JE UPO NDANI YA YESU?

JE UPO NDANI YA YESU?

Yohana 15:7 “Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa”.

Je unaelewa maana ya kukaa ndani ya YESU (kuwepo ndani ya YESU) ??kwasababu ipo tofauti ya Bwana YESU kukaa ndani yako, na wewe kukaa ndani yake.

Kukaa ndani si Kumpa YESU maisha yako!!!…Ni zaidi ya hapo!.

Je ulishawahi kusikia mtu akisema “fulani nimemtoa ndani yangu kabisa au moyoni”..??

Utakuwa unaelewa maana ya hiyo kauli kwamba huenda katendewa kitendo kibaya sana, au cha kuumiza au kudhalilisha…ikasababisha kumtoa huyo mru moyoni kabisa.

Vile vile kuna mtu utamsikia akisema “mtu fulani yupo sana moyoni mwangu”…

Maana yake mpaka kusema hivyo huenda huyo mtu kamfanyia jambo jema sana au la kugusa moyo wake, au la kumvutia, mpaka kufanya aingie moyoni mwake.

Na Bwana YESU ni hivyo hivyo, kuna watu wapo ndani yake (moyoni mwake)..na kuna watu hawapo kabisa moyoni mwake ijapokuwa wanaweza kukiri wanaye…

Kwanini?..

Jibu: Kwasababu hawajawahi kuugusa moyo wa Bwana hata kumfanya Bwana awaweke moyoni mwake..watu hawa kibiblia hawapo ndani ya YESU na Kristo ingawa wanaweza kukiri kwamba wanaye Kristo moyoni, na Bwana atawakana siku ile kwamba hawajui.

Mathayo 7:21 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.

22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?

23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”.

Yafuatayo ni mambo (Matendo) ambayo mtu anaweza  kuyafanya yakaugusa moyo wa Bwana YESU , hata kumfanya mtu huyo awe ndani ya KRISTO (moyoni mwake).

  1. KUSHIRIKI MEZA YA BWANA.

Hili ni jambo la kwanza linalomzamisha mtu kwenye moyo wa KRISTO.

Yohana 6:56 “Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake.

57 Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi”.

Kamwe usiidharau meza ya Bwana, lakini pia hakikisha unashiriki kulingana na Neno lake..Kwa kufanya hivyo utauteka moyo wa Bwana kwa kiwango kikubwa sana.

2.UMOJA.

Hili ni jambo la pili linalouteka moyo wa Bwana sana na kumzamisha mtu ndani ya moyo wake.

Yohana 17:21 “Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.

22 Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja.

23 Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi”.

Hivyo jenga sana desturi ya kutafuta Umoja wa Roho, usipende kukaa peke yako peke yako (huendi kanisani, hushirikiani na wengine..ni hatari kubwa sana).

3. MATOLEO.

Kumtolea Mungu kwa hiari pasipo kulazimishwa wala kushinikizwa, ni kitendo cha tatu kinachougusa sana Moyo wa Bwana (hauwezi kutoka moyoni mwake daima).

Mathayo 26:12 “Maana kwa kunimwagia mwili wangu marhamu hiyo, ametenda hivyo ili kuniweka tayari kwa maziko yangu.

13 Amin, nawaambieni, Kila patakapohubiriwa Injili hii katika ulimwengu wote, tendo hilo alilolitenda huyu litatajwa pia kwa kumbukumbu lake”.

Huyu mwanamke amekuwa ndani ya moyp wa Kristo kwa vizazi vyote, mpaka sasa tunavyozungumza.

Usikwepe matoleo (sadaka) shetani amevuruga sana eneo hili la matoleo kwasababu anajua endapo mtu akipata ufunuo mkamilifu basi ataingia ndani ya Kristo moja kwa moja.

  1. UNYENYEKEVU.

Unyenyekevu ni wa kukiri makosa, na kurudi kitubu na kuyokurudia rudia machafu, ni tendo kubwa sana linamwingiza mtu ndani ya YESU.

Luka 23:40 “Lakini yule wa pili akamjibu akamkemea, akisema, Wewe humwogopi hata Mungu, nawe u katika hukumu iyo hiyo?

41 Nayo ni haki kwetu sisi, kwa kuwa tunapokea malipo tuliyostahili kwa matendo yetu; bali huyu hakutenda lo lote lisilofaa.

42 Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.

43 Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi”

Na yapo mambo mengine mengi katika maandiko yanayomwingiza mtu na kumdumisha ndani ya KRISTO.

Zifuatazo ni faida za kuwa ndani ya KRISTO.

  1. Lolote tuombalo tunapata.

Yohana 15:7 “Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa”

    2.Tunakuwa viumbe vipya.

2 Wakorintho 5:17 “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya”.

Hasara za kutokuwa ndani ya KRISTO ni kinyume cha faida hizo.

Bwana atusaidie tuingie na kudumu ndani yake.

Maran atha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NITASHINDAJE HALI YA KUUMIZWA NA MANENO YA WATU!

USIWE MKRISTO WA KUKAA TU GHALANI,

JE UPANGA UMEINGIA MOYONI MWAKO?.

JINSI YA KUPIGANA MAOMBI YA VITA.

JINSI YA KUEPUKA KUUMIZWA MOYO KUSIKOKUWA NA SABABU.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments