JIBU: Kwanza, ni vizuri kufahamu kubatizwa, ni tendo la rohoni, na linapaswa litoke rohoni, kitendo cha mtu kwenda kubatizwa kwanza anapaswa awe tayari kugeuka [kutubu], kwa kumaanisha kabisa kutoka moyoni mwake, kuacha maisha ya dhambi, na kuanza maisha mapya katika Kristo…
Sasa mtu wa namna hiyo BWANA YESU KRISTO akishaona moyo wake kweli umedhamiria kugeuka, na hajafanya hivyo kama ni desturi
za kidini tu ili kutimiza wajibu, sasa moja kwa moja mtu wa namna hiyo
anapewa UWEZO WA KUSHINDA dhambi, kwasababu yeye mwenyewe hawezi. soma
Yohana 1:12 “Bali wote waliompokea ALIWAPA UWEZO wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake”
Sasa Uwezo huo hauji juu ya mtu kama hajadhamiria kabisa kuacha
dhambi zake, ikiwa na maana kudhamiria kuacha ulevi, anasa, uasherati,
utukanaji, uongo, wizi na mambo yote yanayofanana na hayo..
Hivyo kitendo cha Kubatizwa kama mtu akizingatia vigezo hivyo,
ubatizo ule unakuwa na maana kubwa sana katika maisha yake kuanzia huo
wakati na kuendelea, yeye anakuwa ni milki halali ya Kristo YESU. Ile
hatia ya dhambi Bwana anaifuta juu yake, na UWEZO wa kushinda dhambi
unaachiliwa juu yake..Kwahiyo, kitu anachopaswa kufanya sasa kuanzia huo
wakati wa kubatizwa na kuendelea, ni KUTOKUMZIMISHA ROHO WA MUNGU NDANI
YAKE….Na hii inakuja kwa kudumu katika usafi wa roho, na kujifunza Neno
la Mungu, na kukaa karibu na ndugu wa kikristo wenye Imani moja na
wewe.
Ubarikiwe.
Mada zinazoendana:
JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?
JE, KAMA HAUNA UBATIZO SAHIHI HAUWEZI KUWA NA ROHO MTAKATIFU?
WALIO NA HEKIMA NDIO WATAKAOELEWA.
ROHO I RADHI, LAKINI MWILI NI DHAIFU.
AGANO LAKO LINABEBWA NA NANI?
CHANZO CHA MAMBO.
Rudi Nyumbani:
Print this post