SWALI: Na je! Walawi na makuhani katika kanisa la sasa ni watu wa namna gani?
JIBU: Mungu alilichagua kabila moja kati ya kumi na mbili liwe kabila lake takatifu litakalosimama katika kazi na shughuli zote za kidini na ibada Israeli.
Sasa katikati ya hawa walawi ndipo walipotolewa makuhani ndani yake. Hivyo makuhani wote walikuwa ni walawi lakini walawi wote si makuhani.
Kwasasa, kila mkristo, ni Mlawi. Kwasababu tayari ameshapewa uwezo ndani yake na karama, ya kuifanya kazi ya Mungu pale tu anapookoka. Kila mmoja ni kiungo kwa mwenzake ndani ya kanisa. Lakini mkristo anabadilika kutoka kuwa mlawi mpaka kuwa kuhani pale anaposimama hasaa kwa ajili ya huduma/kazi ya Mungu kwa watu wake.
Anapobeba maono Fulani, labda tuseme kulichunga kanisa, huyo ni kuhani wa Mungu, na hivyo anaposimama na kuwabariki watu basi Baraka hizo huwafikia watu moja kwa moja kutoka kwa Mungu, mfano tu wa makuhani wa agano la kale. Au anapotumika katika kuwafundisha, kuwaombea wengine, kuwasimamia wengine, haijalishi ngazi aliyopo, au mahali au jinsia, huyo rohoni ni kuhani wa Mungu.
Hivyo kila mkristo anaouwezo wa kuwa kuhani wa Mungu, kwasababu lengo la Mungu ni sote tuwe makuhani wake, sio tu walawi, Na Yesu Kristo Bwana wetu akiwa ni kuhani Mkuu.
1Petro 2:9 Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;
Bwana akubariki.
Je! Kristo yupo moyoni mwako?
Kama ni hapana, basi wakati ndio huu, mgeukie, akusamehe dhambi zako, kwa kutubu na kumaanisha kabisa kuziacha, naye atakukomboa. Ikiwa upo tayari kwa ajili ya mwongozo huo, basi waweza fungua hapa kwa mwongozo >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Kwa namna gani tumefanyika Makuhani na Ufalme?.(Ufunuo 1:6)
WALAWI WALIKUWA WENYE MIOYO YA ADILI KWA KUJITAKASA KULIKO MAKUHANI.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
Kwanini Yesu aliwaambia wale wakoma wakajionyeshe kwa makuhani?
About the author