Yesu ni nani? Hili ni swali ambalo sio tu linawachanganya watu wengi wa leo, lakini pia limekuwa ni swali lililowasumbua watu wengi tangu enzi na enzi vizazi na vizazi huko nyuma, hata tangu wakati Bwana Yesu mwenyewe akiwa hapa duniani utaona siku moja aliwauliza wanafunzi wake nao swali kama hilo,
Mathayo 16:13 “Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani? 14 Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii. 15 Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?
Mathayo 16:13 “Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani?
14 Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii.
15 Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?
Unaona, hata leo hii tu angekuwepo duniani angetuuliza na sisi swali hilo hilo, tunamnena yeye kama nani, ni wazi utasikia kila mtu anatoa jibu lake wengine utawasikia watasema, ni mjumbe wa Mungu, wengine watasema ni mmojawapo wa mitume wa Mungu, wangine watasema alikuwa ni nabii wa Mungu, wengine watasema ni mkombozi, wengine watasema ni Mungu…nk. N.k
Lakini Je hiyo inamaanisha mitazamo yao wote haipo sawa?, jibu ni hapana, wanaweza wakawa sawa mahali fulani lakini si sawa kulingana na Mungu anavyotaka watu wamjue Yesu kama nani..Ni sawa tu na leo usimame na boss labda tuseme mbele ya watu 1000 tofauti tofauti, na ukasema kila mmoja aanze kumzungumzia , hutashangaa katikati ya huo mkutano wengine wakimwita, mjomba, wengine wakimwita rafiki, wengine wakimwita baba, wengine wakimwita binamu, wengine wakimwita jirani, wengine wakimwita mwenyekiti, wengine wakimwita shemeji, wengine wakimwita mwenetu n.k…
Hapo utaona akiitwa kila aina ya cheo ambacho hujawahi kutazamia kwamba anaweza akawa nacho boss wako, sasa hapo huwezi kusema hawapo sawa kisa tu kwasababu hukumsikia hata mmoja wao akimwita boss, wao kila mmoja alimwita kulingana na mahusiano aliyonayo naye..ikiwa ni mtoto wake alisimama mbele yake hawezi kumwita shemeji au boss ni lazima atamwita Baba tu..
Lakini hata kama wapo sawa kiasi gani, Bado hawapo sawa kulingana na wewe unavyotaka watu wale wamjue kama boss.
Na vivyo hivyo kwa Bwana Yesu, wengi wanamjua kama mtume wa Mungu, na kweli ndivyo alivyo yeye ndiye mtume mkuu, wengi wanamjua kama nabii, na ni kweli ndivyo ilivyo yeye alikuwa ni nabii mkuu, wengine wanamjua kama kiongozi na kweli ndivyo alivyo, vile vile wengine wanamjua kama Mungu mwenyewe aliyeuchua mwili na kuishi na sisi duniani, na kweli ndivyo ilivyo maandiko mengi yanathibitisha hilo kuwa YESU ndiye Mungu mwenyewe katika mwili wa kibinadamu..lakini swali linakuja pale pale Je! Mungu anataka sisi tumjue YESU kama nani?.
Sasa tukiendelea kusoma pale chini tunaona Petro anamjibu Bwana maneno haya:
15 Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani? 16 Simoni Petro akajibu akasema, WEWE NDIWE KRISTO, MWANA WA MUNGU ALIYE HAI. 17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni. 18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.”Unaona Ufunuo aliopata Petro juu ya YESU kama KRISTO, aliyekuja kama mwana wa Mungu, ndio aliokuwa anauhitaji na ndio kwa kupitia huo huo YESU amelijengea kanisa lake na milango ya kuzimu haiwezi kulishinda.
16 Simoni Petro akajibu akasema, WEWE NDIWE KRISTO, MWANA WA MUNGU ALIYE HAI.
17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.
18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.”Unaona Ufunuo aliopata Petro juu ya YESU kama KRISTO, aliyekuja kama mwana wa Mungu, ndio aliokuwa anauhitaji na ndio kwa kupitia huo huo YESU amelijengea kanisa lake na milango ya kuzimu haiwezi kulishinda.
Hivyo hatupaswi kuhangaika sana, kutafuta kumjua YESU ni nani? Tukianza kumchambua hatutammaliza, lakini biblia imetupa mwongozo mwepesi uliomwelezea yeye kwamba tumjue yeye kama KRISTO, maana ya neno Kristo ni mtiwa mafuta, yaani mtu aliyetiwa mafuta kuwakomboa wanadamu,..hivyo tukishamjua YESU kama mkombozi huo ni ufunguo mkubwa sana uliobeba vyeo vyake vingine vyote vilivyobakia.. Kwamba yeye ndio njia ya kwenda mbinguni, na mtu hawezi kufika kwa Mungu pasipo kupitia yeye.
Hivyo ukiulizwa leo YESU ni nani, jibu tayari lipo yeye ni KRISTO, yaani mkombozi wa ulimwengu, hilo linatosha kumwelezea yeye..Na mtu yeyote akimwelewa kwa namna hiyo hivyo akamruhusu ayakomboe maisha yake basi ajue kuwa shetani atagonga mwamba, tiketi ya kwenda mbinguni ipo mikononi mwake.
Ubarikiwe.
Mada Nyinginezo:
KWANINI YESU KRISTO ALIKUJA DUNIANI?
KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?
JINA LA MUNGU NI LIPI?
UBATILI.
RACA
KWANINI AWE NI PUNDA NA MWANA-PUNDA?
MUNGU MWENYE HAKI.
Rudi Nyumbani:
Print this post