Kisonono kinachozungumziwa katika Mambo ya Walawi 15:2 ni kipi?

Kisonono kinachozungumziwa katika Mambo ya Walawi 15:2 ni kipi?

Jibu: Turejee..

Walawi 15:1 “Kisha Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,

2 Haya, semeni na wana wa Israeli, mkawaambie, Mtu ye yote atakapokuwa na kisonono kimtokacho mwilini mwake, atakuwa najisi kwa ajili ya kisonono chake.

3 Na unajisi wake katika kisonono chake ni huu; kama mwili wake unachuruzika kisonono chake, au kama kisonono chake kimezuiwa mwilini mwake, ni unajisi wake.

4 Kitanda cho chote akilaliacho mwenye kisonono kitakuwa najisi; na kitu cho chote ambacho akiketia kitakuwa najisi”.

Moja ya magonjwa yaliyotajwa kwenye biblia ni pamoja na huu wa “kisonono” lakini kisonono hiki ni Zaidi ya hiki tukujuacho ambacho kipo mingoni mwa magonjwa ya zinaa (Maarufu kama Gonorrea).

Mistari mingine iliyotaja ugonjwa huo ni (Walawi 22:14 na Hesabu 5:2)

Kisonono kilichozungumzwa katika biblia ni mjumuiko wa magonjwa yote yanayosababisha kutokwa na uchafu katika njia za haja ndogo (kwa jinsia zote), yawe yanasababishwa na zinaa, au yasiyosababishwa na zinaa….na uchafu huo ni pamoja na (usaha, damu au mchanganyiko).

Kwahiyo katika biblia mtu yeyote aliyetokwa na chochote kati ya hivyo katika viungo vyake vya uzazi alihesabika kuwa na kisonono na alikuwa najisi mpaka atakapopona ugonjwa huo (hawezi kukusanyika katika kusanyiko la Bwana, na alikuwa anatengwa).

Lakini je hata sasa mtu wa namna hii anapaswa kutengwa?

Katika agano jipya hakuna agizo la kuwatenga wagonjwa wa aina yoyote, au wanawake walio katika mzunguko wa hedhi. Wote wanaweza kukusanyika katika nyumba ya Mungu (kwasababu kimtokacho mtu katika mwili hakimtii unajisi, bali kile kimtokacho kutoka moyoni, ndicho kinachomtia mtu unajisi, sawasawa na Marko 7:20-22).

Marko 7:20  “Akasema, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi.

21  Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati,

22  wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.

23  Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi”.

Ikiwa mtu huyo amejitakasa moyoni kwa viwango vya kustahili kumfanyia Mungu ibada, hata akiwa na maradhi mwilini, bado ibada yake itapokelewa na Bwana.

Ikiwa kisonono mtu alichokipata ni matokeo ya zinaa, huyu mtu anapaswa atubie kwanza zinaa yake aliyoifanya kwa kumaanisha kuacha hiyo dhambi (kwa ufupi aokoke), na baada ya toba akiwa katika hatua za kutafuta uponyaji, anaweza kujumuika na wengine katika majumuiko ya kumwabudu Mungu.

Vile vile ikiwa ameupata kwa njia nyingine isiyohusisha zinaa, atajitakasa nafsi yake kwa toba na rehema kwa makosa mengine na atajiunga na wengine katika kumwabudu Mungu.

Mwisho: Mshahara wa dhambi ni mauti..ikimbie dhambi, na sehemu salama ya kukimbilia ili upate msaada ni msalabani, kwasababu msaada kamili upo msalaban, Kama hujampokea Bwana YESU upo hatarini…na hauwezi kushindana na dhambi.

Ni heri leo ukayasalimisha maisha yako kwake, na yeye atakuokoa.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

FAHAMU ZA WATU HUWA ZINAONDOLEWA NA NINI?

Tatizo la Bawasiri kibiblia

Je mwanamke anaruhusiwa kupanda madhabahuni akiwa katika siku zake?

JINSI UNAJISI UNAVYOMGHARIMU MTU.

Tofauti kati ya makuhani na walawi ni ipi?

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments