayari umeshaokoka, Jifunze sana Neno, ujue mamlaka, na haki uliyonayo katika Msalaba wa YESU KRISTO. Hiyo itakufanya usiishi maisha ya woga,wala wasiwasi wa nguvu zozote za giza, kwasababu utakuwa tayari umeshajua uwezo uliopewa jinsi ulivyo mkubwa kuliko wa ibilisi

Lakini ukiwa ni mkristo, mvivu, Neno husomi ujue kabisa shetani ataendelea kukusumbua tu, haijalishi utakuwa ni mwombaji kiasi gani.

Hivyo zingatia hayo mambo mawili.

  1. Wokovu
  2. Neno

Ikiwa bado hujaokoka na upo tayari leo, kumpa Yesu maisha yako, ili akusamehe na kukupa wokovu, na kuyafukuza maroho yote machafu yaliyokuvamia. Basi uamuzi huo ni wa busara sana kwako, ambao hautakaa uujutie milele.

Hivyo fungua hapa, kwa mwongozo wa sala hiyo>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Je shetani ana uwezo wa kujua mawazo ya mtu?

Mjoli ni nani katika biblia?

Gombo ni nini?

WANA-NDOA: Baba Mkwe, Na mama Mkwe.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

6 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Stephen Nchimbi
Stephen Nchimbi
2 years ago

Mungu awabariki kwa mafundisho mazuri

MBONIMPA COSMAS
MBONIMPA COSMAS
2 years ago

Mungu awabariki sana

Emmanuel Buberwa Kitengule
Emmanuel Buberwa Kitengule
2 years ago

Barikiwa sana mwalimu kwa masomo mazuri.

Maige
Maige
2 years ago

Amen. Naendelea kubarikiwa na masomo haya. Mungu AWABARIKI mno.

Onesmo Zacharia
Onesmo Zacharia
2 years ago

Asanteni

kwa masomo yenu